bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Corinthians 12
1 Corinthians 12
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 13 →
1
*Lakini ndugu, sitaki, ninyi mkose kuyajua mambo ya Kiroho.
2
Mnajua: Mlikuwa wamizimu, napo po pote, mlipoongozwa, mlipenda kuyafuata matambiko ya vinyago visivyosema.
3
Kwa hiyo nawatambulisha, ya kuwa hakuna mwenye Roho ya Mungu anayeweza kusema: Yesu na awe ameapizwa! Tena hakuna anayeweza kusema: BWANA NI YESU! asipokuwa na Roho takatifu.
4
Kweli yako mapitano ya magawio, lakini Roho ni yule mmoja.
5
Tena yako mapitano ya utumishi, lakini Bwana ni yule mmoja.
6
Tena yako mapitano ya nguvu, lakini Mungu anayevitia vyote nguvu kwa watu wote ni yule mmoja.
7
Lakini kila mtu hufunuliwa kipaji chake cha Roho, kwa kwamba wote wakionee upato.
8
Kwani mmoja hupewa na Roho kusema ya werevu wa kweli, mwingine kusema ya utambuzi unaopatana na Roho yule yule.
9
Mwingine hupewa kumtegemea Mungu kwa nguvu ya Roho yuleyule, mwingine hupewa magawio ya kuponya wagonjwa kwa nguvu ya Roho yule mmoja.
10
Mwingine hupewa kutenda ya nguvu, mwingine ufumbuaji, mwingine kuyapambanua ya Kiroho, mwingine misemo migeni, mwingine kuieleza ile misemo.
11
Lakini haya yote huyatenda Roho yule mmoja akimgawia kila mmoja, kama anavyopenda.*
12
Kwani ni kama vya mwili: ulio mmoja unavyo viungo vingi; tena viungo vyote vya mwili, ingawa ni vingi, ni mwili mmoja tu; vivyo hivyo naye Kristo.
13
Kwani kwa nguvu ya ile Roho moja tumebatiziwa sisi sote kuwa mwili mmoja, tukiwa Wayuda au Wagriki, tukiwa watumwa au waungwana; nasi sote tulinyweshwa Roho moja.
14
Kwani nao mwili sio kiungo kimoja, ila vingi.
15
Mguu ukisema: Kwa sababu si mkono, mimi si wa mwili, je? Kwa hiyo sio wa mwili?
16
Nalo sikio likisema: Kwa sababu si jicho, mimi si la mwili je? Kwa hiyo silo la mwili?
17
Mwili wote kama ungekuwa jicho, tungesikiaje? Kama wote ungekuwa sikio, tungenusaje?
18
Lakini Mungu ameviweka viungo mwilini kila kimoja hapo, alipokitaka.
19
Lakini vyote kama vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungepatikana wapi?
20
Sasa viungo ni vingi, lakini mwili ni mmoja.
21
Jicho haliwezi kuuambia mkono: Sikutumii; wala kichwa hakiwezi kuiambia miguu: Siwatumii ninyi.
22
Lakini ni hivyo: vile viungo vya mwili, tunavyoviwazia kuwa vinyonge, hatumika kuliko vingine.
23
Navyo, tunavyoviwazia kuwa vyenye soni, hupata heshima kuliko vingine; navyo visivyo vizuri hupambwa kuliko vingine.
24
Maana vile vilivyo vizuri machoni petu havipambwi. Lakini Mungu ameuunganisha mwili, nacho kilichopunguka uzuri akakipatia heshima kuliko vingine.
25
Maana mwilini msiwe na migawanyiko, ila viungo vipatane kutunzana kila kiungo na mwenziwe.
26
Napo kiungo kimoja kinapoumia, basi, viungo vyote huumia pamoja nacho; napo kiungo kimoja kinapotukuzwa, basi, viungo vyote hufurahi pamoja nacho.
27
Lakini ninyi m mwili wake Kristo, tena m viungo kila mmoja mahali pake.
28
Wako, Mungu aliowawekea wateule: kwanza mitume, wa pili wafumbuaji, wa tatu wafunzi, kisha wenye nguvu, kisha wenye magawio ya kuponya wagonjwa nao watumikizi nao wenye kuongoza nao wenye misemo migeni.
29
Wote ni mitume? Wote ni wafumbuaji? Wote ni wafunzi? Wote ni wenye nguvu?
30
Wote huponya wagonjwa? Wote husema misemo migeni? Wote hufumbua?
31
Jikazeni, mpate magawio yapitayo hayo! Nami nitawaonyesha njia iliyo nzuri kuzipita zote.
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 13 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16