bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Proverbs 2
Proverbs 2
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 3 →
1
Mwanangu, ukiyakubali maneno yangu, na kuyathamini maagizo yangu;
2
ukitega sikio lako kusikiliza hekima, na kuuelekeza moyo wako upate ufahamu;
3
naam, ukiomba upewe busara, ukisihi upewe ufahamu;
4
ukiitafuta hekima kama fedha, na kuitaka kama hazina iliyofichika;
5
hapo utaelewa ni nini kumcha Mwenyezi-Mungu, utafahamu maana ya kumjua Mungu.
6
Maana Mwenyezi-Mungu huwapa watu hekima; kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu.
7
Huwawekea wanyofu akiba ya hekima safi, yeye ni ngao kwa watu waishio kwa uaminifu.
8
Huilinda mienendo ya watu watendao haki, na kuzihifadhi njia za waaminifu wake.
9
Ukinisikiliza utafahamu uadilifu na haki, utajua jambo lililo sawa na jema.
10
Maana hekima itaingia moyoni mwako, na maarifa yataipendeza nafsi yako.
11
Busara itakulinda, ufahamu utakuhifadhi;
12
vitakuepusha na njia ya uovu, na watu wa maneno mapotovu;
13
watu waziachao njia nyofu, ili kuziendea njia za giza;
14
watu wafurahiao kutenda maovu, na kupendezwa na upotovu wa maovu;
15
watu ambao mienendo yao imepotoka, nazo njia zao haziaminiki.
16
Hekima itakuwezesha kumkwepa mwanamke mwasherati, mwanamke malaya wa maneno matamu;
17
mwanamke amwachaye mwenzi wa ujana wake, na kulisahau agano la Mungu wake.
18
Nyumba yake yaelekea kuzimu, njia zake zinakwenda ahera.
19
Yeyote amwendeaye kamwe harudi, wala hairudii tena njia ya uhai.
20
Kwa hiyo utafuata mfano wa watu wema, na kuzingatia mienendo ya waadilifu.
21
Maana wanyofu wataipata nchi, na waaminifu watadumu ndani yake.
22
Lakini waovu wataondolewa nchini, na wenye hila watangolewa humo.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31