bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Mark 12
Mark 12
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 13 →
1
Akaanza kusema nao kwa mifano. Mtu alipanda mizabibu, akaizungusha ugo, akachimbua kamulio la kuzikamulia zabibu, ajenga dungu, akaipangisha wakulima, kisha akaenda katika nchi nyingine.
2
Siku zilipotimia, akatuma mtumwa kwa wale wakulima, apewe na wakulima matunda ya mizabibu.
3
Nao wakamkamata, wakampiga, wakamrudisha mikono mitupu.
4
Akatuma tena kwao mtumwa mwingine, naye wakampiga na kumtia vidonda vya kichwani na kumtukana.
5
Alipotuma tena mwingine, huyo naye wakamwua. Nao wengine wengi, wengine wakawapiga, wengine wakawaua.
6
Alikuwa na mmoja tena, ndiye mwanawe mpendwa; huyo akamtuma kwao wa mwisho akisema: Watamcha mwanangu.
7
Lakini wale wakulima wakasemezana wao kwa wao: Huyu ndiye kibwana, njoni, tumwue! Kisha nao urithi wake utakuwa wetu!
8
Kwa hiyo wakamkamata, wakamwua, wakamtupa nje ya mizabibu.
9
Basi, mwenye mizabibu atafanya nini? Atakapokuja atawaangamiza wale wakulima, nayo mizabibu atawapa wengine.
10
Hamjalisoma bado andiko hilo la kwamba: Jiwe, walilolikataa waashi, hilihili limekuwa la pembeni?
11
Hivyo vimefanywa na Bwana; nasi tukivitazama, ni vya kustaajabu.
12
Ndipo, walipotafuta kumkamata, lakini waliliogopa kundi la watu. Kwani walitambua, ya kuwa amewasemea wao wenyewe mfano huo. Lakini wakamwacha, wakaenda zao.
13
Wakatuma kwake Mafariseo na watu wa Herode, wamtege kwa maneno yake.
14
Wakaja, wakamwambia: Mfunzi, tumekujua, ya kuwa wewe ni mtu wa kweli, tena humwuliziulizi mtu ye yote, kwani hutazami nyuso za watu, nayo njia ya Mungu unaifundisha, ilivyo kweli.
15
Iko ruhusa ya kumtolea Kaisari kodi au haiko? Tumpe au tusimpe? Kwa kuujua ujanja wao akawaambia: Mwanijaribiaje? Nileteeni shilingi, niitazame!
16
Walipomletea, akawauliza: Chama hiki cha nani? Maandiko nayo ya nani? Wakamwambia: Ni yake Kaisari.
17
Ndipo, Yesu alipowaambia: Yaliyo yake Kaisari mtoleeni Kaisari, naye Mungu yaliyo yake Mungu! Wakamstaajabu sana.
18
Masadukeo wanaosema: Hakuna ufufuko walipokuja kwake wakamwuliza wakisema:
19
Mfunzi, Mose alituandikia kama hivi: Mtu akifiwa na mkubwa wake aliyeacha mkewe, lakini hakuacha mwana, nduguye amchukue huyo mke, amzalie mkubwa wake mwana.
20
Kulikuwa na waume saba walio ndugu. Wa kwanza akaoa mke, lakini alipokufa hakuacha mwana.
21
Wa pili naye akamchukua, akafa, asiache mwana. Naye wa tatu vivi hivi.
22
Nao wote saba hawakuacha mwana. Mwisho wao wote akafa naye mwanamke.
23
Basi, katika ufufuko watakapofufuka, atakuwa mke wa yupi wa hao? Kwani wote saba walikuwa naye yule mwanamke.
24
Yesu akawaambia: Mkipotelewa hivyo, maana hamyajui Maandiko wala nguvu ya Mungu?
25
Kwani watakapofufuka katika wafu hawataoa, wala hawataolewa, ila watakuwa, kama malaika walivyo mbinguni.
26
Lakini kwa ajili ya wafu, kwamba wafufuliwa, hamkusoma katika kitabu cha Mose, Mungu alivyomwambia hapo kichakani: Mimi ni Mungu wa Aburahamu na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo?
27
Basi, Mungu siye wa wafu, ila wao walio hai. Ninyi mnapotelewa sana.
28
Akamjia mwandishi mmoja aliyewasikia, walivyobishana; naye alijua, ya kuwa amewajibu vizuri. Huyo akamwuliza: Katika maagizo yote lililo la kwanza ni lipi?
29
Yesu akajibu: La kwanza ndilo hili: Sikia, Isiraeli! Bwana Mungu wetu ni Bwana peke yake.
30
Nawe umpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa mawazo yako yote na kwa nguvu yako yote!
31
La pili ndilo hili: Umpende mwenzio, kama unavyojipenda mwenyewe! Agizo jingine lililo kubwa kuliko haya haliko.
32
Yule mwandishi akamwambia: Vema, mfunzi, umesema ya kweli: Mungu ni mmoja tu, hakuna mwingine ila yeye.
33
Tena kumpenda yeye kwa moyo wote na kwa mawazo yote na kwa nguvu yote, na kumpenda mwenzio, kama unavyojipenda mwenyewe, hupita ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na vipaji vyote vya tambiko.
34
Yesu alipomwona, ya kuwa amejibu yenye maana, akamwambia: Wewe hu mbali ya ufalme wa Mungu. Kisha hakuwako hata mmoja aliyejipa moyo wa kumwuliza neno tena.
35
Yesu alipofundisha hapo Patakatifu akawauliza akisema: Waandishi husemaje, ya kuwa Kristo ni mwana wa Dawidi?
36
Dawidi mwenyewe alisema kwa nguvu ya Roho Mtakatifu: Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti kuumeni kwangu, mpaka niwaweke adui zako chini miguuni pako!
37
Basi, Dawidi mwenyewe akimwita Bwana, anakuwaje tena mwana wake? Kwa kuwa watu wengi walipendezwa kumsikiliza,
38
akasema na kuwafundisha: Jiangalieni kwa ajili ya waandishi wanaotaka kutembea wenye kanzu ndefu na kuamkiwa na watu sokoni!
39
Namo nyumbani mwa kuombea hupenda viti vya mbele, hata wakialikwa chakulani hupenda kukaa penye wakuu.
40
Huzila nyumba za wajane wakijitendekeza, kama wanakaza kuwaombea. Walio hivyo mapatilizo yao yatakuwa kuliko ya wengine.
41
*Akakaa na kuielekea sanduku ya vipaji, akatazama, watu wanavyotia mapesa katika sanduku ya vipaji. Wenye mali wengi wakatia mengi.
42
Akaja mwanamke mjane mmoja aliyekuwa mkiwa, akatia visenti viwili, pamoja ni hela moja.
43
Ndipo, alipowaita wanafunzi wake, akawaambia: Kweli nawaambiani: Huyu mjane mkiwa ametia mengi kuliko wote waliotia mapesa humu sandukuni mwenye vipaji.
44
Kwani wote walitoa mali katika mali zao nyingi, lakini huyu kwa ukiwa wake amevitoa vyote, alivyokuwa navyo, ndivyo vyote vilivyomlisha.*
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 13 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16