bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Proverbs 29
Proverbs 29
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 28
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 30 →
1
Anayeonywa mara nyingi akawa mkaidi, ataangamia ghafla asipone tena.
2
Waadilifu wakitawala watu hufurahi, lakini waovu wakitawala watu hulalamika.
3
Apendaye hekima humfurahisha baba yake; lakini aandamanaye na malaya hufuja mali yake.
4
Mfalme akitumia haki huipatia nchi uthabiti, lakini akipenda hongo taifa huangamia.
5
Mwenye kumbembeleza jirani yake, anatega mtego wa kujinasa mwenyewe.
6
Mtu mbaya hunaswa kwa kosa lake, lakini mtu mwadilifu huimba na kufurahi.
7
Mwadilifu anajua haki za maskini, lakini mtu mwovu hajui mambo hayo.
8
Wenye dharau huutia vurugu mji mzima, lakini wenye hekima hutuliza ghadhabu.
9
Mwenye hekima akibishana na mpumbavu, mpumbavu huwaka hasira na kucheka bila kutulia.
10
Wapendao kumwaga damu humchukia mtu asiye na hatia, lakini watu wema huyalinda maisha yake.
11
Mpumbavu huonesha hasira yake wazi, lakini mwenye hekima huizuia na kuituliza.
12
Mtawala akisikiliza mambo ya uongo, maofisa wake wote watakuwa waovu.
13
Maskini na mkandamizaji wanafanana kwa kitu kimoja: Wote wawili wamepewa macho na Mwenyezi-Mungu.
14
Mfalme anayewaamua maskini kwa haki, atauona utawala wake umeimarika milele.
15
Adhabu na maonyo huleta hekima, lakini mtoto aliyeachwa afanye apendavyo humwaibisha mama yake.
16
Waovu wakitawala maovu huongezeka, lakini waadilifu watashuhudia kuanguka kwao.
17
Mpe nidhamu mwanao naye hatakupa wasiwasi; yeye ataufurahisha moyo wako.
18
Pasipo maono ya kinabii watu hukosa nidhamu; heri mtu yule anayeshika sheria.
19
Mtumwa haonyeki kwa maneno matupu, maana ingawa anayaelewa yeye hatayatii.
20
Wamwona mtu apayukaye bila kufikiri? Mtu mpumbavu ni afadhali kuliko yeye.
21
Ambembelezaye mtumwa wake tangu utoto, mwishowe mtumwa huyo atamrithi.
22
Mwenye ghadhabu huchochea ugomvi, mtu wa hasira husababisha makosa mengi.
23
Kiburi cha mtu humporomosha mwenyewe, lakini mnyenyekevu wa roho atapata heshima.
24
Anayeshirikiana na mwizi anajidhuru mwenyewe; husikia laana ya aliyeonewa bila kusema neno.
25
Kuwaogopa watu ni kujitega mwenyewe, lakini anayemtumaini Mwenyezi-Mungu yu salama.
26
Wengi hupenda kujipendekeza kwa mtawala, hali mtu hupata haki yake kwa Mwenyezi-Mungu.
27
Mdhalimu ni chukizo kwa mnyofu, naye mnyofu ni chukizo kwa mwovu.
← Chapter 28
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 30 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31