bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Mark 14
Mark 14
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 15 →
1
Palikuwa pamesalia siku mbili kuwa sikukuu ya Pasaka na ya mikate isiyotiwa chachu. Nao watambikaji wakuu na waandishi wakatafuta kumkamata kwa werevu, wapate kumwua;
2
lakini walisema: Kwanza sikukuu ipite, watu wasije, wakafanya fujo!
3
Naye alipokuwa Betania nyumbani mwa Simoni Mkoma akikaa chakulani, akamjia mwanamke mwenye kichupa chepe cha jiwe kilichojaa mafuta ya maua yanayoitwa Narada; ni yenye bei kubwa, nayo yalikuwa hayakuchanganywa na mengine. Akakivunja kile kichupa, akayamiminia kichwani pake.
4
Mlikuwamo waliochukiwa mioyoni mwao kwamba: Upotevu huu wa haya mafuta mazuri sana ni wa nini?
5
Kwani mafuta haya yangaliwezekana kuuzwa kwa shilingi 300 na kupita, wakapewa maskini! Kwa hiyo wakamfokea sana.
6
Lakini Yesu akasema: Mwacheni! Mbona mnamsikitisha? Amenitendea tendo zuri.
7
Kwani maskini mnao kwenu siku zote, kila mnapotaka mweze kuwafanyia vema; lakini mimi hamwi nami siku zote.
8
Amefanya, alivyoweza; ameanza kuupaka mwili wangu mafuta haya, autengenezee kuzikwa.
9
Kweli nawaambiani: Po pote katika ulimwengu wote, patakapotangazwa huu Utume mwema, patasemwa nacho hiki, alichokitenda yeye, naye akumbukwe.
10
Kisha Yuda Iskariota aliyekuwa mwenzao wale kumi na wawili akaenda zake kwa watambikaji wakuu, amtie mikononi mwao.
11
Nao walipoyasikia wakafurahi, wakaagana naye kumpa fedha. Ndipo, alipotafuta njia iliyofaa, amtoe.
12
Siku ya kwanza ya kula mikate isiyotiwa chachu, watu walipochinjia kondoo ya Pasaka, wanafunzi wake wakamwuliza: Unataka, twende, tukuandalie wapi, uile kondoo ya Pasaka?
13
Akawatuma wanafunzi wake wawili, akawaambia: Nendeni mjini! Humo mtakutana na mtu anayechukua mtungi wa maji, mfuateni!
14
Mle atakamoingia mwambieni mwenye nyumba: Mfunzi anauliza: Kiko wapi chumba cha kukaa mimi, ndimo niile kondoo ya Pasaka pamoja na wanafunzi wangu?
15
Ndipo, mwenyewe atakapowaonyesha chumba kikubwa kilichokwisha kutandikwa; namo mle tuandalieni!
16
Wale wanafunzi wakatoka, wakaenda, wakaingia mjini, wakaona, kama alivyowaambia, wakaiandaa kondoo ya Pasaka.
17
Ilipokuwa jioni, akaja pamoja na wale kumi na wawili.
18
Walipokaa wakila, Yesu akasema: Kweli nawaambiani: Mwenzenu mmoja anayekula pamoja nami atanichongea.
19
Wakaanza kusikitika na kumwuliza mmoja mmoja: Ni mimi?
20
Naye akawaambia: Ninyi kumi na wawili mwenzenu aliyetowelea pamoja nami bakulini ndiye.
21
Mwana wa mtu anakwenda njia yake, kama alivyoandikiwa; lakini yule mtu, ambaye Mwana wa mtu atachongewa naye, atapatwa na mambo. Ingalimfalia yule mtu, kama-asingalizaliwa.
22
Walipokuwa wakila, akatwaa mkate, akauombea, akaumega, akawapa, akasema: Twaeni! Huu ndio mwili wangu.
23
Kisha akatwaa kinyweo, akashukuru, akawapa, wakanywa wote humo,
24
akawaambia: Hii ndiyo damu yangu ya Agano Jipya inayomwagwa kwa ajili ya wengi.
25
Kweli nawaambiani: Tangu sasa sitayanywa tena mazao ya mizabibu mpaka siku ile, nitakapoyanywa mapya katika ufalme wa Mungu.
26
Walipokwisha kuimba wakatoka kwenda mlimani pa michekele.
27
Yesu akawaambia: Nyote mtajikwaa, kwani imeandikwa: Nitampiga mchungaji, kondoo watawanyike;
28
lakini nitakapokwisha kufufuliwa nitawatangulia kwenda Galilea.
29
Ndipo, Petero alipomwambia: Ijapokuwa, wote wajikwae, lakini mimi sio.
30
Yesu akamwambia: Kweli nakuambia: Usiku huu wa leo jogoo atakapokuwa hajawika mara mbili, utakuwa umenikana mara tatu.
31
Naye akakaza mno kusema: Hata ijaponipasa kufa pamoja nawe, sitakukana kabisa. Nao wote wakasema vivyo hivyo.
32
Walipofika mahali, jina lake Getisemane, akawaambia wanafunzi wake: Kaeni hapa, mpaka niishe kuomba!
33
Akamchukua Petero na Yakobo na Yohana, akaenda nao, akaanza kuingiwa na kituko na kuhangaika,
34
akawaambia: Roho yangu inaumizwa sana na masikitiko, imesalia kufa tu. Kaeni papa hapa, mkeshe!
35
Akaendelea mbele kidogo, akaanguka chini, akaomba, ikiwezekana, saa hiyo impite, isimfikie.
