bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Mark 6
Mark 6
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 7 →
1
Akatoka kule, akaenda kwao, alikokulia, nao wanafunzi wake wakamfuata.
2
Ilipokuwa siku ya mapumziko, akaanza kufundisha katika nyumba ya kuombea, nao wengi waliomsikia wakashangaa, wakasema: Huyu haya ameyapata wapi? Werevu huu ulio wa kweli amepewa na nani? Hizo nguvu nazo zinazotendwa na mikono yake ni nguvu gani?
3
Huyu si seremala, mwana wa Maria? Huyu si ndugu yao Yakobo na Yose na Yuda na Simoni? Nao maumbu zake hawako huku kwetu? Wakajikwaa kwake.
4
Yesu akawaambia: Mfumbuaji habezwi, isipokuwa kwao, alikokulia, na kwa ndugu zake namo nyumbani mwake.
5
Kwa hiyo hakuweza kufanya kule la nguvu hata moja, ila wanyonge wachache akawabandikia mikono, akawaponya.
6
Akastaajabu, jinsi walivyokataa kumtegemea.
7
Akaenda akizunguka katika vijiji vya pembenipembeni na kufundisha watu. Akawaita wale kumi na wawili, akaanza kuwatuma wawiliwawili, akawapa nguvu za kufukuza pepo wachafu.
8
Akawaagiza, washike fimbo tu, wasichukue kingine cha njiani, wala chakula wala mkoba wala senti mishipini.
9
Mwende mmevaa viatu, lakini msivae nguo mbili!
10
Akawaambia: Kila mtakamoingia nyumbani, kaeni mwake, mpaka mtakapotoka tena!
11
Napo mahali, wasipowapokea, wasiwasikilize, basi, tokeni pale na kuyakung'uta mavumbi yaliyoishika miguu yenu, yaje yanishuhudie kwao!
12
Kisha wakatoka, wakaenda na kutangaza, watu wajute.
13
Wakafukuza pepo wengi, wakapaka wanyonge wengi mafuta, wakawaponya.
14
Mfalme Herode akayasikia, kwani Jina lake lilivuma, maana watu walisema: Yohana Mbatizaji amefufuka katika wafu, kwa sababu hii nguvu hizo humtendesha kazi.
15
Lakini wengine walisema: Ndiye Elia; wengine tena walisema: Ni mfumbuaji kama wale wafumbuaji wenzake.
16
Lakini Herode alipoyasikia akasema: Ndiye Yohana, niliyemkata kichwa mimi, huyo amefufuka.
17
Kwani Herode mwenyewe alikuwa ametuma kumkamata Yohana na kumfunga kifungoni kwa ajili ya Herodia, mke wa nduguye, Filipo, ambaye alikuwa amemwoa.
18
Kwani Yohana alimwambia Herode: Ni mwiko kwako kuwa na mke wa nduguyo.
19
Lakini Herodia alimvizia, akataka kumwua, asiweze.
20
Kwani Herode alimwogopa Yohana, kwa vile, alivyomjua kuwa mtu mwongofu na mtakatifu, akamshika na kumlinda. Naye alipomsikia mara kwa mara akahangaishwa sana moyoni, tena akapendezwa kumsikiliza.
21
Siku iliyofaa ya kumpata ilikuwa sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode; ndipo, alipowaalika chakulani watawala miji yake na wakubwa wa askari na watu wenye cheo wa Galilea.
22
Binti Herodia alipoingia na kucheza ngoma, akampendeza Herode na wale waliokaa pamoja naye chakulani. Ndipo, mfalme alipomwambia huyo msichana:
23
Niombe kila, utakacho! nitakupa; kisha akamwapia: Cho chote, utakachoniomba, nitakupa, ijapo iwe nusu ya ufalme wangu.
24
Yule akatoka, akamwuliza mama yake: Niombe nini? Naye akasema: Kichwa chake Yohana Mbatizaji!
25
Papo hapo akaingia mbio kwa mfalme, akaomba akisema: Nataka, unipe sasa hivi katika chano kichwa chake Yohana Mbatizaji.
26
Mfalme akasikitika sana, lakini kwa ajili ya viapo vyake na kwa ajili ya wale waliokaa chakulani hakutaka kumnyima.
