bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Mark 2
Mark 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 3 →
1
Siku zilipopita, akaingia tena Kapernaumu. Watu waliposikia, ya kuwa yumo nyumbani,
2
wakakusanyika wengi, wasienee mle nyumbani, wala mlangoni, akawaambia lile Neno.
3
Kukaja watu waliomletea mgonjwa wa kupooza, akichukuliwa na watu wanne;
4
wasipoweza kumpelekea yeye kwa ajili ya watu wengi wakafumua paa hapo, alipokuwapo. Walipokwisha kupatoboa wakakishusha kitanda, alichokilalia yule mgonjwa wa kupooza.
5
Yesu alipoona, walivyomtegemea, akamwambia mwenye kupooza: Mwanangu, makosa yako yameondolewa.
6
Mlikuwamo na waandishi waliokaa mlemle, wakawaza mioyoni mwao ya kwamba: Haya huyu anayasemaje? Anambeza Mungu
7
Yuko nani awezaye kuondoa makosa? Siye Mungu peke yake?
8
Kwa kutambua rohoni mwake, ya kuwa wanawaza hivyo mioyoni mwao, Yesu akawaambia: Mbona mnawaza hivyo mioyoni mwenu?
9
Kilicho chepesi ni kipi? Kumwambia mwenye kupooza: Makosa yako yameondolewa! au kusema: Inuka, ukichukue kitanda chako, uende?
10
Lakini kusudi mpate kujua, ya kuwa Mwana wa mtu ana nguvu ya kuondoa makosa nchini, akamwambia mwenye kupooza:
11
Nakuambia: Inuka, jitwishe kitanda chako, uende nyumbani kwako!
12
Ndipo, alipoinuka, akajitwisha papo hapo kitanda, akatoka machoni pao wote. Kwa hiyo wote wakashangaa, wakamtukuza Mungu wakisema: Yaliyo kama hayo hatujayaona kamwe.
13
Alipotoka tena kwenda kandokando ya bahari, kundi lote la watu likamjia, akawafundisha.
14
Kisha alipokuwa akitembea akamwona Lawi, mwana wa Alfeo, amekaa forodhani. Akamwambia: Nifuata! Akainuka, akamfuata.
15
Ikawa, alipokaa chakulani nyumbani mwake, ndipo, watoza kodi na wakosaji wengi walipokaa chakulani pamoja na Yesu na wanafunzi wake; kwani walikuwa wengi walipokaa chakulani pamoja na Yesu na wanafunzi wake; kwani walikuwa wengi waliomfuata.
16
Waandishi wa Kifariseo walipomwona, ya kuwa anakula pamoja na wakosaji na watoza kodi, wakawaambia wanafunzi wake; Kumbe anakula pamoja na watoza kodi na wakosaji!
17
Yesu alipoyasikia akawaambia: Walio wazima hawapaswi na mganga, ila walio wagonjwa. Sikujia kuwaita waongofu, ila wakosaji.
18
Wanafunzi wa Yohana na Mafariseo walikuwa wakifunga. Wakaja, wakamwambia: Kwa nini wanafunzi wa Yohana na wanafunzi wa Mafariseo hufunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?
19
Yesu akawaambia: Walioalikwa arusini hawawezi kufunga, bwana arusi akingali pamoja nao. Siku zote, wanapokuwa na bwana arusi, hawawezi kufunga.
20
Lakini siku zitakuja, watakapoondolewa bwana arusi; siku ile ndipo, watakapofunga.
21
Hakuna mtu anayetia kiraka cha nguo mpya katika kanzu chakavu; kama anafanya hivyo, kile kiraka kipya kinaondoa pote paliposhonwa katika kanzu chakavu; hivyo tundu lake litakuwa kubwa zaidi.
22
Wala hakuna mtu anayetia mvinyo mpya katika viriba vichakavu; kwani akiitia mle, mvinyo itavipasua viriba, nayo mvinyo itaangamia pamoja na viriba. Ila mvinyo mpya hutiwa katika viriba vipya.
23
Akawa akipita katika mashamba siku ya mapumziko; nao wanafunzi wake wakaanza kuendelea njiani wakikonyoa masuke.
24
Lakini Mafariseo wakamwambia: Tazama! Mbona wanafanya siku ya mapumziko yaliyo mwiko?
25
Naye akawaambia: Hamjasoma bado, Dawidi alivyofanya alipokosa chakula, wakaona njaa yeye na wenziwe?
26
Hapo aliingia Nyumbani mwa Mungu kwa mtambikaji mkuu Abiatari, akaila mikate aliyowekewa Bwana, nayo kuila ni mwiko, huliwa na watambikaji tu; kisha akawapa nao wenziwe waliokuwa naye.
27
Akawaambia: Siku ya mapumziko iliwekwa kwa ajili ya mtu; lakini mtu hakuwekwa kwa ajili ya siku ya mapumziko.
28
Kwa hiyo Mwana wa mtu ni bwana hata wa siku ya mapumziko.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16