bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Mark 4
Mark 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 5 →
1
Akaanza tena kufundisha kandokando ya bahari. Wakamkusanyikia kundi la watu wengi mno; kwa hiyo akaingia chomboni, akakaa ufukoni, watu wote wakiwa pwani kandokando ya bahari.
2
Akawafundisha maneno mengi kwa mifano, akawaambia katika mafunzo yake:
3
Sikilizeni! Tazameni, mpanzi alitoka kumiaga mbegu.
4
Ikawa, alipozimiaga, nyingine zikaangukia njiani; ndege wakaja, wakazila.
5
Nyingine zikaangukia penye miamba pasipo na udongo mwingi. Kuota zikaota upesi kwa kuwa na udongo kidogo,
6
lakini jua lilipokuwa kali, zikanyauka, kwa kuwa hazina mizizi.
7
Nyingine zikaangukia penye miiba; nayo miiba ilipoota ikazisonga, zisizae.
8
Nyingine zikaangukia penye mchanga mzuri, zikazaa zikikua na nguvu, zikatoa kama punje thelathini, hata sitini, hata mia.
9
Akasema: Mwenye masikio yanayosikia na asikie!
10
Naye alipokuwa peke yake, wafuasi wake pamoja na wale kumi na wawili wakamwuliza maana ya mifano.
11
Akawaambia: Ninyi mmepewa kulitambua fumbo la ufalme wa Mungu, lakini wale walioko nje huambiwa hayo yote kwa mifano,
12
kusudi watazame, lakini wasione, wasikilize, lakini wasijue maana, wasije wakanigeukia, wakaondolewa makosa.
13
Akawaambia: Msipoujua mfano huu mtaitambuaje mifano yote?
14
Mwenye kumiaga analimiaga Neno.
15
Lakini zilizoko njiani ndio hao: Neno linapomiagwa, wakiisha kulisikia, papo hapo Satani huja, akaliondoa Neno lililomiagwa mwao.
16
Vilevile zilizomiagwa penye miamba ndio hao: wanapolisikia Neno, papo hapo hulipokea kwa furaha,
17
lakini hawana mizizi mioyoni mwao, ila wanalishika kwa kitambo kidogo tu. Yanapotukia maumivu au mafukuzo kwa ajili ya Neno, mara hujikwaa.
18
Nyingine ndizo zilizomiagwa penye miiba, ndio hao: wanalisikia Neno,
19
lakini masumbuko ya dunia hii na udanganyifu wa mali na tamaa nyingine zikiwaingia hulisonga Neno, lisizae matunda.
20
Nazo zile zilizomiagwa penye mchanga mzuri ndio hao: wanalisikia Neno na kulipokea, kisha huzaa matunda, kama thelathini, hata sitini, hata mia.
21
Akawauliza: Iko taa inayoletwa, iwekwe chini ya kapu au mvunguni mwa kitanda? Hailetwi, iwekwe juu ya mwango?
22
Kwani hakuna lililofichwa, isipokuwa kwamba lipate kufunuliwa halafu; wala hakuna njama, ila kwamba ipate kutokea waziwazi.
23
Mtu akiwa na masikio yanayosikia na asikie!
24
Akawaambia: Mwangalie, jinsi mnavyosikia! Kipimo, mnachokipimia wengine, ndicho, mtakachopimiwa nanyi, tena mtaongezewa.
25
Kwani aliye na mali atapewa; lakini asiye na kitu atachukuliwa hata kile, alicho nacho.
26
*Akasema: Ufalme wa Mungu unakuwa hivyo, kama mtu anayemiaga mbegu katika nchi.
27
Kisha hulala na kuamka usiku na mchana, nazo mbegu humea na kukua, yeye asivijue, vilivyo.
28
Nchi huzaa yenyewe kwanza hutoa mimea, halafu suke, halafu ngano zinazojaa katika suke.
29
Lakini punje zinapopevuka, mwenyewe mara hutuma wenye miundu, kwani mavuno yamefika.*
30
Akasema: Ufalme wa Mungu tuufananishe na nini? Au tuueleze kwa mfano gani?
31
Umefanana na kipunje cha haradali. Kinapopandwa katika nchi ni kidogo kuliko mbegu zote zilizoko huku nchini.
32
Tena kikiisha pandwa hukua, kiwe mkubwa kuliko miboga yote kwa kuchipuza matawi makubwa, hata ndege wa angani huweza kuja na kutua katika kivuli chake.
33
Kwa mifano mingi inayofanana na huu akawaambia Neno, kama walivyoweza kusikia; lakini pasipo mfano hakuwaambia neno.
34
Lakini wanafunzi wake akawafungulia yote, walipokuwa peke yao.
35
Siku ile ilipokuwa jioni, akawaambia: Tuvuke kwenda ng'ambo!
36
Wakaliacha kundi la watu, wakamchukua hivyo alivyokuwa chomboni; navyo vyombo vingine vilikuwa pamoja naye.
37
Kukawa na msukosuko mkubwa wa upepo, mawimbi yakakipigapiga chombo, hata chombo kikawa kinajaa maji.
38
Naye alikuwa chomboni upande wa nyuma, amelala usingizi juu ya mto. Ndipo, walipomwamsha wakimwambia: Mfunzi, huoni uchungu, tukiangamia?
39
Akainuka, akaukaripia upepo, akaiambia bahari: Nyamaza, utulie! Papo haupepo ukakoma, kukawa kimya kabisa.
40
Kisha akawaambia: Mbona mnaogopa hivyo? Mbona hamnitegemei?
41
Wakaingiwa na woga mkubwa, wakasemezana wao kwa wao: Ni mtu gani huyu, ya kuwa hata upepo na bahari zinamtii?
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16