bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Mark 1
Mark 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 2 →
1
Utume mwema wa Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, ulianza,
2
kama ulivyoandikwa na mfumbuaji Yesaya: Utaniona mimi, nikimtuma mjumbe wangu, akutangulie, aitengeneze njia yako.
3
Iko sauti ya mtu apigaye mbiu nyikani: Itengenezeni njia ya Bwana! Yanyosheni mapito yake!
4
Yohana Mbatizaji alikuwa nyikani akibatiza na kutangaza ubatizo wa kujutisha, wapate kuondolewa makosa.
5
Wakamtokea wote wa Yudea na wenyeji wote wa Yerusalemu, wakabatizwa naye katika mto wa Yordani wakiyaungama makosa yao.
6
Naye Yohana alikuwa amevaa nguo ya manyoya ya ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni pake, akala nzige na asali ya mwituni.
7
Akatangaza akisema: Nyuma yangu anakuja aliye na nguvu kunipita mimi, nami sifai kuinama, nimfungulie kanda za viatu vyake.
8
Mimi nimewabatiza kwa maji, lakini yeye atawabatiza kwa Roho takatifu.
9
Ikawa siku zile, Yesu akaja toka Nasareti wa Galilea, akabatizwa na Yohana mle Yordani.
10
Papo hapo alipotoka majini akaona, mbingu zikipasuka, akamwona Roho, anavyomshukia kama njiwa.
11
Sauti ikatoka mbinguni: Wewe ndiwe mwanangu mpendwa, nimependezwa na wewe.
12
Papo hapo Roho akamchukua, akampeleka nyikani.
13
Akawa huko nyikani siku 40 akijaribiwa na Satani, tena wenzake walikuwa nyama wa porini. Kisha malaika wakamtumikia.
14
Yohana alipokwisha fungwa, Yesu akaja Galilea, akautangaza Utume mwema wa Mungu,
15
akasema: Siku zimetimia, nao ufalme wa Mungu umekaribia. Juteni, mwutegemee Utume mwema!
16
Naye alipokuwa akitembea kandokando ya bahari ya Galilea, akamwona Simoni na Anderea, nduguye Simoni, wakitupa nyavu zao baharini, kwani walikuwa wavuvi.
17
Yesu akawaambia: Njoni, mnifuate! Nami nitawafanya kuwa wavua watu.
18
Papo hapo wakaziacha nyavu, wakamfuata.
19
Alipoendelea mbele kidogo, akamwona Yakobo, mwana wa Zebedeo, na Yohana nduguye; nao walikuwa chomboni wakizitengeneza nyavu.
20
Mara akawaita, nao wakamwacha baba yao Zebedeo mle chomboni pamoja na wafanya kazi, wakaja, wakamfuata nyuma yake.
21
Wakaenda, wakaingia Kapernaumu. Ilipokuwa siku ya mapumziko, akaiingia nyumba ya kuombea, akafundisha.
22
Wakashangazwa na mafundisho yake; kwani alikuwa akiwafundisha kama mwenye nguvu, si kama waandishi.
23
Humo nyumbani mwao mwa kuombea mkawa na mtu aliyekuwa na pepo mchafu; akapaza sauti
24
akisema: Tuko na jambo gani sisi na wewe, Yesu wa Nasareti? Umekuja kutuangamiza. Nakujua, kama u nani; ndiwe Mtakatifu wa Mungu.
25
Yesu alipomkaripia akisema: Nyamaza, umtoke!
26
ndipo, yule pepo mchafu alipomsukumasukuma, akalia kwa sauti kuu, kisha akamtoka.
27
Wote wakaingiwa na kituko, hata wakaulizana wao kwa wao wakisema: Hilo ni jambo gani? Ni ufundisho mpya wa kinguvu. Anawaagiza hata pepo wachafu, nao humtii.
28
Huo uvumi wake ukatoka, ukaenea upesi po pote katika nchi zote zilizozunguka Galilea.
29
Hapo walipotoka nyumbani mwa kuombea wakaingia pamoja na Yakobo na Yohana nyumbani mwao Simoni na Anderea.
30
Naye mama ya mkewe Simoni alikuwa amelala kwa kuwa na homa. Papo hapo, walipomwambia, alivyokuwa,
31
akamjia, akamwinua na kumshika mkono; ndipo, homa ilipomwacha, akawatumikia.
32
Ilipokuwa jioni, jua lilipokwisha kuchwa, wakampelekea wote waliokuwa hawawezi, nao waliopagawa na pepo,
33
mji wote ukawa umekusanyika mlangoni.
34
Akawaponya wengi waliokuwa hawawezi, wenye magonjwa mengi, akafukuza pepo wengi akiwakataza pepo kusema, ya kuwa walimjua.
35
Asubuhi na mapema sana akainuka, akatoka, akaenda zake mahali palipokuwa pasipo watu; hapo ndipo, alipomwomba Mungu.
36
Naye Simoni na wenziwe wakamfuata mbio;
37
walipomwona wakamwambia: Wote wanakutafuta.
38
Akawaambia: Twendeni pengine penye vijiji vya pembenipembeni, nipate kupiga mbiu humo namo! Kwani hiyo ndiyo, niliyojia.
39
Akaenda katika nchi yote ya Galilea, akapiga mbiu katika nyumba zao za kuombea, akafukuza pepo.
40
Mwenye ukoma akaja kwake, akambembeleza na kumpigia magoti akimwambia: Ukitaka waweza kunitakasa.
41
Ndipo, alipomwonea uchungu, akanyosha mkono, akamgusa, akamwambia: Nataka, utakaswe.
42
Mara ukoma ukamwondoka, akatakaswa.
43
Papo hapo akamkimbiza na kumkemea
44
akimwambia: Tazama, usimwambie mtu neno! Ila uende zako, ujionyeshe kwa mtambikaji, uvitoe vipaji kwa ajili ya kutakaswa kwako, Mose alivyoviagiza, vije vinishuhudie kwao!
45
Lakini alipotoka akaanza kutangaza mengi na kulisimulia jambo hilo po pote. Kwa hiyo Yesu hakuweza tena kuingia mjini waziwazi, ila alikuwa akikaa nje mahali palipokuwa pasipo watu, lakini watu wakamwendea toka pande zote.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16