bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Proverbs 20
Proverbs 20
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 21 →
1
Divai huleta dhihaka na kileo huleta ugomvi; yeyote anayevutiwa navyo hana hekima.
2
Ghadhabu kali ya mfalme ni kama simba angurumaye; anayemkasirisha anayahatarisha maisha yake.
3
Ni jambo la heshima kuepa ugomvi; wapumbavu ndio wanaogombana.
4
Mvivu halimi wakati wa kulima; wakati wa mavuno atatafuta asipate chochote.
5
Fikira za mtu zimefichika kama kilindi cha maji; lakini mtu mwenye busara ajua kuzichota humo.
6
Watu wengi hujivunia kuwa wema, lakini mwaminifu wa kweli apatikana wapi?
7
Mtu mwadilifu akiishi kwa unyofu; watoto wake atakaowaacha watabarikiwa.
8
Mfalme mwema aketipo kutoa hukumu, huupepeta uovu wote kwa macho yake.
9
Nani athubutuye kusema: “Nimeutakasa moyo wangu; mimi nimetakasika dhambi yangu?”
10
Mizani ya udanganyifu na vipimo vya udanganyifu, vyote ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu.
11
Hata mtoto hujulikana kwa matendo yake, kama tabia yake ni njema na aminifu.
12
Sikio lisikialo na jicho lionalo, yote mawili kayafanya Mwenyezi-Mungu.
13
Usipende kulala tu usije ukawa maskini; uwe macho nawe utakuwa na chakula kingi.
14
“Hakifai, hakifai”, mnunuzi hulalamika, lakini akiondoka hujisifu amepunguziwa bei.
15
Kuna dhahabu na wingi wa mawe ya thamani kubwa; lakini cha thamani kubwa zaidi ni maneno ya busara!
16
Mtu akiahidi mbele yako kumdhamini mgeni, chukua nguo yake; mfanye awajibike kwa kuwadhamini wageni.
17
Chakula kipatikanacho kwa udanganyifu ni kitamu, lakini baadaye huwa kama mchanga kinywani.
18
Mipango mizuri hufanyika kwa kushauriana; ukitaka kuanza vita lazima kutafakari kwanza.
19
Mpiga domo hafichi siri, kwa hiyo mwepe mtu wa kuropoka.
20
Anayemlaani baba yake au mama yake, mwanga wa uhai wake utazimwa kama taa gizani.
21
Mali iliyopatikana kwa haraka mwanzoni, haitakuwa ya heri mwishoni.
22
Usiseme, “Nitalipiza ubaya niliotendewa.” Mtegemee Mwenyezi-Mungu naye atakusaidia.
23
Mizani ya udanganyifu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, na vipimo visivyo halali ni kitu kibaya.
24
Hatua za mtu huongozwa na Mwenyezi-Mungu; awezaje binadamu kujua njia ya kwenda?
25
Ni hatari kusema kwa mzaha “Usiahidi kumpa Mungu kitu bila kufikiri, la sivyo utaanza kusikitika baada ya nadhiri yako.”
26
Mfalme mwenye busara huwapepeta waovu; huwaadhibu bila huruma.
27
Dhamiri ya mtu ni taa ya Mwenyezi-Mungu; huchunguza nafsi yake mtu mpaka ndani kabisa.
28
Wema na uaminifu humkinga mfalme; utawala wake huimarishwa kwa uadilifu.
29
Fahari ya vijana ni nguvu zao, uzuri wa vikongwe ni mvi za uzee.
30
Mapigo yanayoumiza ni dawa ya kuondoa uovu; viboko husafisha nafsi mpaka ndani kabisa.
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 21 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31