bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Proverbs 4
Proverbs 4
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 5 →
1
Wanangu, sikilizeni mwongozo wa baba yenu, tegeni sikio mpate kuwa na akili.
2
Maana ninawapa maagizo mema, msiyakatae mafundisho yangu.
3
Mimi pia nilikuwa mtoto mwenye baba, nilikuwa mpole, kipenzi cha mama yangu.
4
Baba yangu alinifundisha hiki: “Zingatia kwa moyo maneno yangu, shika amri zangu nawe utaishi.
5
Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usisahau wala kupuuza maneno yangu.
6
Usimwache Hekima, naye atakutunza; umpende, naye atakulinda.
7
Jambo la msingi ni kujipatia hekima; toa vyote ulivyonavyo ujipatie akili.
8
Mthamini sana Hekima, naye atakutukuza; ukimshikilia atakupa heshima.
9
Atakuvika kilemba kizuri kichwani pako, atakupa taji maridadi.”
10
Mwanangu, sikia na kuyapokea maneno yangu, ili upate kuwa na miaka mingi ya kuishi.
11
Nimekufundisha njia ya hekima, nimekuongoza katika njia nyofu.
12
Ukitembea hatua zako hazitazuiwa, wala ukikimbia hutajikwaa.
13
Zingatia mafundisho ya Hekima na usimwache aponyoke, mshike kwa makini maana yeye ni uhai wako.
14
Usijiingize katika njia ya waovu, wala usifuate mwenendo wa watu wabaya.
15
Iepe njia hiyo wala usiikaribie; jiepushe nayo, uende zako.
16
Waovu kamwe hawalali wasipotenda uovu; hawapati usingizi wasipomkwaza mtu.
17
Maana uovu ndicho chakula chao, ukatili ndiyo divai yao.
18
Njia ya watu wema ni kama nuru ya alfajiri, ambayo hungaa zaidi na zaidi hata mchana kamili.
19
Lakini njia ya waovu ni kama giza nene, hawajui kinachowafanya wajikwae.
20
Mwanangu, sikiliza kwa makini maneno yangu, itegee sikio misemo yangu.
21
Usiyaache yatoweke machoni pako, yahifadhi ndani ya moyo wako.
22
Maana hayo ni uhai kwa mtu anayeyapata, ni dawa kwa mwili wake wote.
23
Linda moyo wako kwa uangalifu wote, maana humo zatoka chemchemi za uhai.
24
Tenga mbali nawe lugha potovu; wala midomo yako isitamke maneno madanganyifu.
25
Uyaelekeze macho yako mbele kwa ujasiri, mtazamo wako uwe mbele moja kwa moja.
26
Fikiria njia utakayochukua, na hatua zako zote zitakuwa kamili.
27
Usigeukie kulia wala kushoto; epusha mguu wako mbali na uovu.
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31