27
Ndipo, mfalme alipotuma askari, akamwagiza, akilete kile kichwa chake.
28
Yule akaenda, akamkata kichwa chake mle kifungoni, kisha akakileta katika chano, akampa msichana, naye msichana akampa mama yake.
29
Wanafunzi wake walipoyasikia wakaja, wakautwaa mwili wake, wakauweka kaburini.
30
Nao mitume wakakusanyika kwa Yesu, wakamsimulia mambo yote, waliyoyafanya nayo waliyoyafundisha.
31
Akawaambia: Njoni ninyi peke yenu, twende mahali pasipo na watu, mpumzike kidogo! Kwani watu wengi walikuwa wakija, tena wakienda, wasipate hata kula.
32
Wakaondoka, wakaenda chomboni peke yao mahali palipokuwa pasipo watu.
33
Watu walipowaona, wakitoka, nao wengi walipotambua, wanapokwenda, wakatoka miji yote kwa miguu, wakapiga mbio kuwakuta palepale, wakatangulia kufika.
34
Alipotoka chomboni akaona, watu ni wengi sana, akawaonea uchungu, kwani walikuwa kama kondoo wasio na mchungaji, akaanza kuwafundisha mengi.
35
Saa zilipofika za jioni, wanafunzi wake wakamjia, wakasema: Hapa tulipo ni nyika, nazo saa zimefika za jioni.
36
Uwaage watu, waende zao mashambani na vijijini huko pembenipembeni, wajinunulie vyakula!
37
Lakini akawajibu akiwaambia: Wapeni ninyi vyakula! Wakamwambia: Twende, tununue mikate ya shilingi 200, tuwape, wale?
38
Akawauliza: Mnayo mikate mingapi? Haya! Nendeni, mtazame! Walipoijua wakasema: Mitano, tena visamaki viwili.
39
Akawaagiza wote, wakae mafungumafungu uwandani penye majani.
40
Wakakaa kikao kwa kikao, pengine mia, pengine hamsini.
41
Akaitwaa ile mikate mitano na vile visamaki viwili, akatazama juu mbinguni, akaviombea, akawamegeamegea ile mikate, akawapa wanafunzi, wawapangie; navyo vile visamaki viwili akawagawia wote.
42
Wakala wote, wakashiba.
43
Kisha wakaokota makombo ya mikate wakajaza vikapu kumi na viwili pamoja na vipande vya samaki.
44
Nao waliokula ile mikate walikuwa 5000 waume tu.
45
Papo hapo akawashurutisha wanafunzi wake, waingie chomboni, wamtangulie kwenda ng'ambo huko Beti-Saida, mpaka yeye kwanza aliage kundi la watu.
46
Naye alipokwisha kuwaaga akaondoka kwenda mlimani kuomba.
47
Jua lilipokwisha kuchwa, chombo kilikuwa katikati ya bahari, naye mwenyewe alikuwa peke yake pwani.
48
Akawaona, wakihangaishwa, wasiweze kwendelea, kwani upepo uliwatokea mbele. Ilipofika zamu ya nne ya usiku, akawajia akienda juu ya bahari, akataka kuwapita.
49
Nao walipomwona, anavyokwenda juu ya bahari, wakawaza kuwa ni mzimu, wakapiga makelele,
50
kwani wote walimwona, wakatetemeka. Papo hapo yeye akasema nao akawaambia: Tulieni! Ni miye, msiogope!
51
Alipowapandia chomboni, upepo ukakoma. Ndipo, walipostuka na kushangaa mno mioyoni mwao;
52
kwani hawajaelewa maana ya ile mikate, mioyo yao nayo ilikuwa imeshupaa.
53
Walipokwisha vuka wakafika nchini kwa Genesareti, wakatia nanga hapo.
54
Nao walipotoka chomboni, papo hapo watu wakamtambua;
55
wakaenda mbio wakiizunguka nchi ile yote, wakaanza kuwachukua vitandani waliokuwa hawawezi, wakaenda nao huko na huko, walikomsikia, ya kuwa yeye yuko.
56
Kila alipoingia katika vijiji au miji au mashamba waliwaweka wagonjwa sokoni, wakambembeleza, wamguse pindo la lanzu yake tu; nao wote walioligusa wakapona.
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 7 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16