bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Mark 15
Mark 15
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 16 →
1
Asubuhi kulipokucha, papo hapo watambikaji wakuu wakala njama pamoja na wazee na waandishi nao wote wa baraza ya wakuu wote, wakamfunga Yesu, wakampeleka, wakamtia mikononi mwa Pilato.
2
Pilato alipomwuliza: Wewe ndiwe mfalme wa Wayuda? akamjibu akimwambia: Wewe unavyosema, ndivyo.
3
Watambikaji wakuu walipomsuta mengi,
4
Pilato akamwuliza tena: Hujibu neno? Tazama yote, wanayokusuta!
5
Lakini Yesu hakujibu neno tena, ikawa, Pilato akastaajabu.
6
Kwa desturi ya sikukuu huwafungulia mfungwa mmoja, waliyemtaka.
7
Kulikuwako mtu, jina lake Baraba, alifungwa pamoja na watu waliofunga kondo na kuua watu.
8
Watu wengi walipokwenda bomani kwa kutaka, kwanza awafanyie, kama alivyozoea,
9
Pilato akawajibu akisema: Mwataka, niwafungulie mfalme wa Wayuda?
10
Kwani alitambua, ya kuwa watambikaji wakuu walikuwa wamemtoa kwa wivu.
11
Lakini watambikaji wakuu wakalichochea hilo kundi la watu, sharti awafungulie Baraba.
12
Pilato akajibu tena akiwaambia: Basi, nimfanyie nini huyu, mnayemwita mfalme wa Wayuda?
13
Wakapiga kelele tena kwamba: Mwambe msalabani!
14
Pilato alipowauliza: Ni kiovu gani alichokifanya? wakakaza kupiga makelele kwamba: Mwambe msalabani!
15
Ndipo, Pilato, kwa kuwa alitaka kuyafanya yanayopendeza watu, alipowafungulia Baraba, lakini Yesu akamtoa, apigwe viboko, kisha awambwe msalabani.
16
Nao askari wakampeleka, wakamwingiza uani mwa bomani, wakakiita kikosi chote cha askari, wakusanyike.
17
Wakamvika nguo nyekundu, wakasuka kilemba cha miiba, wakamvika kichwani,
18
wakaanza kumwamkia: Pongezi, mfalme wa Wayuda!
19
Kisha wakampiga kichwani kwa mwanzi, wakamtemea mate, wakampigia magoti na kumwangukia.
20
Walipokwisha kumfyoza, wakamvua ile nguo nyekundu na kumvika nguo zake, wakampeleka nje, waje, wamwambe msalabani.
21
Wakakamata mtu aliyepiga akitoka shambani; ni Simoni wa Kirene, baba yao Alekisandro na Rufu, wakamshurutisha, amchukulie msalaba wake.
22
Wakampeleka mahali pa Golgota, maana yake ni kwamba: Fuvu la kichwa.
23
Wakampa mvinyo iliyochanganyika na manemane, lakini hakunywa.
24
Walipokwisha kumwamba msalabani, wakazigawanya nguo zake na kuzipigia kura, ndizo mtu achukue.
25
Lakini ilikuwa saa tatu, walipomwamba msalabani.
26
Juu yake kulikuwa na andiko la mashtaka yake la kwamba: MFALME WA WAYUDA.
27
Pamoja naye wakawamba misalabani wanyang'anyi wawili, mmoja kuumeni, mmoja kushotoni kwake.
28
Ndipo, lilipotimia lile neno la kwamba: Akahesabiwa kuwa mwenzao wapotovu.
29
Waliopita wakamtukana, wakavitingisha vichwa vyao wakisema: Wewe unayelivunja Jumba la Mungu na kulijenga tena kwa siku tatu,
30
jiokoe mwenyewe, ushuke mtini!
31
Vilevile nao watambikaji wakuu wakamfyoza pamoja na waandishi wakisema wao kwa wao: Wengine aliwaokoa, lakini mwenyewe hawezi kujiokoa.
32
Huyu Kristo, mfalme wa Waisiraeli, ashuke sasa hivi msalabani, tuvione, tupate kumtegemea! Hata wale waliowambwa misalabani pamoja naye wakamtukana.
33
Ilipokuwa saa sita, pakawa na giza katika nchi yote nzima mpaka saa tisa. Ilipokuwa saa tisa, Yesu akapaza sauti sana:
34
Eli, Eli, lama sabaktani? Maana yake ni kwamba: Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?
35
Wengine wao waliosimama hapo walipoyasikia wakasema: Tazama, anamwita Elia!
36
Mmoja akapiga mbio, akachovya mwani sikini, akautia katika utete, akamnywesha akisema: Acheni, tuone, kama Elia anakuja kumshusha!
37
Kisha Yesu akatoa sauti kubwa, nayo pumzi ikamtoka.
38
Ndipo, pazia la Jumbani mwa Mungu lilipopasuka toka juu mpaka chini, likawa vipande viwili.
39
Lakini bwana askari aliyesimama hapo na kumwelekea alipoona, pumzi ilivyomtoka, akasema: Kweli, mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.
40
Palikuwako nao wanawake, walisimama mbali wakitazama. Kati yao walikuwapo Maria Magadalene na Maria, mama yao Yakobo mdogo na Yose, na Salome;
41
ndio waliomfuata na kumtumikia yeye, alipokuwa huko Galilea. Palikuwako nao wengine wengi walipanda pamoja naye kwenda Yerusalemu.
42
Ilipokwisha kuwa jioni, kwa sababu ilikuwa andalio, ndio siku ya kutangulia sikukuu,
43
akaja Yosefu wa Arimatia aliyekuwa mkuu mwenye macheo; naye mwenyewe alikuwa akiungoja ufalme wa Mungu. Akajipa moyo, akaingia kwa Pilato, akataka kupewa mwili wa Yesu.
44
Pilato akastaajabu aliposikia, ya kuwa amekwisha kufa, akamwita bwana askari, akamwuliza, kama amekwisha kufa.
45
Alipotambulishwa na bwana askari akampa Yosefu mwili wake.
46
Naye akanunua sanda, akamshusha msalabani, akamtia katika ile sanda, akamweka katika kaburi lililochongwa mwambani, akafingirisha jiwe mlangoni pa kaburi.
47
Nao akina Maria Magadalene na Maria, mama yake Yose, wakatazama, alipowekwa.
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 16 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16