bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Corinthians 15
1 Corinthians 15
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 16 →
1
*Ndugu, nataka kuwatambulisha vena huo Utume mwema, niliowatangazia; ndio, mlioupokea na kuukalia,
2
tena ndio, ambao mnaokolewa nao, ikiwa mmeyashika maneno ya hiyo mbiu njema, niliyowapigia, isipokuwa mmeitegemea bure.
3
Kwani kwanza nimewatolea, niliyoyapokea hata mimi ya kwamba: Kristo alikufa kwa ajili ya makosa yetu, kama alivyoandikiwa;
4
nayo ya kwamba: Alizikwa, akafufuliwa siku ya tatu, kama alivyoandikiwa.
5
Kisha alimtokea Kefa, kisha akawatokea wale kumi na wawili.
6
Kisha akawatokea ndugu waliopita mia tano, walipokuwa pamoja; namo miongoni mwao wengi wako wazima hata sasa, lakini wengine wamelala.
7
Kisha akamtokea Yakobo, kisha mitume wote.
8
Hayo yote yakiisha, akanitokea hata mimi, ijapo sikuzaliwa, siku zilipotimia.
9
Kwani mimi ni mdogo kuliko mitume wote, hainipasi kuitwa mtume, kwa sababu naliwafukuza wateule wake Mungu.
10
Lakini ni gawio la Mungu nikiwa hivyo, nilivyo, nalo gawio lake, nililopewa, halikuwa la bure; ila nimejisumbua kuwapita wao wote, lakini si mimi, ila ni gawio lake Mungu lililofuatana nami.*
11
Basi, nikiwa mimi, au wakiwa wale, hivyo ndivyo, tunavyovitangaza, tena ndivyo, mlivyovitegemea.
12
*Lakini Kristo akitangazwa, ya kuwa amefufuka katika wafu, kwenu wengine husemaje: Hakuna ufufuko wa wafu?
13
Kama hakuna ufufuko wa wafu, hata Kristo hakufufuka.
14
Lakini kama Kristo hakufufuka, matangazo yetu ni ya bure, nako kumtegemea kwenu ni kwa bure.
15
Tena sisi tungeonekana kuwa mashahidi wa Mungu wa uwongo, kwa sababu tulimshuhudia Mungu, ya kuwa alimfufua Kristo, asiyemfufua, ikiwa watu hawafufuki.
16
Kwani kama wafu hawafufuki, hata Kristo hakufufuka.
17
Lakini kama Kristo hakufufuka, kumtegemea kwenu ni kwa bure, nayo makosa yenu mkingali mnayo bado.
18
Basi, nao waliolala katika Kristo wangekuwa wamepotea.
19
Vikiwa hivyo, nasi katika maisha yetu ya huku nchini, kama kingojeao chetu ni Kristo tu, tungekuwa wakiwa kuliko watu wote.
20
Lakini sasa Kristo amekwisha fufuka katika wafu, ni limbuko lao waliolala.*
21
Kwani kama kufa kulivyoletwa na mtu, vivyo hivyo hata kufufuka kwa wafu kuliletwa na mtu.
22
Kwani kama wanavyokufa wote kwa kuwa wana wa Adamu, vivyo hivyo wote watarudishwa uzimani kwa kuwa wake Kristo,
23
lakini kila mmoja mahali pake: limbuko ndio Kristo; pafuatana walio wake Kristo hapo, atakapojia;
24
mwisho ni hapo, atakapompa Mungu Baba ufalme, ni hapo, atakapokuwa amekwisha kuutangua ukubwa wote na nguvu na uwezo wote.
25
Kwani yeye sharti ashike ufalme, mpaka awaweke adui zake wote chini miguuni pake.
26
Adui wa mwisho atakayeshindwa ni kifo.
27
Kwani aliyaweka yote chini miguuni pake. Lakini pakisemwa: Yote yaliwekwa chini yake, iko waziwazi, ya kuwa ndiyo yote pasipo yule aliyeyaweka yote chini yake.
28
Lakini hapo, yote yatakapokuwa yamekwisha kuwekwa chini yake, ndipo, naye Mwana mwenyewe atajiweka chini yake yule aliyeyaweka yote chini yake. Maana yote yawe yake Mungu po pote.
29
Kama sivyo, wale wanaobatizwa kwa ajili ya wafu wangewapatia nini? Kama wafu hawafufuki kamwe, hubatizwaje?
30
Nasi tunajiponzaje saa zo zote?
