bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Corinthians 16
1 Corinthians 16
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
1
Lakini kwa ajili ya mchango, watakatifu wanaochangiliwa, fanyeni nanyi, kama nilivyowaagiza wateule wa Galatia!
2
Kila siku ya kwanza ya juma kila mmoja wenu na aweke kwake na kuyalimbika yapatanayo na mapato yake, kisha ayachanganye yote, maana machango yasianzwe hapo, nitakapofika!
3
Lakini ndipo nifike, wale, mtakaowachagua ninyi, nitawatuma na barua, wavipeleke vipaji vyenu Yerusalemu.
4
Lakini vikiwa vingi vya kupasa, niende nami, watakwenda pamoja nami.
5
Lakini nitafika kwenu, nitakapokwisha kupita huko Makedonia. Kwani Makedonia nitapita tu;
6
lakini kwenu, kama vinapatikana, nitakaa, labda nitamaliza kwenu siku za kipupwe, ninyi mpate kunisindikiza huko nitakakokwenda
7
Kwani sasa sitaki kuonana nanyi kwa kupita tu; kwani nangojea, nikae kwenu kitambo cha siku, Bwana akipenda.
8
Lakini huku Efeso nitakaa mpaka sikukuu ya Pentekote.
9
Kwani nimefunguliwa mlango mkubwa, tena kazi inaendelea, ijapo wabishi wawe wengi.
10
Lakini Timoteo atakapofika, mmtazame, akae kwenu pasipo woga! Kwani naye anaifanya kazi ya Bwana kama mimi.
11
Pasiwe anayembeza! Ila msindikizeni na kupatana, afike kwangu! Kwani tunamngojea mimi na ndugu.
12
Lakini kwa ajili ya ndugu yetu Apolo mjue, ya kuwa nimemhimiza mara kwa mara, aje kwenu pamoja na hao ndugu; lakini hakutaka kabisa kwenda sasa. Lakini atakuja, patakapomfalia.
13
Kesheni! Kukalieni kumtegemea Bwana, mwe waume wenye nguvu!
14
Mambo yenu yote yafanywe katika upendano!
15
Ndugu, nitakalo tena, ni hili: mwawajua akina Stefana, ya kuwa ndio malimbuko ya nchi ya Akea, tena wamejitoa wenyewe, waje wawatumikie watakatifu.
16
Kwa hiyo nanyi mwatii walio hivyo na kila aliye mwenzao wa kazi na wa masumbuko!
17
Nimefurahiwa na kuja kwake Stefana na Fortunato na Akaiko, kwani ndio walionifanyizia, ambavyo ninyi hamkuweza kunifanyizia.
18
Kwani wameituliza roho yangu nazo roho zenu. Basi, watambueni walio hivyo!
19
Wateule wote walioko Asia wanawasalimu. Akila na Puriskila pamoja nao wote wanaokusanyika nyumbani mwao wanawasalimu sana, kwa kuwa m wa Bwana.
20
Nao ndugu wote wanawasalimu. Mwamkiane mkinoneana, kama watakatifu walivyozoea!
21
Hii salamu yangu mimi Paulo naiandika kwa mkono wangu.
22
Mtu asiyempenda Bwana na awe ameapizwa! Bwana anakuja.
23
Upole wa Bwana Yesu uwakalie ninyi!
24
Upendo wangu wa kuwapenda ninyi, kwa kuwa m wake Yesu Kristo, uwakalie ninyi nyote! Amin.
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16