bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Mark 3
Mark 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 4 →
1
Alipoingia tena katika nyumba ya kuombea, mle mlikuwa na mtu mwenye mkono uliokuwa umekaukiana.
2
Wakamtunduia, kama atamponya siku ya mapumziko, wapate kumsuta.
3
Akamwambia yule mwenye mkono uliokaukiana: Inuka, uje hapa katikati!
4
Kisha akawauliza: Iko ruhusa siku ya mapumziko kufanya mema au kufanya maovu? kuponya roho ya mtu au kuiua? Waliponyamaza,
5
ukali ukamjia, akawatazama waliokuwako, akausikitikia ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu: Unyoshe mkono wako! Alipounyosha, huo mkono wake ukageuka kuwa mzima.
6
Mafariseo wakatoka, papo hapo wao pamoja na watu wa Herode wakamlia njama ya kumwangamiza.
7
Yesu akaondoka pamoja na wanafunzi wake kwenda upande wa baharini. Kundi la watu wengi sana waliotoka Galilea likamfuata. Tena wengi waliotoka Yudea
8
na Yerusalemu na Idumea na ng'ambo ya Yordani na upande wa Tiro na Sidoni, wakamwendea, kwani waliyasikia yote, aliyoyafanya.
9
Akawaambia wanafunzi wake, wamtengenezee chombo kidogo kwa ajili ya makundi ya watu, wasije kumsongasonga.
10
Kwa kuwa aliponya wengi, wote walioteseka wakamwangukiaangukia, wapate kumgusa tu.
11
Hata pepo wachafu, kila walipomwona, wakamwangukia wakipiga kelele wakisema: Wewe ndiwe Mwana wa Mungu!
12
Akawatisha sana, wasimtangaze.
13
Kisha akapanda mlimani, akawaita, aliowataka mwenyewe; wakaja kwake.
14
Akawaweka kumi na wawili, wawe pamoja naye, apate kuwatuma kupiga mbiu,
15
wakiisha kupewa nguvu za kufukuza pepo.
16
Akawaweka hao kumi na wawili: Simoni akampa jina la Petero.
17
Yakobo, mwana wa Zebedeo, na Yohana, nduguye Yakobo, akawapa jina la Boanerge, ni kwamba: Wana wa Ngurumo.
18
Akawaweka nao akina Anderea na Filipo na Bartolomeo na Mateo na Toma na Yakobo, mwana wa Alfeo, na Tadeo na Simoni wa Kana
19
na Yuda Iskariota aliyemchongea halafu.
20
Alipoingia nyumbani, ndipo, kundi la watu lilipokusanyika tena, wenyewe wasiweze hata kula mkate.
21
Lakini ndugu zake walipoyasikia wakatoka, waje kumchukua, kwa maana walisema: Amepatwa na kichaa.
22
Nao waandishi waliokuwa wametelemka toka Yerusalemu walisema: Ana Belzebuli. Tena wakasema: Nguvu ya huyo mkuu wa pepo ndiyo, anayofukuzia pepo.
23
Akawaita, akawaambia kwa mifano: Satani awezaje kumfukuza Satani mwenziwe?
24
Ufalme unapogombana wao kwa wao, ufalme huo hausimamiki.
25
Nayo nyumba inapogombana wao kwa wao, nyumba hiyo haitaweza kusimama.
26
Naye Satani anapojiinukia mwenyewe na kujigombanisha hawezi kusimama, ila ataishiwa.
27
Hakuna mtu awezaye kuingia katika nyumba ya mwenye nguvu, aviteke vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu; kisha ataweza kuiteka nyumba yake.
28
Kweli nawaambiani: Wana wa watu wataondolewa yote, hata maneno yote ya kumbeza Mungu.
29
Lakini mtu atakayembeza Roho Mtakatifu hapati kuondolewa kale na kale, ila kosa lake litamkalia pasipo mwisho.
30
Aliwaambia hivyo kwa vile walivyosema: Ana pepo mchafu.
31
Kisha mama yake na ndugu zake wakaja, wakasimama nje, wakatuma mtu kwake, amwite.
32
Kundi la watu likawamo likimzunguka, wakamwambia: Tazama, mama yako na ndugu zako wako nje, wanakutafuta.
33
Akajibu akiwaambia: Aliye mama yangu ni nani? Ndugu zangu ni akina nani?
34
Akawatazama waliokaa huko na huko, wakimzunguka pande zote, akasema: Watazameni walio mama yangu na ndugu zangu!
35
Mtu ye yote atakayeyafanya, Mungu ayatakayo, huyo ndiye ndugu yangu na dada yangu na mama yangu.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16