bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Corinthians 2
1 Corinthians 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 3 →
1
Nami, ndugu, nilipokuja kwenu nalijia kuutangaza ushuhuda wa Mungu; sikuja kuwaambia maneno makuu ya werevu ulio wa kweli.
2
Kwani kwenu sikuwaza werevu mwingine, asipokuwa Yesu Kristo, naye hivyo, alivyowambwa msalabani.
3
Nami nalikaa kwenu mwenye unyonge na woga na matetemeko mengi.
4
Hata nilipowaambia mbiu yangu, sikutumia maneno ya werevu yenye nguvu ya kushinda, ila nimetumia Roho yenye nguvu,
5
kusudi mmtegemee Bwana, ila visiwe kwa kushindwa na werevu wa kimtu, ila kwa kushindwa na nguvu yake Mungu.
6
*Tena yako ya werevu wa kweli; tunawaambia wale wenye kuyatimiza yote. Lakini nayo siyo ya werevu wa ulimwengu huu, wala wa wakuu wa ulimwengu huu walio wenye kufa.
7
Ila yaliyo ya werevu wa Mungu ulio wa kweli ndiyo, tunayoyasema, nayo yalikuwa hayajatokea bado, maana yalikuwa yamefichwa; huko kale, ulimwengu ulipokuwa haujawa bado, Mungu aliyachagua yayo hayo, yatokee sasa kututukuza sisi.
8
Kwao wanaoutawala ulimwengu huu hakuna aliyeyatambua. Maana kama wangaliyatambua, wasingalimwamba msalabani Bwana aliye mwenye utukufu.
9
Ila ilikuwa, kama ilivyoandikwa: Jicho lisiyoyaona, sikio lisiyoyasikia, moyo wa mtu usiyoweza kuyatia mwake, ndiyo, Mungu aliyowaandalia wale wampendao.
10
Lakini sisi Mungu ametufunulia hayo alipotupa Roho wake. Kwani Roho huyapambanua mambo yote, hata vilindi vya Mungu
11
Kwani yuko mtu ayajuaye mambo ya mtu, isipokuwa roho yake yule mtu iliyomo mwake? Vivyo hivyo mambo ya Mungu nayo hakuna ayatambuaye, asipokuwa Roho wake Mungu.
12
Lakini sisi hatukupewa roho ya ulimwengu huu, ila tumepewa Roho iliyotoka kwa Mungu, tupate kuyajua, tuliyogawiwa na Mungu.
13
Nayo ndiyo, tuyasemayo; tena hatuyasemi kwa maneno, tuliyofundishwa na werevu wa kimtu, ila tulifundishwa na Roho; hivyo mambo ya Roho tunayapatia hata maneno ya Roho.
14
Lakini mtu anayeutii moyo wake tu hayafumbui ya Roho wake Mungu; huyawazia kuwa mapumbavu tu, hawezi kuyatambua, kwani hayo sharti yachunguzwe kwa nguvu ya Roho.
15
Lakini mtu anayemtii Roho huyachunguza yote, lakini mwenyewe hakuna, ambaye achunguzwa naye.
16
Maana: Yuko aliyeyatambua mawazo ya Bwana, amjulishe jambo? Lakini sisi tunayo mawazo yake Kristo.*
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16