bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Corinthians 11
1 Corinthians 11
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 12 →
1
Niigeni mimi, kama nami ninavyomwiga Kristo!
2
Nawasifu ninyi, ya kuwa mnanikumbuka po pote, mkashikamana nayo maagizo yangu, kama nilivyowaagiza.
3
Lakini nataka, mjue, ya kuwa kichwa cha kila mume ni Kristo, nacho kichwa cha mke ni mume, nacho kichwa cha Kristo ni Mungu.
4
Kila mume akiomba au akifumbua Neno na kuvaa kichwani, hukipatia kichwa chake soni.
5
Lakini kila mke akiomba au akifumbua Neno pasipo kuvaa kichwani, hukipatia kichwa chake soni, maana hujifananisha kuwa mamoja, kama wenye kunyolewa walivyo.
6
Maana mke asipovaa kichwani, naye akatwe nywele! Lakini mke akiona soni ya kukatwa nyuwele au kunyolewa avae kichwani!
7
Maana mume haimpasi kuvaa kichwani, kwani yeye ubwana wake hufanana nao wake Mungu; lakini mke ubwana wake ndio uleule wa mume.
8
Maana walipoumbwa, mume hakutoka katika mke, ila mke alitoka katika mume.
9
Tena mume hakuumbwa kwa ajili ya mke, ila mke aliumbwa kwa ajili ya mume.
10
Kwa hiyo imempasa mke kushurutishwa kuvaa kichwani kwa ajili ya malaika.
11
Kisha wakiwa wa Bwana, hakuna, mke anachokuwa pasipo mume, wala hakuna, mume anachokuwa pasipo mke.
12
Kwani kama mke atokavyo katika mume, vivyo hivyo hata mume huzaliwa na mke; lakini yote hutoka kwake Mungu.
13
Yapambanueni ninyi kwa ninyi, kama inampasa mke kuomba mbele ya Mungu pasipo kuvaa kichwani!
14
Navyo mlivyoumbwa haviwafundishi, ya kuwa mume haimpasi kamwe kuwa na nywele ndefu?
15
Lakini mke akiwa na nywele ndefu, ni pambo lake zuri. Maana amepewa nywele ndefu, ziwe mavazi yake.
16
Lakini kama yuko anayependa mabisho, basi, mazoea kama hayo hayako wala kwetu wala po pote palipo na wateule wa Mungu.
17
Lakini liko neno, sharti niliseme waziwazi, silisifu, ni hili: Hamkutanii mema, ila mabaya.
18
Kwani kwanza nasikia, ya kuwa hapo, mnapokutania wateule na wateule, yako magawanyiko, nami menginemengine nayasadiki.
19
Kwani matengano hayana budi kuwa kwenu, kusudi walio wakweli kwenu waonekane.
20
Ninyi mnapokutania pamoja, siko kukila Chakula cha Bwana.
21
Kwani mnapokula, kila mmoja huanza kunyang'anya chakula chake mwenyewe; kwa hiyo mwingine yuko na njaa, mwingine amelewa.
22
Je, hamna nyumba zenu za kuliamo na kunyweamo? Au mwawabeza wateule wake Mungu mkiwatia soni wasio na kitu? Niwaambieje? Niwasifu? La! Katika hayo siwasifu.
23
*Maana mimi nalipewa na Bwana, niliyowapa nanyi: Bwana Yesu usiku ule, alipotolewa, akatwaa mkate,
24
akashukuru, akaumega, akasema: Twaeni, mle! Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu. Fanyizeni hivyo, mnikumbuke!
25
Vivyo hivyo akakitwaa nacho kinyweo, walipokwisha kula, akisema: Kinyweo hiki ndicho Agano Jipya katika damu yangu. Fanyizeni hivyo, kila mtakapokinywea, mnikumbuke!
26
Kwani kila mnapoula mkate huu, mkakinywea nacho kinyweo hiki, kutangazeni kufa kwake Bwana, mpaka atakapokuja!
27
Kwa hiyo kila anayejilia tu mkate huo na kujinywea tu kinhweo cha Bwana atajionea mapatilizo ya mwili na damu ya Bwana.
28
Sharti mtu ajichunguze mwenyewe, kisha aule mkate huo, akinywee nacho kinyweo hicho!
29
Maana mwenye kujilia na kujinywea tu hujilia mapatilizo, hujinywea mapatilizo, kwani haupambanui mwili wa Bwana.
30
Kwa hiyo kwenu wako wengi walio wanyonge na wagonjwa, nao waliolala si wachache.
31
Lakini tunapojichunguza wenyewe hatutapatilizwa.
32
Ila tukipatilizwa na Bwana tunaonywa, tusije kuhukumiwa pamoja nao wa ulimwengu huu.*
33
Kwa hiyo, ndugu zangu, mnapokutania kula, sharti mngojane!
34
Mtu akiwa na njaa ale mwake, kwamba msikutanie mapatilizo! Nayo yaliyosalia nitayaagiza nitakapokuja.
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 12 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16