bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Mark 10
Mark 10
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 11 →
1
Akaondoka huko, akaja mipakani kwa Yudea na ng'ambo ya Yordani. Walipomkusanyikia tena makundi ya watu, akawafundisha tena, kama alivyozoea.
2
Mafariseo wakamjia, wakamwuliza, kama iko ruhusa, mwanamume amwache mkewe.
3
Naye akajibu akiwaambia: Mose aliwaagiza nini?
4
Nao wakasema: Mose alitupa ruhusa kuandika cheti cha kuachana, kisha kumwacha.
5
Yesu akawaambia: Kwa ajili ya ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia agizo hilo.
6
Lakini tokea hapo mwanzo wa viumbe aliwaumba mume na mke.
7
Kwa sababu hii mtu atamwacha baba yake na mama yake,
8
nao hao wawili watakuwa mwili mmoja.
9
Kwa hiyo sio wawili tena, ila wamekuwa mwili mmoja tu. Basi, Mungu alichokiunga, mtu asikiungue!
10
Nyumbani wanafunzi wakamwuliza tena kwa ajili ya neno hilo.
11
Akawaambia: Mtu akimwacha mkewe na kuoa mwingine anazini naye.
12
Naye mke akimwacha mumewe na kuolewa na mwingine anazini.
13
*Wakamletea vitoto, awaguse. Lakini wanafunzi waliwatisha waliowaleta.
14
Yesu alipoviona akachukizwa, akawaambia: Waacheni vitoto, waje kwangu, msiwazuie! Kwani walio hivyo ufalme wa Mungu ni wao.
15
Kweli nawaambiani: Mtu asiyeupokea ufalme wa Mungu kama kitoto hatauingia kamwe.
16
Kisha akawakumbatia, akawabariki akiwabandikia mikono.*
17
*Alipotoka na kufika njiani, mmoja akamjia mbio, akampigia magoti, akamwuliza: Mfunzi mwema, nifanye nini, niurithi uzima wa kale na kale?
18
Yesu akamwambia: Unaniitaje mwema? Hakuna aliye mwema, asipokuwa Mungu peke yake tu.
19
Maagizo unayajua, ya kwamba: Usiue! Usizini! Usiibe! Usisingizie! Usipunje! Mheshimu baba yako na mama yako!
20
Naye akamwambia: Mfunzi, hayo yote nimeyashika, tangu nilipokuwa kijana.
21
Yesu akamtazama, akampenda, akamwambia: Umesaza kimoja: nenda, uviuze vyote, ulivyo navyo, uvigawie maskini! Hivyo utakuwa na kilimbiko mbinguni. Kisha uje, ujitwishe msalaba wako, unifuate!
22
Lakini alipolisikia neno hili alikunjamana uso, akaenda zake na kusikitika, kwani alikuwa mwenye mali nyingi.
23
Kisha Yesu akatazama huko na huko, akawaambia wanafunzi wake: Vitazameni vigumu vinavyowazuia waegemeao mali kuingia katika ufalme wa Mungu!
24
Wanafunzi walipoingiwa na kituko kwa hayo mnaneno yake, Yesu akajibu, akawaambia tena: Wanangu, vitazameni vigumu vinavyozuia kuingia katika ufalme wa Mungu!
25
Masumbuko ya ngamia ya kupenya tunduni mwa sindano ni madogo kuliko yake mwenye mali ya kuuuingia ufalme wa Mungu.
26
Nao wakastuka mno, wakasemezana wao kwa wao: Ikiwa hivyo, yuko nani awezaye kuokoka?
27
Yesu akawachungua, akasema: Kwa watu haliwezekani, lakini kwa Mungu linawezekana, kwani kwa Mungu mambo yote huwezekana.*
28
Petero akaanza kumwambia: Tazama, sisi tumeviacha vyote, tukakufuata wewe.
