bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Proverbs 9
Proverbs 9
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 10 →
1
Hekima amejenga nyumba yake, nyumba yenye nguzo saba.
2
Amechinja wanyama wa karamu, divai yake ameitayarisha, ametandika meza yake.
3
Amewatuma watumishi wake wa kike mjini, waite watu kutoka kwenye vilele vya miinuko:
4
“Yeyote aliye mjinga na aje hapa!” Na yeyote aliye mpumbavu humwambia:
5
“Njoo ukale chakula, na unywe divai niliyotengeneza.
6
Achana na ujinga upate kuishi; fuata njia ya akili.”
7
Anayemkosoa mwenye dharau hupata matusi, amkaripiaye mwovu huishia kwa kuumizwa.
8
Usimwonye mwenye dharau maana atakuchukia; mwonye mwenye hekima naye atakupenda.
9
Mfunze mwenye hekima naye atazidi kuwa na hekima; mfundishe mwadilifu naye atazidi kuelimika.
10
Kumcha Mwenyezi-Mungu ni msingi wa hekima; na kumjua yule Mtakatifu ni kupata akili.
11
Kwa msaada wangu mimi Hekima siku zako zitaongezwa; utaongezewa miaka mingi maishani mwako.
12
Kama una hekima, itakufaa wewe mwenyewe; kama ukiidharau, mwenyewe utapata hasara.
13
Mwanamke mpumbavu ana kelele, hajui kitu wala hana haya.
14
Hukaa kitako mlangoni mwa nyumba yake, huweka kiti chake mahali pa juu mjini,
15
na kuwaita watu wapitao njiani, watu wanaokwenda kwenye shughuli zao:
16
“Yeyote aliye mjinga na aje hapa!” Na yeyote aliye mpumbavu humwambia:
17
“Maji ya wizi ni matamu sana; mkate unaoliwa kwa siri ni mzuri sana.”
18
Lakini mjinga hajui kwamba humo mna wafu, wageni wa mwanamke huyo wamo chini Kuzimu.
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 10 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31