bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Mark 9
Mark 9
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 10 →
1
Akawaambia: Kweli nawaambiani: Miongoni mwao wanaosimama hapa wamo wengine, ambao hawatakuonja kufa, mpaka watakapouona ufalme wa Mungu, ukiisha kuja kwa nguvu.
2
Baada ya siku sita Yesu akamchukua Petero na Yakobo na Yohana, akapanda pamoja nao peke yao pasipo watu wengine juu ya mlima mrefu. Huko akageuzwa sura yake machoni pao,
3
nazo nguo zake zikawa nyeupe sana, zikamerimeta; nchini hakuna fundi anayeweza kuzing'aza hivyo.
4
Wakatokewa na Elia pamoja na Mose, wakawa wakiongea na Yesu.
5
Petero akasema akimwambia Yesu: Mfunzi mkuu, hapa ni pazuri kuwapo sisi, na tujenge vibanda vitatu, kimoja chako, na kimoja cha Mose, na kimoja cha Elia!
6
Kwani hakujua, alilolisema, kwa maana waliingiwa na woga mkubwa.
7
Kisha hapo pakawa na wingu, likawatia kivuli, sauti ikatoka winguni kwamba: Huyu ndiye mwanangu mpendwa, msikilizeni yeye!
8
Mara walipotazama huko na huko, hakuna waliyemwona, asipokuwa Yesu peke yake pamoja nao.
9
Walipokuwa wakishuka mlimani, akawakataza, wasimsimulie mtu ye yote, waliyoyaona, isipokuwa hapo, Mwana wa mtu atakapokwisha kufufuka katika wafu.
10
Wakalishika neno hili wakiulizana wao kwa wao: Huko kufufuka katika wafu maana yake nini?
11
Wakamwuliza wakisema: Waandishi husemaje: Sharti kwanza Elia aje?
12
Akawaambia: Kweli, Elia anakuja kwanza, vyote avigeuze kuwa vipya. Kisha Mwana wa mtu ameandikiwaje, ya kuwa atateswa mengi na kubezwa?
13
Lakini nawaambiani: Elia amekwisha kuja, wakamtendea yote, waliyoyataka, kama alivyoandikiwa.
14
Walipokuja kwa wanafunzi wakaona kundi la watu wengi lililowazunguka, hata waandishi walikuwapo wakibishana nao.
15
Papo hapo kundi lote lilipomwona yeye, wakastuka, wakamwendea mbio, wakamwamkia.
16
Akawauliza: Mnabishana nini nao?
17
Mmoja wao wale watu wengi akamjibu: Mfunzi, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo wa ububu.
18
Napo pote anapomkamata anamsukumasukuma kwa nguvu, naye hutoka pofu na kukereza meno, kisha mwili wake hunyauka. Nami nikawaambia wanafunzi wako, wamfukuze huyo pepo, lakini hawakuweza.
19
Naye akawajibu akisema: Enyi wa kizazi kisichomtegemea Mungu! Nitakuwapo nanyi mpaka lini? Nitawavumilia mpaka lini? Mleteni hapa, nilipo!
20
Wakampeleka kwake; naye alipomwona, mara pepo akamkumba, akaanguka chini, akafingirika na kutoka pofu.
21
Akamwuliza baba yake: Hivyo vimempata tangu lini? Akasema: Tangu utoto wake;
22
mara nyingi humtupa motoni na majini, maana amwue. Lakini ukiweza kitu tusaidie ukituonea uchungu!
23
Yesu akamwambia: Ukiweza kumtegemea Mungu! Yote huwezekana kwake anayemtegemea Mungu.
24
Papo hapo baba wa kijana akapaza sauti akisema: Namtegemea Mungu; nisaidie, nisipomtegemea!
25
Yesu alipoona, watu wengi wanavyomkusanyikia mbiombio, akamkaripia yule pepo mchafu akimwambia: Wee pepo uliye bubu na kiziwi, mimi nakuagiza, umtoke huyu, usimwingie tena!