31
Ndugu, ninakufa siku kwa siku; ndivyo, ninavyotukuzwa kwenu, tena ndivyo, na Bwana wetu Yesu Kristo anavyonitukuza.
32
Kama nimeshindana na nyama wakali kimtu tu huko Efeso, vingenifaliaje? Wafu wasipofufuka, basi: Na tule, na tunywe! Kwani kesho tutakufa!
33
Msipotelewe! Maongezi maovu huangamiza mazoezo mazuri.
34
Levukeni kweli, msikose! Kwani wengi hawamtambui Mungu. Haya nayasemea kuwatia soni ninyi.
35
Lakini labda yuko atakayeuliza: Wafu watafufukaje? Nao watakuja wenye miili gani?
36
Mjinga wee! Unachokipanda, hakirudi uzimani, isipokuwa kife kwanza.
37
Tena ukipanda hupandi mwili utakaokuwapo, ila unapanda kipunje kitupu, ikiwa cha ngano au cha mbegu nyinginyingine.
38
Lakini Mungu hukipa mwili, kama anavyotaka, kila mbegu hupewa mwili wake mwenyewe.
39
Nyama zote si nyama moja tu, ila nyingine ni ya watu, nyingine ni ya ng'ombe, nyingine ni ya ndege, nyingine ni ya samaki.
40
Tena iko miili ya mbinguni na miili ya nchini. Lakini uzuru wao ya mbinguni uko mbali, nao uzuri wao ya nchini uko mbali.
41
Uzuri wa jua uko mbali, nao uzuri wa mwezi uko mbali, nao uzuri wa nyota uko mbali, kwani nazo nyota na nyota zinapitana uzuri.
42
Nao ufufuko wa wafu utakuwa vivyo hivyo. Hupandwa yenye kuoza, hufufuliwa isiyooza.
43
Hupandwa yenye kubezwa, hufufuliwa yenye kutukuzwa. Hupandwa yenye unyonge, hufufuliwa yenye nguvu.
44
Hupandwa miili ya kimtu, hufufuliwa miili ya kiroho. Kama iko miili ya kimtu, nayo ya kiroho iko.
45
Kwani ndivyo, vilivyoandikwa kwamba: Adamu, yule mtu wa kwanza, alipata kuwa mwenye roho ya uzima. Naye Adamu wa mwisho amepata kuwa roho yenye kurudisha uzimani.
46
Lakini mwili wa kiroho sio wa kwanza, ila wa kimtu ndio uliotangulia, kisha kukafuata wa kiroho.
47
Mtu wa kwanza alitoka nchini, ni wa nchini; mtu wa pili alitoka mbinguni.
48
Yule wa nchini alivyo, ndivyo, wa nchini walivyo nao. Naye yule wa mbinguni alivyo, ndivyo, wa mbinguni watakavyokuwa nao.
49
Nasi tulivyokuwa wenye sura ya yule wa nchini, ndivyo, tutakavyokuwa hata wenye sura ya yule wa mbinguni.
50
Ndugu, hili nalisema waziwazi: Yenye nyama na damu haiwezi kuurithi ufalme wa Mungu, wala yenye kuoza haitairithi isiyooza.
51
Tazameni, ninawaambieni neno lililokuwa limefichika siku zote: Hatutalala sisi sote, lakini sote tutageuzwa.
52
Itakuwapo katika kitambo kidogo tu kama cha kufumba jicho tu; ni hapo, baragumu la mwisho litakapolia.
53
Kwani miili hii yenye kuoza sharti ivae isiyooza, nayo yenye kufa sharti ivae isiyokufa.
54
*Lakini hapo, hii miili yenye kuoza itakapovaa isiyooza, nayo yenye kufa itakapovaa isiyokufa, ndipo, litakapokuwapo lile neno lililoandikwa:
55
Kufa kumemezwa, kukashindwa! Wewe kifo, kushinda kwako kuko wapi? Wewe kuzimu, uchungu wako luko wapi?
56
Kwani uchungu wa kufa ndio ukosaji, lakini nguvu ya ukosaji ndiyo Maonyo.
57
Lakini Mungu atukuzwe atupaye kushinda kwa nguvu ya Bwana wetu Yesu Kristo!
58
Kwa hiyo, ndugu zangu wapendwa, mjishupaze, msitukutike! Jikazeni kuendelea kazini mwa Bwana po pote, kwa kuwa mmejua, ya kama masumbuko yenu, mnayoyaona kwa ajili ya Bwana, siyo ya bure!*
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 16 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16