bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Corinthians 13
1 Corinthians 13
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 14 →
1
*Ijapo niseme misemo ya kimtu na ya kimalaika, nisipokuwa na upendo, ndimi upatu wenye milio au njuga yenye makelele.
2
Ijapo niwe mwenye ufumbuaji, nikayajua mafumbo yote na utambuzi wote, hata nikawashinda wote kwa kumtegemea Mungu, nikaweza kuhamisha hata vilima, nisipokuwa na upendo, hakuna nilichokuwa.
3
Ijapo niwagawie maskini mali zangu zote, nikautoa nao mwili wangu, uunguzwe na moto, nisipokuwa na upendo, hakuna nifaacho.
4
Upendo ni wenye uvumilivu na upole; upendo haujui wivu. Upendo haujikwezi, wala haujivuni;
5
haukwazi, wala hauyatafuti yaliyo yake, wala hauchukiziki, wala hauyahesabu maovu.
6
Hauyafurahii mapotovu, ila huyafurahia yaliyo ya kweli.
7
Hujitwika yote, huyategemea yote, huyangojea yote, huyavumilia yote.
8
Hapana, upendo unapokomea; kama ni ufumbuaji, utakoma; kama ni misemo, itanyamaza; kama ni utambuzi, utakoma.
9
Kwani tunayoyatambua, ni fungu tu; nayo tunayoyafumbua, ni fungu tu;
10
lakini matimilifu yatakapokuja, yale ya kifungufungu yatakoma.
11
Nilipokuwa mtoto nalisema kitoto, nikayajua ya kitoto, nikayawaza ya kitoto. Lakini hapo nilipokuwa mtu mzima nimeyaacha yale ya kitoto.
12
Maana sasa tunafanana kama tunaona mfano tu wa yale yasiyofumbuka bado; lakini siku ile tutayaona macho kwa macho. Sasa nayatambua fungu tu, lakini siku ile nitayatambua, kama nitakavyokuwa nimetambulika.
13
Sasa kusikokoma ndiko kumtegemea Mungu na kumngojea na kupenda, huku kutatu. Lakini kuliko kukubwa kukupita kwingine ndiko kupenda.*
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 14 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16