bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Leviticus 1
Leviticus 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 2 →
1
Bwana akamwita Mose, akasema naye toka Hemani mwa Mkutano kwamba:
2
Waambie wana wa Isiraeli na kuwaagiza hivyo: Mtu wa kwenu akitaka kumpelekea Bwana matoleo ya nyama wa kufuga sharti hayo matoleo yenu myatoe katika ng'ombe au katika mbuzi na kondoo.
3
Kama toleo lake ni ng'ombe, anayemtoa kuwa ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima, sharti atoe dume asiye na kilema, ampeleke pa kuliingilia Hema la Mkutano, Bwana apate kupendezwa naye.
4
Kisha aubandike mkono wake kichwani pake hiyo ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima, impatie upendezo wa kupozwa kwake.
5
Kisha amchinje huyo mwana wa ng'ombe mbele ya Bwana, nao wana wa Haroni walio watambikaji na waipeleke damu, nayo hiyo damu wainyunyize pande zote juu ya meza ya kutambikia iliyopo hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano.
6
Kisha aichune hiyo ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima na kuichangua.
7
Kisha wana wa Haroni walio watambikaji watie moto hapo pa kutambikia na kupanga kuni juu ya moto.
8
Kisha wana wa Haroni walio watambikaji na wavipange vile vipande vya nyama, hata kichwa na mafuta juu ya kuni zilizopangwa juu ya moto uliowashwa mezani pa kutambikia.
9
Lakini matumbo na miguu yake na aioshe kwa maji, kisha mtambikaji atayachoma moto yote yaliyowekwa juu ya meza ya kutambikia. Ndivyo, ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima inavyotolewa, iwe moto wenye mnuko wa kumpendeza Bwana.
10
Kama toleo lake, analolitoa kuwa ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima, ni nyama mdogo kama kondoo au mbuzi sharti apeleke dume asiye na kilema.
11
Amchinje mbele ya Bwana kando ya meza ya kutambikia upande wake wa kaskazini, nayo damu yake wana wa Haroni walio watambikaji na wainyunyize pande zote juu ya meza ya kutambikia.
12
Kisha amchangue, naye mtambikaji avipange vipande vyake pamoja na kichwa chake na mafuta yake juu ya moto uliowashwa mezani pa kutambikia.
13
Lakini matumbo na miguu na aioshe kwa maji, kisha mtambikaji atayatoa yote kwa kuyachoma moto yote yaliyowekwa juu ya meza ya kutambikia. Ndivyo, naye nyama mdogo anavyokuwa ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima, ndio moto wenye mnuko wa kumpendeza Bwana.
14
Kama toleo lake, analomtolea Bwana kuwa ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima, ni ndege, basi, sharti apeleke hua au kinda la njiwa manga.
15
Naye mtambikaji atampeleka mezani pa kutambikia, atamvunja kichwa chake, apate kumchoma moto mezani pa kutambikia, lakini damu yake sharti idondoke ukutani pake meza ya kutambikia.
16
Kisha akiondoe kibofu chake cha koo pamoja na machafu yaliyomo, akitupe majivuni kando ya meza ya kutambikia upande wa maawioni kwa jua.
17
Kisha ampasue kidogo mabawani, lakini asiyatenge! Kisha mtambikaji amchome moto mezani pa kutambikia juu ya kuni zilizowekwa juu ya moto. Ndivyo, naye ndege anavyokuwa ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima, ndio moto wenye mnuko wa kumpendeza Bwana.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27