bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Proverbs 13
Proverbs 13
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 14 →
1
Mtoto mwenye hekima husikia maagizo ya baba yake, lakini mwenye dharau hasikilizi maonyo.
2
Mtu mwema hupata mema kutokana na maneno yake, lakini wadanganyifu huishi kwa ukatili.
3
Achungaye mdomo wake huyahifadhi maisha yake, anayeropoka ovyo hujiletea maangamizi.
4
Mvivu hutamani lakini hapati chochote, hali mwenye bidii hujaliwa riziki kwa wingi.
5
Mwadilifu huuchukia uongo, lakini mwovu hutenda kwa aibu na fedheha.
6
Uadilifu huwalinda wenye mwenendo mnyofu, lakini dhambi huwaangusha waovu.
7
Baadhi hujidai kuwa matajiri kumbe hawana kitu; wengine hujiona kuwa maskini hali wana mali tele.
8
Fidia ya mtu ni mali yake, lakini maskini hana cha kutishwa.
9
Mwadilifu hungaa kama taa iwakayo vizuri, lakini waovu ni kama taa inayozimika.
10
Kiburi husababisha tu ugomvi, lakini kwa wanaokubali shauri jema mna hekima.
11
Mali ya harakaharaka hutoweka, lakini akusanyaye kidogokidogo ataiongeza.
12
Tumaini la kungojangoja huumiza moyo, lakini tazamio linalotimia ni mti wa uhai.
13
Anayedharau mawaidha anajiletea maangamizi, lakini anayetii amri atapewa tuzo.
14
Mafundisho ya wenye hekima ni chemchemi ya uhai; humwezesha mtu kuiepa mitego ya kifo.
15
Kuwa na akili huleta fadhili, lakini njia ya waovu ni ya taabu
16
Mwenye busara hutenda kila kitu kwa akili, lakini mpumbavu hutembeza upumbavu wake.
17
Mjumbe mbaya huwatumbukiza watu taabuni, lakini mjumbe mwaminifu huleta nafuu.
18
Umaskini na fedheha humpata asiyejali mafundisho, lakini mwenye kusikia maonyo huheshimiwa.
19
Inafurahisha upatapo kile unachotaka, kwa hiyo wapumbavu huchukia kuepa uovu.
20
Anayeandamana na wenye hekima hupata hekima, lakini anayejiunga na wapumbavu atapata madhara.
21
Watendao dhambi huandamwa na balaa, lakini waadilifu watatuzwa mema.
22
Mtu mwema huwaachia urithi uzao wake, lakini mali ya mwenye dhambi imerundikiwa waadilifu.
23
Shamba la maskini hutoa mazao mengi, lakini bila haki hunyakuliwa.
24
Asiyemwadhibu mtoto wake hampendi; lakini ampendaye mwanawe humrudi mapema.
25
Mwadilifu anacho chakula cha kumtosheleza, lakini tumbo la waovu hutaabika kwa njaa.
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 14 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31