bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Mark 5
Mark 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 6 →
1
Wakafika ng'ambo ya bahari katika nchi ya Wagerasi.
2
Alipotoka chomboni papo hapo akakutana na mtu mwenye pepo mchafu aliyetoka penye makaburi.
3
Kwa kuwa hukaa pale penye makaburi, hakuwako mtu aliyeweza kumfunga kwa mnyororo wo wote.
4
Kwani alikuwa amefungwa mara nyingi kwa mapingu na kwa minyororo, lakini minyororo ikararuliwa naye, nayo mapingu yakasagwa naye, mpaka yakikatika, kwa hiyo hakukuwako kabisa mtu mwenye nguvu za kumshinda.
5
Siku zote mchana kutwa alikuwa penye makaburi nako milimani akipiga makelele na kujipigapiga mawe mwenyewe.
6
Alipomwona Yesu, yuko mbali bado, akapiga mbio, akaja, akamwangukia,
7
akapaza sana sauti akisema: Tuko na jambo gani mimi na wewe Yesu, Mwana wa Mungu Alioko huko juu? Nakuapisha kwa Mungu, usiniumize!
8
Kwani alikuwa amemwambia: Wee pepo mchafu, umtoke mtu huyu!
9
Alipomwuliza: Jina lako nani? akamwambia: Jina langu mimi Maelfu, kwa kuwa tumo wengi.
10
Akambembeleza sana, asiwafukuze, waitoke nchi ile.
11
Basi, kulikuwako kule mlimani kundi kubwa la nguruwe waliokuwako malishoni.
12
Wakambembeleza wakisema: Tutume kwenda kwao wale nguruwe, tupate kuwaingia!
13
Alipowapa ruhusa, pepo wachafu wakamtoka, wakawaingia nguruwe; ndipo, kundi lilipotelemka mbio mwambani, wakaingia baharini, wapata kama 2000, wakatoswa baharini.
14
Lakini wachungaji wao wakakimbia, wakayatangaza mjini na mashambani. Watu wakaja, watazame, lililofanyika lilivyo.
15
Walipofika kwa Yesu na kumtazama yule mtu aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu wa Maelfu, anavyokaa amevaa nguo, tena ana akili zake, wakashikwa na woga.
16
Nao walioyaona wakawasimulia, ya mwenye pepo yalivyoendelea, hata yale ya nguruwe.
17
Wakaanza kumbembeleza, atoke mipakani kwao.
18
Alipojipakia chomboni, yule mtu aliyekuwa amepagawa na pepo akambembeleza, afuatane pamoja naye.
19
Lakini hakumwitikia, ila akamwambia: Uende zako nyumbani mwako kwa ndugu zako ukawasimulie yote, Bwana aliyokutendea kwa kukuhurumia!
20
Ndipo, alipokwenda zake, akaanza kuyatangaza katika ile Miji Kumi yote, Yesu aliyomtendea; watu wote wakastaajabu.
21
Yesu alipokwisha vuka tena chomboni kuja ng'ambo, kundi la watu wengi likakusanyika hapo, alipokuwa kandokando ya bahari.
22
Akaja mmoja wao majumbe wa nyumba ya kuombea, jina lake Yairo; alipomwona akamwangukia miguuni pake,
23
akambembeleza sana akisema: Kibinti changu yumo kufani; nakuomba, uje, umbandikie mikono, apate kupona na kuwa mzima tena.
24
Akaondoka, akaenda naye; watu wengi sana wakamfuata wakimsongasonga.
25
Kukawa na mwanamke mwenye ugonjwa wa kutoka damu miaka 12.
26
Huyo alikuwa amepata maumivu mengi kwa waganga wengi; hivyo alizimaliza mali zake zote, lakini hawakumfaa hata kidogo, ugonjwa wake ukakaza tu kuwa mbaya.
27
Alipoyasikia mambo ya Yesu akaliingia kundi la watu, akamjia nyuma, akaigusa nguo yake.
28
Maana alisema: Hata nikizigusa nguo zake tu nitapona.
29
Papo hapo kijitojito cha damu yake kikakauka, akajiona mwilini, ya kuwa amelipona teso lake.
30
Papo hapo Yesu akatambua mwilini mwake, ya kuwa nguvu imemtoka; akaligeukia kundi la watu, akasema: Yuko nani aliyenigusa nguo zangu?
31
Wanafunzi wake wakamwambia: Unaliona kundi la watu, linakusongasonga, nawe unauliza: Yuko nani aliyenigusa?
32
Alipotazama huko na huko, apate kumwona aliyemgusa,
33
yule mwanamke akashikwa na woga, akatetemeka, kwani alijua lililompata; kwa hiyo akaja, akamwangukia, akamwambia yote, yalivyokuwa kweli.
34
Naye akamwambia: Mwanangu, kunitegemea kwako kumekuponya, nenda na kutengemana, uwe mzima, teso lako lisikurudie tena!
35
Angali akisema, wakaja watu wa jumbe wa nyumba ya kuombea, wakasema: Binti yako amekwisha kufa; mfunzi unamsumbulia nini tena?
36
Yesu alipoyasikia maneno haya, yakisemwa, akamwambia jumbe wa nyumba ya kuombea: Usiogope, nitegemea tu!
37
kisha hakumpa mtu mwingine ruhusa kufuatana naye, ila Petero na Yakobo na Yohana, nduguye Yakobo.
38
Walipoingia nyumbani mwa jumbe wa nyumba ya kuombea, akaona makelele ya watu, wakilia na kuomboleza sana.
39
Akaingia, akawaambia: Mnapigia nini makelele na kulia? Kitoto hakufa, ila amelala usingizi tu;
40
ndipo, walipomcheka sana. Lakini alipokwisha kuwafukuza wote akamchukua baba ya kitoto na mama yake na wale waliokuwa pamoja naye, akaingia mle, yule kitoto alimokuwa.
41
Akamshika kitoto mkono, akamwambia: Talita kumi! ni kwamba: Kijana, nakuambia: Inuka!
42
Papo hapo kijana akafufuka, akaendaenda, kwani alikuwa wa miaka 12. Ndipo, waliposhangaa ushangao mwingi.
43
Akawakataza sana, wasilitambulishe neno hili kwa mtu ye yote; kisha akasema, kijana apewe chakula.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16