bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Corinthians 10
1 Corinthians 10
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 11 →
1
*Ndugu, sitaki, ninyi mkose kujua, ya kuwa baba zetu wote walikwenda wakifunikwa na wingu, nao wote walipita baharini.
2
Wote wakabatiziwa Mose walipokuwa winguni na baharini.
3
Tena chakula cha Kiroho, walichokila wote, ni kile kimoja;
4
nacho kinywaji cha Kiroho, walichokinywa wote, ni kile kimoja. Maana walikunywa maji yaliyotoka katika mwamba wa Kiroho uliofuatana nao; nao mwamba huo ni Kristo.
5
Lakini wale wengi Mungu hakupendezwa nao, kwa hiyo walilazwa jangwani.
6
Hayo yalifanyika, tujifunzie mumo humo, sisi tusitende tamaa ya maovu, kama wale walivyokuwa na tamaa.
7
Wala msitambikie kinyago kama wengine wao! Kama ilivyoandikwa: Watu walikalia kula na kunywa, kisha wakainukia kucheza.
8
Tena tusifanye ugoni, kama wengine wao walivyoufanya, wakauawa siku moja watu 23000.
9
Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaangamizwa na nyoka.
10
Wala msinung'unike, kama wengine wao walivyonung'unika, wakaangamizwa na mwangamizaji.
11
Lakini hayo yote yaliwapata, tujifunzie mumo humo, yakaandikiwa kutuonya sisi tuliofika penye mwisho wa siku.
12
Kwa hiyo: ajiwaziaye kwamba amesimama, aangalie, asianguke!
13
Hamjaingiwa bado na jaribu lo lote linaloipita nguvu ya mtu. Lakini Mungu ni mwelekevu; hatawaacha ninyi, mjaribiwe na mambo yaupitayo uwezo wenu; lakini hapo, mtakapojaribiwa, atawapatia mzungu, mweze kuvumilia.*
14
Kwa hiyo, wenzangu wapendwa, yakimbieni matambiko ya mizimu!
15
Nasema nanyi, kwa kuwa m wenye akili; yatambueni ninyi, niyasemayo!
16
Kinyweo chenye mbaraka, tukibarikicho, hakitupatii bia ya damu yake Kristo? Mkate, tuumegao, hautupatii bia ya mwili wake Kristo?
17
Kwa sababu mkate ni mmoja, nasi tulio wengi tu mwili mmoja, maana sote twagawiwa huo mkate mmoja.*
18
Mwatazame walio Waisiraeli kwa kuzaliwa! Wenye kuzila nyama za tambiko sio wenye bia ya meza ya kutambikia?
19
Basi, nisemeje? Niseme: Nyama ya tambiko ni kitu? Au niseme: Mizimu ni kitu?
20
Siyo, maana wamizimu waitambikia mizimu yao, hawamtambikii Mungu. Nami sitaki, ninyi mwe wenye bia na mizimu.
21
Hamwezi kukinywa kinyweo cha Bwana nacho kinyweo cha mizimu; hamwezi kula mezani pa Bwana na mezani pa mizimu.
22
Au tumchokoze Bwana? Sisi tuko na nguvu kumshinda yeye?
23
Hakuna cho chote chenye mwiko, lakini sivyo vyote vifaavyo; hakuna cho chote chenye mwiko, lakini sivyo vyote vijengavyo.
24
Pasiwe na mtu mwenye kuyatafuta yaliyo yake, sharti ayatafute yaliyo ya mwenziwe!
25
Vyote vinavyouzwa sokoni vileni pasipo kuuliza vitokapo, mioyo isilemewe!
26
Kwani nchi hii ni yake Bwana navyo vyote vilivyomo.
27
Mtu asiyemtegemea Mungu akiwaalika, nanyi mkitaka kwenda, basi, vyote mnavyoandaliwa vileni pasipo kuuliza vitokapo mioyo isilemewe!
28
Lakini akiwaambia: Hii ni nyama ya tambiko, msiile kwa ajili yake yeye aliyewajulisha, tena kwa ajili ya mioyo isiyojua maana, isilemewe!
29
Sisemi hapa moyo wako unaojua maana, ila wa yule mwingine. Maana visivyo vya mwiko kwangu, vitaumbuliwaje na moyo wa mwingine asiye hivyo?
30
Mimi ninapovila kwa kugawiwa, ninabezwaje kwa vile, ninavyovipokea kwa Mungu?
31
Basi, mkila au mkinywa au mkifanya lo lote jingine, yafanyeni yote, yamtukuze Mungu!
32
Jiangalieni, msiwakwaze Wayuda wala Wagriki wala wateule wake Mungu!
33
Kama nami, nawapendeza wote kwa mambo yote, maana siyatafuti yanifaliayo mimi mwenyewe, ila yawafaliayo wale wengi, wapate kuokoka.
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 11 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16