bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Proverbs 10
Proverbs 10
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 11 →
1
Hizi ni methali za Solomoni: Mtoto mwenye hekima ni furaha ya baba yake; lakini mtoto mpumbavu ni huzuni ya mama yake.
2
Mali iliyopatikana kwa njia mbaya haifai, lakini uadilifu huokoa mtu kutoka kifoni.
3
Mwenyezi-Mungu hawaachi waadilifu wapate njaa, lakini huzipinga tamaa za waovu.
4
Uvivu husababisha umaskini, lakini mkono wa mtu wa bidii hutajirisha.
5
Mwenye busara hukusanya wakati wa mavuno, kulala wakati wa kuvuna ni aibu.
6
Mwadilifu hujiletea baraka yeye mwenyewe, lakini kinywa cha mwovu kimesongwa na ukatili.
7
Waadilifu hukumbukwa kwa baraka, lakini waovu watasahaulika kabisa.
8
Mwenye hekima moyoni hutii amri, lakini mpumbavu aropokaye ataangamia.
9
Aishiye kwa unyofu huishi salama, apotoshaye maisha yake atagunduliwa.
10
Akonyezaye kwa nia mbaya huzusha taabu, lakini aonyaye kwa ujasiri huleta amani.
11
Kinywa cha mwadilifu ni chemchemi ya uhai, lakini kinywa cha mwovu kimesongwa na ukatili.
12
Chuki huzusha ugomvi, lakini upendo hufunika makosa yote.
13
Kinywani mwa mwenye ufahamu mna hekima, lakini wasio na akili watachapwa viboko mgongoni.
14
Wenye hekima huhifadhi maarifa, lakini kuropoka kwa mpumbavu huleta maangamizi haraka.
15
Mali ya tajiri ndio ngome yake, umaskini wa maskini humletea maangamizi.
16
Tuzo la mtu mwema ni uhai, lakini mwovu huishia katika dhambi.
17
Anayekubali maonyo anaelekea kwenye uhai, lakini anayekataa kuonywa amepotoka.
18
Amchukiaye mwingine kwa siri ni mnafiki, anayemsingizia mtu ni mpumbavu.
19
Penye maneno mengi hapakosekani makosa, lakini aneyeuzuia ulimi wake ana busara.
20
Maneno ya mwadilifu ni kama fedha bora; akili ya mtu mwovu haina thamani yoyote.
21
Maneno ya mwadilifu huwafaa watu wengi, lakini wapumbavu hufa kwa kukosa akili.
22
Baraka za Mwenyezi-Mungu ndizo ziletazo fanaka, juhudi za mtu haziongezi hapo chochote.
23
Kwa mpumbavu kutenda maovu ni kama mchezo; lakini watu wenye busara hufurahia hekima.
24
Anachoogopa mtu mwovu ndicho kitakachompata, lakini anachotamani mwadilifu ndicho atakachopewa.
25
Kimbunga hupita na mwovu hutoweka, lakini mwadilifu huimarishwa milele.
26
Kama ilivyo siki kwa meno au moshi machoni, ndivyo alivyo mvivu kwa bwana wake.
27
Kumcha Mwenyezi-Mungu hurefusha maisha, lakini miaka ya waovu itakuwa mifupi.
28
Tumaini la mwadilifu huishia kwenye furaha, lakini tazamio la mwovu huishia patupu.
29
Mwenyezi-Mungu ni ngome ya wanyofu, lakini watendao maovu atawaangamiza.
30
Waadilifu kamwe hawataondolewa nchini, lakini waovu hawatakaa katika nchi.
31
Kinywa cha mwadilifu hutoa mambo ya hekima, lakini ulimi wa mtu mbaya utakatiliwa mbali.
32
Midomo ya waadilifu hujua yanayokubalika, lakini vinywa vya waovu husema tu maovu.
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 11 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31