bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Proverbs 21
Proverbs 21
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 22 →
1
Moyo wa mfalme ni kama maji yanayotiririka; Mwenyezi-Mungu, huuongoza popote apendapo.
2
Matendo yote ya mtu ni sawa machoni pake, lakini Mwenyezi-Mungu hupima mioyo.
3
Kutenda mambo mema na ya haki, humpendeza Mwenyezi-Mungu kuliko tambiko.
4
Macho ya kiburi na moyo wa majivuno huonesha wazi dhambi ya waovu.
5
Mipango ya mtu wa bidii huleta mali kwa wingi, lakini kila aliye na pupa huishia patupu.
6
Mali ipatikanayo kwa udanganyifu, ni mvuke upitao na mtego wa kifo.
7
Ukatili wa wakatili utawafutilia mbali, maana wanakataa kutenda yaliyo ya haki.
8
Njia ya mtu mwenye hatia imepotoka, lakini mwenendo wa mnyofu umenyooka.
9
Afadhali kuishi pembeni juu ya paa, kuliko kuishi nyumbani na mwanamke mgomvi.
10
Anachopania kutenda mtu mbaya ni uovu; hata kwa jirani yake hana huruma.
11
Ukimwadhibu mwenye dhihaka, mjinga hupata hekima; ukimfundisha mwenye hekima, unampatia maarifa.
12
Mungu Mwadilifu anajua wanayotenda waovu nyumbani kwao; naye atawaangusha na kuwaangamiza.
13
Anayekataa kusikiliza kilio cha maskini, naye pia hatasikilizwa atakapolilia msaada.
14
Hasira hutulizwa kwa zawadi ya siri; tunu apewayo mtu imefichwa hupooza ghadhabu.
15
Haki ikitekelezwa watu wema hufurahi, lakini watu waovu hufadhaishwa.
16
Anayetangatanga mbali na njia ya busara, atajikuta ametua miongoni mwa wafu.
17
Anayependa anasa atakuwa maskini; anayefikiria tu kula na kunywa hatatajirika.
18
Mwovu atapata pigo ambalo halitampata mtu mwema, mkosefu ataadhibiwa badala ya mnyofu.
19
Afadhali kuishi jangwani, kuliko kukaa na mwanamke mgomvi na msumbufu.
20
Nyumbani kwa mwenye busara mna hazina za thamani, lakini mpumbavu huponda mali yake yote.
21
Anayepania uadilifu na huruma, ataishi maisha marefu na kuheshimiwa.
22
Mwenye hekima aweza kuteka mji wa wenye nguvu, na kuziporomosha ngome wanazozitegemea.
23
Achungaye mdomo wake na ulimi wake, hujiepusha na matatizo.
24
Mwenye majivuno na kiburi jina lake ni “Madharau;” matendo yake yamejaa majivuno ya ufidhuli wake.
25
Mvivu hufa kwa kutotimizwa tamaa zake, maana mikono yake milegevu haitaki kufanya kazi.
26
Mchana kutwa mwovu hutamani kupata kitu, lakini mwadilifu hutoa, tena kwa ukarimu.
27
Tambiko ya mwovu ni kitu cha kuchukiza, huchukiza zaidi akiitoa kwa nia mbaya.
28
Shahidi mwongo ataangamia, lakini msikivu hawezi kunyamazishwa.
29
Mtu mwovu hujionesha kuwa jasiri, lakini mwadilifu huhakikisha ametenda sawa.
30
Hakuna hekima, maarifa, wala mawaidha yoyote ya mtu, yawezayo kumshinda Mwenyezi-Mungu.
31
Farasi hutayarishwa kwa vita, lakini ushindi wamtegemea Mwenyezi-Mungu.
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 22 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31