bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Mark 13
Mark 13
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 14 →
1
Alipotoka Patakatifu, mwanafunzi wake mmoja akamwambia: Mfunzi, yatazame mawe hayo makubwa na majengo hayo makubwa!
2
Yesu akamwambia: Je? Wayatazama majengo haya makubwa? Halitaachwa hata jiwe moja juu ya jiwe lenziwe lisiloporomoshwa chini.
3
Kisha alipokaa mlimani pa michekele kupaelekea Patakatifu, ndipo, Petero na Yakobo na Yohana na Anderea walipomwuliza walipokuwa peke yao wakisema:
4
Tuambie, hayo yatakuwapo lini? Tena kielekezo ni nini, hayo yote yatakapotimia?
5
Yesu akaanza kuwaambia: Angalieni, mtu asiwapoteze!
6
Wengi watakuja kwa jina langu na kusema: Mimi ndiye,
7
nao watapoteza wengi. Nanyi mtakaposikia vita na mavumi ya vita msivihangaikie! Hivyo sharti viwepo, lakini huo sio mwisho.
8
Kwani watainukiana taifa na taifa, tena wafalme na wenzao wafalme. Mahali penginepengine patakuwa na matetemeko, pengine na njaa. Hayo ni mwanzo tu wa uchungu.
9
Lakini ninyi jiangalieni wenyewe! Watawapeleka barazani kwao wakuu namo nyumbani mwa kuombea, mpigwe, kisha mtasimamishwa kwa ajili yangu mbele ya mabwana wakubwa na mbele ya wafalme, mje mnishuhudie kwao.
10
Nao Utume mwema sharti utangazwe kwanza kwa mataifa yote.
11
Napo hapo, watakapowatoa na kuwapeleka, msianze kuyahangaikia maneno ya kusema, ila maneno mtakayopewa saa ile yasemeni yaleyale! Kwani si ninyi mnaosema, ila ni Roho Mtakatifu.
12
Itakuwa hivi: ndugu na ndugu watatoana, wauawe, hata baba watawatoa watoto wao, hata watoto watawainukia wazazi wao, wawaue.
13
Nanyi mtakuwa mmechukiwa na watu wote kwa ajili ya Jina langu. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokoka.
14
Hapo ndipo, mtakapochafukwa mioyo mkiona, mwangamizaji atapishaye akisimama mahali pasipompasa; mwenye kupasoma hapa sharti aangalie, ajue maana! Siku zile watakaokuwako Yudea na wakimbilie milimani!
15
Mtu atakayekuwapo nyumbani juu asishuke na kuingia nyumbani mwake kuchukua kilichomo!
16
Naye atakayekuwako shambani asiyarudie yaliyoko nyuma, aichukue nguo yake!
17
Lakini watakaoona vibaya zaidi ndio wenye mimba na wenye kunyonyesha siku zile.
18
Lakini ombeni, hayo yasitimie siku za kipupwe!
19
Kwani siku zile zitakuwa na maumivu makuu kuyapita yote yaliyopatikana tangu mwanzo wa viumbe, Mungu alivyoviumba, mpaka sasa, hata halafu hayatapatikana tena kama hayo.
20
Nazo siku zile kama Bwana hangalizipunguza, hangaliokoka mtu hata mmoja. Lakini kwa ajili ya wale, waliochaguliwa, aliowachagua, amezipunguza siku zile.
21
Hapo mtu akiwaambia: Tazama, huyu hapa ni Kristo! au: Tazama, yule kule! msiitikie!
22
Watainuka makristo wa uwongo na wafumbuaji wa uwongo; nao watafanya vielekezo na vioja, wawapoteze waliochaguliwa, kama inawezekana.
23
Lakini ninyi angalieni! Nimetangulia kuwaambia yote.
24
Lakini siku zile, yale maumivu yatakapopita, jua litakuwa jeusi lenye giza, nao mwezi hautaumulikisha mwanga wake.
25
Nazo nyota zitakuwa zinaanguka toka mbinguni, nazo nguvu za mbingu zitatukutishwa.
26
Hapo ndipo, watakapomwona Mwana wa mtu, anavyokuja katika mawingu mwenye nguvu na utukufu mwingi.
27
Ndipo, atakapowatuma malaika, awakusanye waliochaguliwa naye toka pande zote nne, upepo unapotokea, aanzie mwanzoni kwa nchi, aufikishe mwisho wa mbingu.
28
Jifundisheni mfano kwa mkuyu: matawi yake yanapochipua na kuchanua majani, mnatambua, ya kuwa siku za vuli ziko karibu.
29
Vivyo hivyo nanyi mtakapoyaona hayo, yakiwapo, tambueni, ya kuwa mwisho umewafikia milangoni!
30
Kweli nawaambiani: Kizazi hiki hakitakoma mpaka hapo, yatakapokuwapo hayo yote.
31
Mbingu na nchi zitakoma, lakini maneno yangu hayatakoma.
32
Lakini ile siku au saa yake itakapofikia, mtu hapajui, wala malaika wa mbinguni, wala Mwana, ila Baba tu.
33
Angalieni! Kesheni! Kwani hamjui, siku zake zitakapokuwapo. Vinafanana na mtu mwenye kufunga safari aliyeiacha nyumba yake, akawapa watumishi wake nguvu akimgawia kila mtu kazi yake, naye mlinda mlango akamwagiza, akeshe.
34
Basi, hivyo kesheni! Kwani hamjui, mwenye nyumba atakaporudia, kama atakuja jioni au kati ya usiku au jogoo awikapo au mapema.
35
Asije na kuwastusha akiwakuta, mmelala.
36
Hilo, ninalowaambia ninyi, nawaambia wote: Kesheni!
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 14 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16