bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Proverbs 31
Proverbs 31
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 30
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
1
Maneno ya mfalme Lemueli. Mawaidha aliyofundishwa na mama yake:
2
Nikuambie nini mwanangu? Nikuambie nini mwanangu niliyekuzaa? Nikuambie nini wewe niliyekuomba kwa Mungu?
3
Usimalize nguvu zako kwa wanawake, usiwape mali yako hao wanaoangamiza wafalme.
4
Haifai ee Lemueli, haifai wafalme kunywa divai, wala wakuu kutamani vileo.
5
Wakinywa watasahau maagizo ya sheria, na kuwanyima haki wenye taabu.
6
Mpe kileo mtu anayekufa, wape divai wale wenye huzuni tele;
7
wanywe na kusahau umaskini wao, wasikumbuke tena taabu yao.
8
Lakini wewe, lazima useme kwa ajili ya wote walio bubu; na kutetea haki za wote wasiojiweza.
9
Sema kwa ajili yao na kuamua kwa haki, linda haki za maskini na fukara.
10
Mke mwema kweli, apatikana wapi? Huyo ana thamani kuliko johari!
11
Mumewe humwamini kwa moyo, kwake atapata faida daima.
12
Kamwe hamtendei mumewe mabaya, bali humtendea mema maisha yake yote.
13
Hutafuta sufu na kitani, na kufanya kazi kwa mikono yake kwa bidii.
14
Yeye ni kama meli za biashara: Huleta chakula chake kutoka mbali.
15
Huamka kabla ya mapambazuko, akaitayarishia jamaa yake chakula, na kuwagawia kazi watumishi wake.
16
Hufikiria kununua shamba, kisha hulinunua, na kulima zabibu kwa faida ya jasho lake.
17
Huwa tayari kufanya kazi kwa nguvu na kuiimarisha mikono yake.
18
Hutambua kwamba shughuli zake zina faida; hufanya kazi hata usiku kwa mwanga wa taa yake.
19
Husokota nyuzi kwa mikono yake mwenyewe, kwa vidole vyake mwenyewe husuka nguo zake.
20
Huufungua mkono wake kuwapa maskini, hunyosha mkono kuwasaidia fukara.
21
Hawahofii watu wake ijapo baridi ya kipupwe, maana kila mmoja anazo nguo za kutosha.
22
Hujitengenezea matandiko, mavazi yake ni ya zambarau ya kitani safi.
23
Mume wake ni mtu mashuhuri barazani, anakoshiriki vikao vya wazee wa nchi.
24
Mwanamke huyo hutengeneza nguo na kuziuza, huwauzia wafanyabiashara mishipi.
25
Nguvu na heshima ndizo sifa zake, hucheka afikiriapo wakati ujao.
26
Hufungua kinywa kunena kwa hekima, huwashauri wengine kwa wema.
27
Huchunguza yote yanayofanyika nyumbani mwake, kamwe hakai bure hata kidogo.
28
Watoto wake huamka na kumshukuru, mumewe huimba sifa zake.
29
Husema, “Wanawake wengi wametenda mambo ya ajabu, lakini wewe umewashinda wote.”
30
Madaha huhadaa na uzuri haufai, bali mwanamke amchaye Mwenyezi-Mungu atasifiwa.
31
Jasho lake lastahili kulipwa, shughuli zake hazina budi kuheshimiwa popote.
← Chapter 30
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31