29
Ndipo, Yesu aliposema: Kweli nawaambiani: Hakuna mtu aliyeacha nyumba au kaka au dada au mama au baba au wana au mashamba kwa ajili yangu na kwa ajili ya Utume mwema,
30
asiporudishiwa na kuongezwa mara mia siku hizi za kuwapo huku nchini nyumba na kaka na dada na mama na wana na mashamba, hata akiwa anafukuzwafukuzwa. Tena siku zile zitakazokuja ataupata nao uzima wa kale na kale.
31
Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, nao walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.
32
Walipokuwa njiani wakipanda kwenda Yerusalemu, Yesu alikuwa anatangulia mbele yao. Nao wakashikwa na kituko, wakamfuata na kuogopa. Akawachukua tena wale kumi na wawili, akaanza kuwaambia mambo yatakayompata,
33
akasema: Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemu. Huko Mwana wa mtu atatiwa mikononi mwao watambikaji wakuu na waandishi, nao watamhukumu, auawe; kwa hiyo watamtia mikononi mwa wamizimu.
34
Ndio watakaomfyoza na kumtemea mate na kumpiga viboko na kumwua. Naye, siku tatu zitakapopita, atafufuka.
35
*Yakobo na Yohana, wana wa Zebedeo, wakamsogelea wakimwambia: Mfunzi, twataka, ufufanyie lo lote, tutakalokuomba.
36
Alipowauliza: Mwataka, niwafanyie nini?
37
wakamwambia: Utuketishe mmoja kuumeni na mmoja kushotoni kwako katika utukufu wako!
38
Yesu akawaambia: Hamjui, mnaloliomba. Mwaweza kukinywa kinyweo, ninachokinywa mimi, au kubatizwa ubatizo, ninaobatizwa mimi?
39
Walipomwambia: Twaweza, Yesu akawaambia: Kinyweo, ninachokinywa mimi, mtakinywa nao ubatizo, ninaobatizwa mimi, mtabatizwa;
40
lakini kumketisha mtu kuumeni au kushotoni kwangu hii si kazi yangu, ila hupewa walioandaliwa.
41
Wenzao kumi walipoyasikia wakaanza kumkasirikia Yakobo na Yohana.
42
Yesu akawaita, wamjongelee, akawaambia: Mnajua: wanaotazamwa kuwa wafalme wa mataifa huwatawala, nao wakubwa wao huwatumikisha kwa nguvu. Kwenu ninyi visiwe hivyo!
43
Ila mtu anayetaka kuwa mkubwa kwenu sharti awe mtumishi wenu!
44
Naye anayetaka kuwa wa kwanza kwenu sharti awe mtumwa wao wote!
45
Kwani naye Mwana wa mtu hakuja, atumikiwe, ila amekuja kutumika na kuitoa roho yake kuwa makombozi ya watu wengi.
46
Wakafika Yeriko. Nao walipotoka Yeriko, yeye na wanafunzi wake na kundi la watu wengi, Bartimeo, mwana wa Timeo, aliyekuwa kipofu alikaa njiani kando akiomba sadaka.
47
Aliposikia, ya kuwa Yesu wa Nasareti yuko, akaanza kupaza sauti na kusema: Yesu, mwana wa Dawidi, nihurumie!
48
Wengi walipomkaripia, anyamaze, yeye akakaza sana kupaza sauti: Mwana wa Dawidi, nihurumie!
49
Ndipo, Yesu aliposimama, akasema: Mwiteni! Wakamwita kipofu, wakamwambia: Tulia moyo, inuka! anakuita.
50
Naye akaitupa kanzu yake, akainuka upesi, akaja kwa Yesu.
51
Yesu alipomwuliza akisema: Wataka, nikufanyie nini? kipofu akamwambia: Mfunzi mkuu, nataka, nipate kuona.
52
Yesu akamwambia: Enenda! Kunitegemea kwako kumekuponya. Mara akapata kuona, akamfuata njiani.
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 11 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16