bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Mark 8
Mark 8
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 9 →
1
Siku zile likakusanyika tena kundi la watu wengi; walipokosa vyakula, akawaita wanafunzi, akawaambia:
2
Kundi hili la watu nalionea uchungu, kwa kuwa wameshinda kwangu siku tatu, wasione chakula.
3
Kama ninawaaga, waende nyumbani kwao pasipo kula, watazimia njiani; tena wako waliotoka mbali.
4
Wanafunzi wake walipomjibu: Hapa nyikani mtu atawezaje kuwashibisha watu hawa mikate?
5
akawauliza: Mnayo mikate mingapi? Nao waliposema: Saba,
6
akawaagiza hao watu wengi, wakae chini, kisha akaitwaa ile mikate saba, akashukuru, akaimega, akawapa wanafunzi wake, wawapangie; nao wakawapangia wao wa hilo kundi la watu.
7
Tena walikuwa na visamaki vichache; navyo akaviombea, akasema, wawapangie hivi navyo.
8
Wakala, wakashiba; kisha wakaokota makombo ya mikate yaliyosalia, yakawa makanda saba.
9
Nao walikuwa kama 4000. Kisha akawaaga, waende zao.
10
Papo hapo akaingia chomboni pamoja na wanafunzi wake, akaja upande wa Dalmanuta.
11
Wakamtokea Mafariseo, wakanza kubisha naye, wakamjaribu wakitaka, afanye kielekezo kitokacho mbinguni.
12
Akapiga kite rohoni mwake, akasema: Mbona wao wa ukoo huu wanataka kielekezo? Kweli nawaambiani: Wao wa ukoo huu hawatapata kielekezo.
13
Kisha akawaacha, akajipakia tena chomboni, akaenda zake ng'ambo.
14
Walikuwa wamesahau kuchukua mikate; namo chomboni hawakuwa na mikate ila mmoja tu.
15
Akawaonya akisema: Tazameni, jiangalieni kwa ajili ya chachu ya Mafariseo na chachu ya Herode!
16
Ndipo, walipoyafikiri na kusemezana wao kwa wao: Ni kwa sababu hatunayo mikate.
17
Kwa kuwatambua akawaambia: Mbona mnafikiri hivyo, ya kuwa hamnayo mikate? Hamjaerevuka bado? Wala hamjajua maana? Mngaliko wenye mioyo iliyoshupaa?
18
Macho mnayo, lakini hamwoni? Nayo masikio mnayo, lakini hamsikii?
19
Wala hamwikumbuki ile mikate mitano, nilipoimegea wale 5000? Hapo mlijaza makapo mangapi mkiokota makombo? Wakamwambia: Kumi na mawili.
20
Wala hamwikumbuki ile mikate saba, nilipoivunjia wale 4000, mlijaza makanda mangapi mkiokota makombo? Wakamwambia: Saba.
21
Akawauliza: Hamjajua bado maana?
22
Walipoingia Beti-Saida, wakamletea kipofu, wakambembeleza, amguse.
23
Akaushika mkono wa kipofu, akamwongoza, watoke kijijini, akamtemea mate machoni, akambandikia mikono, akamwuliza: Kiko, unachokiona?
24
Yule akainua macho, akasema: Naona watu wanaotembea, wanaonekana kuwa kama miti.
25
Hapo akambandikia mikono tena machoni pake, akamwagiza kutazama tena; ndipo, macho yake yaliporudia kuwa mazima, akaona vitu vyote waziwazi, hata vilivyoko mbali.
26
Kisha akamtuma, aende nyumbani mwake, akisema: Kijijini usimwingie! Wala usimwambie mtu wa humu kijijini!
27
Yesu na wanafunzi wake wakatoka, waingie vijiji vya upande wa Kesaria-Filipi. Walipokuwa njiani, akawauliza wanafunzi wake akiwaambia: Watu hunisema kuwa ni nani?
28
Nao wakamwambia wakisema: Wanakusema kuwa u Yohana Mbatizaji, wengine: Elia, wengine: Mmoja wao wafumbuaji.
29
Kisha akawauliza: Lakini ninyi mnanisema kuwa ni nani? Petero akajibu akimwambia: Wewe ndiwe Kristo.
30
Ndipo, alipowatisha, wasimwambie mtu hilo neno lake.
31
Akaanza kuwafundisha, ya kuwa imempasa Mwana wa mtu kuteswa mengi na kukataliwa nao wazee na watambikaji wakuu na waandishi, mpaka auawe, kisha afufuke, siku tatu zitakapopita.
32
Neno hili akalisema waziwazi. Ndipo, Petero alipomchukua pembeni, akaanza kumtisha.
33
Naye akageuka nyuma, akawatazama wanafunzi wake, akamtisha Petero akisema: Niondokea hapa nyuma yangu, wewe Satani! Kwani wewe huyawazi mambo ya Kimungu, ila unayawaza ya kiwatu tu.
34
Akaliita kundi la watu, limjie pamoja na wanafunzi wake, akawaambia: Mtu akitaka kunifuata mimi ajikataze mapenzi yake, ajitwishe nao msalaba wake, kisha anifuate!
35
Maana mtu anayetaka kuiokoa roho yake ataiangamiza. Lakini mtu atakayeiangamiza roho yake kwa ajili yangu mimi na kwa ajili ya Utume mwema ataiokoa.
36
Kwani mtu vinamfaa nini kuvichuma vya ulimwengu wote, roho yake ikiponzwa navyo?
37
Kwani mtu atoe nini, aikomboe roho yake?
38
Kwani mtu atakayenionea soni mimi na maneno yangu kwao wa kizazi hiki kilicho chenye ugoni na ukosaji, basi, naye Mwana wa mtu atamwonea soni huyo atakapokuja mwenye utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 9 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16