26
Ndipo, alipolia, akamsukumasukuma kwa nguvu, akamtoka; naye akawa kama mfu, hata wengi wakasema: Amekufa.
27
Lakini Yesu akamshika mkono, akamwinua; ndipo, aliposimama.
28
Naye alipoingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza walipokuwa peke yao: Mbona sisi hatukuweza kumfukuza huyo?
29
Akawaambia: Pepo walio hivyo hawawezi kutoka, isipokuwa kwa nguvu ya kuomba na ya kufunga.
30
Wakatoka kule, wakatembea huko katikati ya Galilea; naye hakutaka, mtu akivitambua.
31
Kwani alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake na kuwaambia: Mwana wa mtu atatiwa mikononi mwa watu, nao watamwua; lakini akiisha kuuawa, siku zitakapopita tatu, atafufuka.
32
Nao hawakulitambua neno hili, lakini wakaogopa kumwuliza.
33
Wakafika Kapernaumu. Alipokuwa nyumbani akawauliza: Njiani mlibishana nini?
34
Wakanyamaza; maana walikuwa wameshindana njiani wao kwa wao kwamba: Aliye mkuu ni nani?
35
Akakaa, akawaita wale kumi na wawili, akawaambia: Mtu akitaka kuwa wa kwanza, sharti awafuate wenzake wote nyuma, awe mtumishi wao wote!
36
Kisha akatwaa kitoto, akamsimamisha katikati yao, akamkumbatia, akawaambia:
37
Mtu atakayepokea kitoto mmoja aliye kama huyu kwa Jina languhunipokea mimi. Tena mtu akinipokea mimi hanipokei mimi, ila humpokea yule aliyenituma.
38
Yohana akamwambia: Mfunzi, tuliona mtu anayefukuza pepo kwa Jina lako, lakini hafuatani nasi; tukamzuia, kwani hakufuatana nasi.
39
Yesu akasema: Msimzuie! Kwani hakuna mwenye kufanya cha nguvu kwa ajina langua atakayeweza kipunde kidogo kunisema vibaya.
40
Kwani asiyetukataa yuko upande wetu.
41
Kwani atakayewanywesha ninyi kinyweo cha maji tu, kwa sababu m wa Kristo, kweli nawaambiani Mshahara wake hautampotea kamwe.
42
Lakini mtu atakayekwaza mmoja tu aliye mwenzao hawa wadogo wanaonitegemea, itamwia vizuri zaidi, akitundikwa shingoni pake jiwe kubwa la kusagia, kisha atumbukizwe baharini.
43
Nawe, mkono wako ukikukwaza, uukate! Kuingia penye uzima mwenye kilema kutakufaa kuliko hapo, ukiwa mwenye mikono miwili, ukajiendea kuzimuni penye moto usiozimika.
44
Hapo ndipo, mdudu mwenye kuwaumiza asipokufa, tena ndipo, pasipozimika moto.
45
Nawe, mguu wako ukikukwaza, uukate! Kuingia penye uzima, ukiwa kiwete, kutakufaa kuliko hapo, ukiwa mwenye miguu miwili, ukatupwa shimoni mwa moto.
46
Hapo ndipo, mdudu mwenye kuwaumiza asipokufa, tena ndipo pasipozimika moto.
47
Nalo jicho lako likikukwaza, basi, ling'oe, ulitupe mbali! Kuuingia ufalme wa Mungu mwenye chongo kutakufaa kuliko hapo, ukiwa mwenye macho mawili ukatupwa shimoni mwa moto.
48
Hapo ndipo, mdudu mwenye kuwaumiza asipokufa, tena ndipo, pasipozimika moto.
49
Kwani chumvi ya kumkoleza mtu ye yote ni moto.
50
Chumvi ni nzuri; lakini chumvi ikiwa imepotewa na ukolezi, mtaitia kitu gani, ipate kukolea tena? Mwe na chumvi mioyoni mwenu! Tena mwendeane kwa utengemano!
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 10 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16