bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Proverbs 17
Proverbs 17
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 18 →
1
Afadhali mkate mkavu kwa amani, kuliko karamu katika nyumba ya ugomvi.
2
Mtumwa mwenye busara atachukua nafasi ya mwana mpumbavu, atapata sehemu ya urithi wa jamaa hiyo.
3
Ubora wa dhahabu ama fedha hupimwa kwa moto, lakini Mwenyezi-Mungu ndiye apimaye mioyo ya watu.
4
Mtenda maovu husikiliza maneno mabaya, mwongo hutegea sikio ulimi mdanganyifu.
5
Anayemdhihaki maskini anamtukana Muumba wake; anayefurahia maafa hatakosa kuadhibiwa.
6
Wazee huwaonea fahari wajukuu zao; watoto huwaonea fahari wazazi wao.
7
Maneno mazuri si kawaida kinywani mwa mpumbavu, sembuse maneno ya uongo kinywani mwa kiongozi!
8
Kwa mhongaji, hongo ni kama hirizi; kila afanyacho hufanikiwa.
9
Anayesamehe makosa hujenga urafiki, lakini anayekumbusha makosa hutenga rafiki.
10
Onyo kwa mwenye busara lina maana, kuliko mapigo mia kwa mpumbavu.
11
Afanyalo mtu mwovu ni kuasi tu; mjumbe mkatili atatumwa dhidi yake.
12
Afadhali kukutana na dubu jike aliyenyanganywa watoto wake, kuliko kukutana na mpumbavu katika upumbavu wake.
13
Mwenye kulipiza mema kwa mabaya, mabaya hayataondoka nyumbani mwake.
14
Kuanzisha ugomvi ni kama kufanya ufa kwenye bwawa; achana na ugomvi kabla haujafurika.
15
Kumsamehe mwenye hatia na kumwadhibu asiye na hatia yote mawili ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu.
16
Ya nini mpumbavu kuwa na fedha mkononi kununulia hekima, wakati yeye mwenyewe hana akili?
17
Rafiki wa kweli ni rafiki siku zote, ndugu huzaliwa asaidie wakati wa taabu.
18
Si jambo la akili kuweka rehani, na kuwa mdhamini wa mtu mwingine.
19
Anayependa ugomvi anapenda dhambi; anayejigamba anajitafutia maangamizi.
20
Mwenye moyo mpotovu hafanikiwi, na msema uongo hupatwa na maafa.
21
Mtoto mpumbavu ni huzuni kwa baba yake, na baba wa mpumbavu hana furaha.
22
Moyo mchangamfu ni dawa, bali moyo wenye huzuni hudhoofisha mwili.
23
Mtu mbaya hupokea hongo kwa siri ili apate kupotosha haki.
24
Mtu mwenye busara lengo lake ni hekima, lakini mpumbavu hupania kila kitu duniani.
25
Mtoto mpumbavu ni huzuni kwa baba yake, na uchungu kwa mama yake mzazi.
26
Si vizuri kumtoza faini mtu asiye na hatia; ni kosa kumchapa viboko muungwana.
27
Asiyesema sana ana maarifa; mtu mtulivu ni mwenye busara.
28
Hata mpumbavu akinyamaza huonekana ana hekima; akifunga mdomo wake huonekana kuwa mwenye akili.
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 18 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31