bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Proverbs 7
Proverbs 7
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 8 →
1
Mwanangu, yashike maneno yangu, zihifadhi kwako amri zangu.
2
Zifuate amri zangu nawe utaishi; yalinde mafundisho yangu kama mboni ya jicho lako.
3
Yafunge vidoleni mwako; yaandike moyoni mwako.
4
Iambie Hekima: “Wewe ni dada yangu”, na Busara “Wewe ni rafiki yangu”.
5
Vitakulinda mbali na mwanamke mbaya, vitakuepusha na maneno matamu ya mwanamke mgeni.
6
Siku moja dirishani mwa nyumba yangu, nilichungulia nje kupitia viunzi vya dirisha,
7
nikawaona vijana wengi wajinga, na mmoja hasa aliyekuwa mpumbavu.
8
Huyo alikuwa akitembea kwenye barabara ile, karibu na kona alikoishi mwanamke fulani. Basi akashika njia iendayo nyumbani kwa mwanamke huyo.
9
Ilikuwa yapata wakati wa jioni, giza na usiku vilikuwa vimeanza kuingia.
10
Punde kijana akakutana na huyo mwanamke; amevalia kama malaya, ana mipango yake.
11
Alikuwa mwanamke wa makelele na mkaidi; miguu yake haitulii nyumbani:
12
Mara barabarani, mara sokoni, katika kila kona ya njia hakosekani akivizia.
13
Alimkumbatia kijana huyo na kumbusu, na kwa maneno matamu, akamwambia:
14
“Ilinilazimu kutoa tambiko zangu; leo hii nimekamilisha nadhiri yangu.
15
Ndio maana nimetoka ili nikulaki, nimekutafuta kwa hamu nikakupata.
16
Nimetandika kitanda changu vizuri, kwa shuka za rangi za kitani kutoka Misri.
17
Nimekitia manukato, manemane, udi na mdalasini.
18
Njoo tulale pamoja mpaka asubuhi; njoo tujifurahishe kwa mahaba.
19
Mume wangu hayumo nyumbani, amekwenda safari ya mbali.
20
Amechukua bunda la fedha; hatarejea nyumbani karibuni.”
21
Alimshawishi kwa maneno mengi ya kubembeleza; kijana akashawishika kwa maneno yake matamu.
22
Hapo akamfuata huyo mwanamke moja kwa moja, kama ng'ombe aendaye machinjioni, kama paa arukiaye mtegoni.
23
Hakutambua kwamba hiyo itamgharimu maisha yake, mpaka alipojikuta amekuwa kama amechomwa mshale moyoni, amekuwa kama ndege aliyenaswa wavuni.
24
Sasa wanangu, nisikilizeni; yategeeni sikio maneno ya kinywa changu.
25
Msikubali kuongozwa na mwanamke kama huyo, wala msipitepite katika mapito yake.
26
Maana amewaangusha wanaume wengi; ni wengi mno hao aliowachinja.
27
Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, ni mahali pa kuteremkia mautini.
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31