36
Akasema: Aba baba, yote yanawezekana kwako; kipitishe kinyweo hiki, nisikinywe! Lakini yasifanyike, niyatakayo mimi, ila yafanyike, uyatakayo wewe!
37
Alipokuja akawakuta, wamelala usingizi, akamwambia Petero: Simoni, umelala usingizi? Hukuweza kukesha saa moja tu?
38
Kesheni na kuomba, msije kuingia majaribuni! Roho inataka kuitikia, lakini mwili ni mnyonge.
39
Akaenda tena, akaomba na kusema maneno yaleyale.
40
Alipokuja tena akawakuta, wamelala usingizi, kwani macho yao yalikuwa mazito, hawakujua ya kumjibu.
41
Alipokuja mara ya tatu akawaambia: Mwafuliza kulala usingizi, uchovu uwatoke? Pametimia, saa imefika; tazameni, Mwana wa mtu anatiwa mikononi mwa wakosaji!
42
Inukeni, twende! Tazameni, mwenye kunichongea yuko karibu!
43
Angali akisema, papo hapo akaja Yuda, mmoja wao wale kumi na wawili, pamoja na kundi la watu wengi wenye panga na rungu waliotoka kwa watambikaji wakuu na kwa waandishi na kwa wazee.
44
Lakini mwenye kumchongea alikuwa amewapa kielekezo akisema: Nitakayemnonea ndiye, mkamateni, mwende naye mkimwangalia sana!
45
Naye alipofika, mara akamjia, akasema: Mfunzi mkuu! akamnonea;
46
ndipo, walipomkamata kwa mikono yao.
47
Lakini mmoja wao waliosimama hapo akauchomoa upanga wake, akampiga mtumwa wa mtambikaji mkuu, akamkata sikio.
48
Lakini Yesu akajibu, akawaambia: Mmetoka wenye panga na rungu, mnikamate mimi, kama watu wanavyomwendea mnyang'anyi.
49
Kila siku nilikuwa kwenu hapo Patakatifu nikifundisha, lakini hamkunikamata; lakini yamekuwapo, Maandiko yatimizwe.
50
Hapo waliokuwa naye wakamwacha, wakakimbia wote.
51
Kulikuwa na kijana mmoja aliyefuatana naye, alikuwa ameufunika uchi wake kwa kitambaa cha bafta tu. Lakini walipomkamata,
52
akakiacha kile kitambaa cha bafta, akakimbia mwenye uchi.
53
Wakampeleka Yesu kwa mtambikaji mkuu. Wakakusanyika wote, watambikaji wakuu na wazee na waandishi.
54
Naye Petero akamfuata mbalimbali, mpaka akaingia uani kwa mtambikaji mkuu, akakaa pamoja na watumishi penye mwangaza akiota moto.
55
Lakini watambikaji wakuu na baraza ya wakuu wote wakamtafutia Yesu ushuhuda, wapate kumwua, lakini hawakuupata.
56
Kwani wengi walimshuhudia ya uwongo, lakini ushuhuda wao haukupatana.
57
Kisha wakainuka wengine, wakamshuhudia ya uwongo na kusema:
58
Sisi tumesikia, alivyosema: Mimi nitalivunja Jumba hili la Mungu lililojengwa na mikono, tena nitajenga jingine muda wa siku tatu lisilojengwa na mikono.
59
Lakini hata hivyo ushuhuda wao haukupatana.
60
Ndipo, mtambikaji mkuu alipoinuka, akaja katikati, akamwuliza Yesu akisema: Hujibu neno, hawa wanayokusimangia?
61
Lakini akanyamaza kimya, asimjibu neno. Mtambikaji mkuu akamwuliza tena akimwambia: Wewe ndiwe Kristo, mwana wake Mtukufu?
62
Yesu akasema: Mimi ndiye. Nanyi mtamwona Mwana wa mtu, anavyokaa kuumeni kwa nguvu, tena atakavyokuja na mawingu ya mbinguni.
63
Ndipo, mtambikaji mkuu alipozirarua nguo zake, akasema: Mashahidi tunawatakia nini tena?
64
Mmesikia, anavyombeza Mungu. Mwaonaje? Nao wote wakamhukumu kwamba: Amepaswa na kufa.
65
Kisha wengine wakaanza kumtemea mate, tena wakamfunika uso, wakampiga makonde, wakamwambia: Fumbua! Nao watumishi wakamchukua, wakampiga makofi.
66
Naye Petero alipokuwa amekaa chini uani, akaja mmoja wao vijakazi wa mtambikaji mkuu.
67
Alipomwona Petero, alivyoota moto, akamchungulia, akasema: Hata wewe ulikuwa pamoja na yule Yesu wa Nasareti.
68
Akakana akisema: Sijui, wala sitambui, wewe unayoyasema. Kisha akatoka kufika nje ukumbini.
69
Yule kijakazi alipomwona, akaanza tena kuwaambia waliosimama pale: Huyu ni mwenzao.
70
Lakini akakana tena. Tena punde kidogo waliosimama pale wakamwambia Petero: Kweli u mwenzao, kwani nawe u Mgalilea.
71
Ndipo, alipoanza kujiapiza na kuapa akisema: Simjui mtu huyo, mnayemsema.
72
Mara hiyo jogoo akawika mara ya pili. Hapo Petero akalikumbuka lile neno, kama Yesu alivyomwambia: Jogoo atakapokuwa hajawika mara mbili, utakuwa umenikana mara tatu. Alipovifikiri akaanza kulia.
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 15 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16