bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Proverbs 24
Proverbs 24
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 25 →
1
Usiwaonee wivu watu waovu, wala usitamani kuwa pamoja nao,
2
maana fikira zao zote ni juu ya ukatili, hamna jema lolote litokalo midomoni mwao.
3
Nyumba hujengwa kwa hekima, na kuimarishwa kwa busara.
4
Kwa maarifa vyumba vyake hujazwa vitu vya thamani na vya kupendeza.
5
Kuwa na hekima ni bora kuliko kuwa na nguvu, naam, maarifa ni bora kuliko nguvu.
6
Maana kwa mwongozo mzuri waweza kupigana vita, na kwa washauri wengi ushindi hupatikana.
7
Kwa mpumbavu hekima ni ngumu kuielewa; penye mkutano wa mashauri hafungui mdomo.
8
Afikiriaye kutenda maovu daima ataitwa mtu mwenye fitina.
9
Mpango anaofikiria mpumbavu ni dhambi; mwenye dharau huchukiwa na kila mtu.
10
Ukifa moyo wakati wa shida, basi wewe ni dhaifu kweli.
11
Mwokoe mtu anayechukuliwa kuuawa bure; usisite kumwokoa anayeuawa bila hatia.
12
Usiseme baadaye: “Hatukujua!” Maana Mungu apimaye mioyo ya watu huona; yeye atakulipa kulingana na matendo yako!
13
Mwanangu, ule asali maana ni nzuri; sega la asali ni tamu mdomoni.
14
Ndivyo ilivyo hekima nafsini mwako; ukiipata utakuwa na matazamio mema, wala tumaini lako halitakuwa la bure.
15
Usivizie kama mwovu kushambulia makao ya mtu mwema, wala usijaribu kuiharibu nyumba yake,
16
maana mtu mwema huanguka mara nyingi lakini huinuka, lakini mtu mwovu huangamizwa na janga.
17
Usishangilie kuanguka kwa adui yako; usifurahie moyoni mwako kujikwaa kwake,
18
maana Mwenyezi-Mungu aonaye hayo hatapendezwa; huenda akaacha kumwadhibu.
19
Usihangaike kwa sababu ya watenda mabaya, wala usiwaonee wivu watu waovu,
20
maana mwovu hatakuwa na mema baadaye; taa ya uhai wake itazimwa.
21
Mwanangu, umche Mwenyezi-Mungu na kumheshimu mfalme, wala usishirikiane na wale wasio na msimamo,
22
maana maangamizi yao huwapata ghafla. Hakuna ajuaye maafa watakayozusha.
23
Ifuatayo pia ni misemo ya wenye hekima: Kupendelea watu katika hukumu si vizuri.
24
Anayemwachilia mtu mwenye hatia, hulaaniwa na watu na kuchukiwa na mataifa.
25
Lakini wanaowaadhibu waovu watapata furaha, na baraka njema zitawajia.
26
Jibu lililo la haki, ni kama busu la rafiki.
27
Kwanza fanya kazi zako nje, tayarisha kila kitu shambani, kisha jenga nyumba yako.
28
Usishuhudie bure dhidi ya jirani yako, wala usiseme uongo juu yake.
29
Usiseme, “Nitamtenda kama alivyonitenda! Ni lazima nilipize kisasi!”
30
Nilipitia karibu na shamba la mvivu; shamba la mzabibu la mtu mpumbavu.
31
Nilishangaa kuona limemea miiba, magugu yamefunika eneo lake lote, na ukuta wake wa mawe umebomoka.
32
Nilitazama, nikawaza, mwishowe nikapata funzo:
33
Lala tu kidogo; sinzia tu kidogo! Kunja mikono yako tu upumzike!
34
Lakini kumbuka kwamba uwapo usingizini, umaskini utakuvamia kama mnyanganyi, ufukara kama mtu mwenye silaha.
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 25 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31