bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Mark 16
Mark 16
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
1
*Siku ya mapumziko ilipokwisha pita, ndipo, Maria Magadalene na Maria, mama yake Yakobo, na Salome waliponunua manukato, wapate kwenda kumpaka.
2
Siku ya kwanza ya juma asubuhi na mapema wakajidamka, wakaenda kaburini, jua lilipochomoza.
3
Wakasema wao kwa wao: Nani atatufingirishia lile jiwe, litoke mlangoni pa kaburi?
4
Walipotazama wakaona, jiwe limekwisha fingirishwa; kwani lilikuwa kubwa mno.
5
Walipoingia kaburini wakaona kijana, amekaa kuumeni, amejitanda nguo nyeupe, wakaingiwa na kituko.
6
Naye akawaambia: Msistuke! Mnamtafuta Yesu wa Nasareti aliyewambwa msalabani, amefufuliwa, hayumo humu. Patazameni mahali, walipomweka!
7
Lakini nendeni, mwaambie wanafunzi wake na Petero, ya kuwa anawatangulia ninyi kwenda Galilea! Huko ndiko, mtakakomwona, kama alivyowaambia.
8
Wakatoka kaburini, wakakimbia, kwani walikuwa wameshikwa na utetemeko na ushangao. Kisha hawakumwambia mtu neno, kwani waliogopa.*
9
Alipokwisha fufuka asubuhi na mapema siku ya kwanza ya juma, akamtokea kwanza Maria Magadalene, aliyemfukuzia pepo saba.
10
Ndipo, alipokwenda, akawasimulia wale waliokuwa pamoja naye, walipoomboleza na kulia.
11
Nao waliposikia, ya kuwa anaishi, ya kuwa yeye amemwona, hawakuitikia.
12
Kisha akawatokea wenzao wawili kwa sura nyingine, wakitembea kwenda shambani.
13
Nao wakaenda, wakavisimulia wenzi wao wengine, lakini nao hawakuwaitikia.
14
*Mwisho akawatokea wale kumi na mmoja, walipokaa wakila. Akawakaripia, kwa sababu walikuwa wameshindwa na kumtegemea, na kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao, kwani hawakuwaitikia wale waliomwona, ya kuwa amefufuka.
15
Akawaagiza: Nendeni katika nchi zote za ulimwenguni, mwatangazie wote walioumbwa Utume mwema!
16
Anayemtegemea Mungu akibatizwa ataokoka, lakini asiyemtegemea atahukumiwa.
17
Nao wamtegemeao vielekezo vitakavyowafuata ni hivi: kwa Jina langu watafukuza pepo, watasema kwa ndimi mpya,
18
watashika nyoka, hata wakinywa machawi, hayatawaua kabisa; watakapobandikia wagonjwa mikono, ndipo, watakapoponapona.
19
Bwana Yesu alipokwisha kusema nao akachukuliwa na kupazwa mbinguni, akaketi kuumeni kwa Mungu.
20
Kisha wale wakatoka, wakapiga mbiu mahali po pote. Naye Bwana alifanya kazi pamoja nao akilitia Neno lake nguvu na kutenda vielekezo vilivyowafuata.*
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16