bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Corinthians 1
1 Corinthians 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 2 →
1
Mimi Paulo niliyeitwa kuwa mtume wa Kristo Yesu kwa hayo, Mungu ayatakayo, na ndugu Sostene
2
tunawaandikia ninyi wateule wa Mungu mlioko Korinto; mlitakaswa na Kristo Yesu, mkaitwa kuwa watakatifu pamoja na wote wanaolitambikia Jina la Bwana wetu Yesu Kristo ko kote, huko kwao nako huku kwetu.
3
Upole uwakalie na utengemano unaotoka kwa Mungu, Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo!
4
*Nayavumisha siku zote mema yake Mungu, aliyowagawia ninyi, mwe katika Kristo Yesu.
5
Kwa hivyo, mnavyomkalia, mwazipata mali zote zilizomo katika ufundisho na katika utambuzi wote;
6
nao ushuhuda wa Kristo ukapata nguvu kwenu.
7
Kwa sababu hii hakuna gawio, mnalolikosa mkiwa mnangoja, Bwana wetu Yesu Kristo atokee waziwazi.
8
Yeye ndiye atakayewatia nguvu mpaka mwisho, mpate kutokea siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo mkiwa hamnayo ya kuwakamia.
9
Mungu ni mwelekevu aliyewaita kuwa wenziwe Mwana wake Yesu Kristo aliye Bwana wetu.*
10
Lakini nawaonya, ndugu, kwa ajili ya Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, wote mseme mamoja, kwenu kusiwe na matengano, ila nguvu yenu iwe ile ya kutenda moyo mmoja na kutambua neno moja tu.
11
Kwani ndugu zangu, nimeambiwa mambo yenu na wale wa Kloe, ya kuwa kwenu yako magomvi.
12
Nalisema lile la kwamba: Kwenu kila mmoja husema: Mimi wa Paulo! au: Mimi wa Apolo! au: Mimi wa Kefa! au: Mimi wa Kristo! Je?
13
Kristo amegawanyika? Au ni Paulo aliyewambwa msalabani kwa ajili yenu? Au mmebatiziwa jila la Paulo?
14
Namshukuru Mungu, ya kuwa sikubatiza mtu kwenu ila Krispo na Gayo,
15
maana mtu asiseme: Mmebatiziwa jina langu mimi.
16
Kweli naliwabatiza nao wa nyumbani mwa Stefana. Tena sijui, kama yuko mwingine, niliyembatiza.
17
Kwani Kristo hakunituma kubatiza, ila amenituma kuipiga hiyo mbiu njema, lakini si kwa maneno ya ujuzi wa kimtu, msalaba wake Kristo usitenguliwe.
18
Kwani neno la kuwambwa msalabani ndilo la upuzi kwao wanaoangamia, lakini kwetu sisi tunaookolewa ndilo la nguvu ya Mungu.
19
Kwani imendikwa: Nitauangamiza werevu wao walio werevu wa kweli nao utambuzi wao watambuzi.
20
Yuko wapi aliye mwerevu wa kweli? Yuko wapi aliye mwandishi? Yuko wapi aliye mbishi wa siku hizi? Je? Mungu hakuupumbaza werevu wa ulimwengu huu?
21
*Kwani kwa huo werevu wake ulimwengu huu haukumtambua Mungu na werevu wake wa Kimungu ulio wa kweli; kwa hiyo Mungu amependezwa kuwaokoa wenye kumtegemea akiwatangazia mapumbavupumbavu.
22
Kwani Wayuda hutaka vielekezo, nao Wagriki hutafuta werevu ulio wa kweli.
23
Lakini sisi twamtangaza Kristo, alivyowambwa msalabani; ndipo, Wayuda wajikwaliapo, tena ndipo, wamizimu waoneapo mapumbavu tu.
24
Lakini wale walioitwa, Wayuda na Wagriki, kwao twamtangaza Kristo kwamba: Ni nguvu ya Mungu, tena: Ni werevu wa Mungu ulio wa kweli.
25
Kwani yaliyo mapumbavu ya Mungu ndiyo yenye werevu wa kweli kuupita wa watu, nayo yaliyo manyonge ya Mungu ndiyo yenye nguvu kuzipita za watu.
26
Kwani utazameni, ndugu, wito wenu! Hakuna wengi walio werevu wa kimtu; hakuna wengi walio wenye nguvu; hakuna wengi walio wenye macheo.
27
Lakini walio wapumbavu wa ulimwengu huu ndio, Mungu aliowachagua, awatweze walio werevu wa kweli. Tena walio wanyonge wa ulimwengu huu ndio, Mungu aliowachagua, awatweze wenye nguvu.
28
Tena walio wakiwa wa ulimwengu huu nao waliobezwa ndio, Mungu aliowachagua, hata wasiowaziwa kuwa watu, awaumbue wanaotukuzwa kwamba: Ni watu,
29
kusudi mbele ya Mungu mwenye mwili wa kimtu asijivune, hata mmoja.
30
Kwake yeye ndio, mlikotoka ninyi mliomo mwake Kristo Yesu. Huyu ndiye werevu wetu wa Kimungu ulio wa kweli, na wongufu na utakasi na ukombozi.
31
Basi, iwe, kama ilivyoandikwa: Mwenye kujivuna na ajivunie kuwa wa Bwana!*
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16