bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Mark 11
Mark 11
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 12 →
1
Hapo, walipoukaribia Yerusalemu na kufika Beti-Fage na Betania penye mlima wa michekele, akatuma wanafunzi wake wawili,
2
akawaambia: Nendeni katika kijiji kinachowaelekea! Mtakapoingia mle mara mtaona, pamefungwa mwana punda, ambaye mtu hajampanda bado; mfungueni, mmlete!
3
Kama mtu atawauliza: Mbona mnafanya hivi? semeni: Bwana wetu anamtakia kazi! Mara atawapani, mmlete hapa.
4
Walipoondoka kwenda, wakamwona mwana punda aliyefungwa mlangoni nje njiani, wakamfungua.
5
Wengine waliosimama huko wakawauliza: Mnafanya nini mkimfungua mwana punda?
6
Nao wakajibu, kama Yesu alivyowaambia; ndipo, walipowaacha.
7
Wakampeleka mwana punda kwa Yesu, wakatandika nguo zao upesiupesi juu yake, kisha akampanda.
8
Watu wengi wakatandika nguo zao njiani, wengine wakatandika matawi ya miti, waliyoyakata mashambani.
9
Nao waliotangulia nao waliofuata wakapaza sauti: Hosiana!
10
Na atukuzwe ajaye kwa jina la Bwana! Utukuzwe ufalme wa baba yetu Dawidi utujiao! Hosiana juu mbinguni!
11
Alipoingia Yerusalemu, akaenda Patakatifu. Alipokwisha kuvitazama vyote vilivyomo, mchana ukawa umekuchwa; kwa hiyo akatoka kwenda Betania pamoja na wale kumi na wawili.
12
Kesho yake walipotoka Betania akaona njaa.
13
Huko mbali akaona mkuyu wenye majani, akaenda, aone, kama liko tunda juu yake. Akaufikia, asione kitu, ila majani tu, kwani siku za kuyu hazijawa.
14
Ndipo, alipotoa neno la kwamba: Kale na kale mtu asile tena kwako tunda! Wanafunzi wake wakayasikia.
15
Walipofika Yerusalemu, akapaingia Patakatifu, akaanza kuwafukuza wenye kuuzia na kununulia hapo Patakatifu, akaziangusha meza za wavunja fedha na viti vya wachuuzi wa njiwa.
16
Tena hakuacha, mwenye kuchukua chombo apapitie hapo Patakatifu.
17
Akawafundisha akiwaambia: Haikuandikwa ya kuwa: Nyumba yangu itaitwa nyumba ya kuombea kwao makabila yote ya watu? Lakini ninyi mmeigeuza kuwa pango la wanyang'anyi.
18
Watambikaji wakuu na waandishi walipoyasikia, wakatafuta, watakavyomwangamiza, kwani walimwogopa, kwa sababu watu wote pia walishangazwa na mafundisho yake.
19
Lakini kila siku ilipokuwa jioni, wakatoka mjini.
20
Asubuhi walipopita wakauona mkuyu, umekuwa umekauka toka mizizini.
21
Petero akalikumbuka neno lile, akamwambia: Bwana, tazama, mkuyu, uliouapiza, umenyauka.
22
Yesu akawajibu akisema: Mwe wenye kumtegemea Mungu!
23
Kweli nawaambiani: Kila atakayeuambia mlima huu: Ondoka hapa, ulipo, ujitupe baharini! basi, litatimia vivyo hivyo, asipokuwa na mashaka moyoni mwake, ila akiwa anayategemea tu ya kuwa: Analolisema, litatendeka.
24
Kwa hiyo nawaambiani: Yo yote mnayoyaomba kwa kuyataka, yategemeeni tu, ya kuwa mtayapata! ndipo, mtakapoyapata kweli.
25
Nanyi mtakaposimama na kuomba mwondoleane, mkiwa mnamwekea mtu mfundo, Baba yenu alioko mbinguni naye awaondolee ninyi makosa yenu!
26
Lakini ninyi msipoondoleana, naye Baba alioko mbinguni hatawaondolea makosa yenu.
27
Walipoingia tena Yerusalemu, naye alipotembea Patakatifu, wakamjia watambikaji wakuu na waandishi na wazee,
28
wakamwuliza: Hayo unayafanya kwa nguvu gani? au ni nani aliyekupa nguvu hii, uyafanye hayo?
29
Yesu akawaambia: Nanyi nitawauliza neno moja; mtakaponijibu, nitawaelezea nguvu yangu ya kuyafanya hayo.
30
Ubatizo wake Yohana ulitoka mbinguni au kwa watu? Nijibuni!
31
Wakafikiri mioyoni mwao kwamba: Tukisema: Ulitoka mbinguni, atatuuliza: Mbona hamkumtegemea?
32
Lakini tukisema: Ulitoka kwa watu, basi, waliwaogopa watu; kwani watu wote walimshika Yohana kuwa mfumbuaji wa kweli.
33
Kwa hiyo wakamjibu Yesu wakisema: hatujui. Ndipo, Yesu alipowaambia: Basi, hata mimi siwaambii nguvu inayonifanyisha hayo.
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 12 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16