bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Proverbs 3
Proverbs 3
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 4 →
1
Mwanangu, usiyasahau mafundisho yangu, bali kwa moyo wako uzishike amri zangu.
2
Maana yatakupa wingi wa siku, maisha marefu na fanaka kwa wingi.
3
Utii na uaminifu visitengane nawe. Vifunge shingoni mwako; viandike moyoni mwako.
4
Hivyo utakubalika na kusifika, mbele ya Mungu na mbele ya wanadamu.
5
Mtumaini Mwenyezi-Mungu kwa moyo wako wote, wala usitegemee akili zako mwenyewe.
6
Umtambue Mungu katika kila ufanyalo, naye atazinyosha njia zako.
7
Usijione wewe mwenyewe kuwa mwenye hekima; mche Mwenyezi-Mungu na kujiepusha na uovu.
8
Hiyo itakuwa dawa mwilini mwako, na kiburudisho mifupani mwako.
9
Mheshimu Mwenyezi-Mungu kwa mali yako, na kwa malimbuko ya mazao yako yote.
10
Hapo ghala zako zitajaa nafaka, na mapipa yako yatafurika divai mpya.
11
Mwanangu, usidharau adhabu ya Mwenyezi-Mungu, wala usiudhike kwa maonyo yake;
12
maana Mwenyezi-Mungu humwonya yule ampendaye, kama baba amwonyavyo mwanawe mpenzi.
13
Heri mtu anayegundua hekima, mtu yule anayepata ufahamu.
14
Hekima ni bora kuliko fedha, ina faida kuliko dhahabu.
15
Hekima ina thamani kuliko johari, hamna unachotamani kiwezacho kulingana nayo.
16
Kwa mkono wake wa kulia Hekima atakupa maisha marefu; kwa mkono wake wa kushoto atakupa mali na heshima.
17
Njia zake ni za kupendeza, zote zaelekea kwenye amani.
18
Hekima ni mti wa uhai kwa wote wampatao; wana heri wote wanaoshikamana naye.
19
Kwa hekima Mwenyezi-Mungu aliweka misingi ya dunia, kwa akili aliziimarisha mbingu.
20
Kwa maarifa yake vilindi vilipasuka, na mawingu yakadondosha umande.
21
Mwanangu, zingatia hekima safi na busara; usiviache vitoweke machoni pako,
22
navyo vitakuwa uhai nafsini mwako, na pambo zuri shingoni mwako.
23
Hapo utaweza kwenda zako kwa usalama, wala mguu wako hautajikwaa.
24
Ukiketi hutakuwa na hofu; ukilala utapata usingizi mtamu.
25
Usiogope juu ya tishio la ghafla, wala shambulio kutoka kwa waovu,
26
Maana Mwenyezi-Mungu ndiye atakayekutegemeza; atakuepusha usije ukanaswa mtegoni.
27
Usimnyime mtu anayehitaji msaada, ikiwa unao uwezo wa kufanya hivyo.
28
Usimwambie jirani yako aende zake hadi kesho, hali wewe waweza kumpa anachohitaji leo.
29
Usipange maovu dhidi ya jirani yako, anayeishi karibu nawe bila wasiwasi.
30
Usigombane na mtu bila sababu ikiwa hajakudhuru kwa lolote.
31
Usimwonee wivu mtu mkatili, wala usiige mwenendo wake.
32
Maana waovu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu; lakini yeye huwafanya marafiki zake wale walio wanyofu.
33
Mwenyezi-Mungu huapiza nyumba za waovu, lakini huyabariki makao ya waadilifu.
34
Yeye huwadharau wenye dharau, lakini huwafadhili wanyenyekevu.
35
Wenye hekima watavuna heshima, lakini wapumbavu watapata fedheha.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31