bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Proverbs 26
Proverbs 26
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 25
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 27 →
1
Heshima apewayo mpumbavu haimfai; ni kama theluji ya kiangazi, au mvua ya wakati wa mavuno.
2
Kama shomoro au mbayuwayu wasiotua, kadhalika laana asiyostahili mtu haimtui.
3
Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda, na fimbo kwa mgongo wa mpumbavu.
4
Usimjibu mpumbavu kipumbavu, usije ukafanana naye.
5
Mjibu mpumbavu kama ustahilivyo upumbavu wake, asije akajiona kuwa mwenye hekima zaidi.
6
Kumtuma mpumbavu ujumbe, ni kama kujikata miguu au kujitafutia shida.
7
Methali mdomoni mwa mpumbavu, ni kama miguu ya kiwete inayoninginia.
8
Kumpa mpumbavu heshima, ni kama kufunga jiwe kwenye kombeo.
9
Mpumbavu anayejaribu kutumia methali, ni kama mlevi anayejaribu kungoa mwiba mkononi.
10
Mtu amwajiriye mpumbavu au mlevi, ni kama mpiga upinde anayejeruhi kila mtu.
11
Mpumbavu anayerudiarudia upumbavu wake, ni kama mbwa anayekula matapishi yake.
12
Wamwona mtu ajionaye kuwa mwenye hekima? Nakuambia mpumbavu ni nafuu kuliko huyo.
13
Mvivu husema: “Huko nje kuna simba; siwezi kwenda huko.”
14
Kama vile mlango uzungukiapo bawaba zake, ndivyo mvivu juu ya kitanda chake.
15
Mvivu huutia mkono wake katika sahani ya chakula, lakini hawezi kuuinua hadi mdomoni.
16
Mvivu hujiona kuwa mwenye hekima kuliko watu saba wawezao kujibu kwa busara.
17
Ajiingizaye katika ugomvi usiomhusu, ni kama mtu amshikaye masikio mbwa anayepita.
18
Kama mwendawazimu achezeavyo mienge, au mishale ya kifo,
19
ndivyo alivyo mtu ampotoshaye jirani, kisha aseme, “Nilikuwa natania tu!”
20
Bila kuni, moto huzimika; bila mchochezi, ugomvi humalizika.
21
Kama vile makaa au kuni huchochea moto, ndivyo mgomvi achocheavyo ugomvi.
22
Maneno ya msengenyaji ni kama kitoweo; hushuka mpaka ndani kabisa tumboni.
23
Kama rangi angavu iliyopakwa kigae, ndivyo yalivyo maneno matamu yenye nia mbaya.
24
Mwenye chuki huficha chuki yake kwa maneno mazuri, lakini huwa ana hila moyoni mwake.
25
Akiongea vizuri usimwamini, moyoni mwake mna chuki chungu nzima.
26
Huenda akaficha chuki yake, lakini nia zake mbaya zitajulikana kwa wote.
27
Amchimbiaye mwenzake shimo, hutumbukia mwenyewe; abingirishaye jiwe litamrudia mwenyewe.
28
Asemaye uongo huwachukia hao anaowaumiza, naye abembelezaye huleta maangamizi.
← Chapter 25
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 27 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31