bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Leviticus 2
Leviticus 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 3 →
1
Mtu akimpelekea Bwana toleo la vilaji vya tambiko sharti hilo toleo lake liwe unga mwembamba sana, alioumiminia mafuta na kuweka uvumba juu yake.
2
Kisha aupeleke kwa wana wa Haroni walio watambikaji; ndipo, mtambikaji atakapochukua katika huo unga mwembamba wa kulijaza gao lake pamoja na mafuta, lakini uvumba atauchukua wote, kisha atauvukiza mezani pa kutambikia, uwe wa kumkumbushia Bwna, maana ndio moto wenye mnuko wa kumpendeza Bwana.
3
Lakini masao ya vilaji vya tambiko ni yao Haroni na wanawe, ndiyo matakatifu yenyewe yatokayo kwenye mioto ya Bwana.
4
Lakini ukipeleka toleo la vilaji vya tambiko vilivyookwa jikoni, liwe la vikate vilivyotengenezwa pasipo chachu kwa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta au la maandazi yasiyochachwa yaliyopakwa mafuta.
5
Lakini kama toleo lako ni vilaji vya tambiko vilivyokaangwa, liwe la maandazi yaliyotengenezwa pasipo chachu kwa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta;
6
nawe uyakatekate vipande, kisha uvimiminie mafuta; ndivyo, vitakavyokuwa vilaji vya tambiko.
7
Lakini kama toleo lako ni vilaji vya tambiko vilivyookwa katika chungu, na vitengenezwe kwa unga mwembamba na kutiwa mafuta.
8
Ukitaka kumtolea Bwana vilaji vya tambiko vilivyotengenezwa hivyo, uvipeleke kwa mtambikaji, naye ataviweka mezani pa kutambikia.
9
Kisha humo katika hivyo vilaji mtambikaji atanyanyua vingine, viwe vya kumkumbushia Bwana, atavivukiza mezani pa kumtambikia; ndio moto wenye mnuko wa kumpendeza Bwana.
10
Navyo vilaji vya tambiko vitakavyosalia vitakuwa vyao Haroni na wanawe, ndivyo vitakatifu vyenyewe, vitokavyo kwenye mioto ya Bwana.
11
Vilaji vyote vya tambiko, mtakavyomtolea Bwana, visitengenezwe na kuchachwa. Kwani yote yaliyo yenye chachu au asali msiyavukize kuwa moto wa Bwana.
12
Yakiwa ni matoleo ya malimbuko, basi, nayo mtamtolea Bwana, lakini penye meza ya kutambikia yasifike juu yake kuwa mnuko wa kumpendeza.
13
Vilaji vyote vya tambiko, utakavyovitoa, uvitie chumvi, usiache kabisa, vilaji vyako vya tambiko vikose chumvi ya agano la Mungu wako, ila vilaji vyako vyote vya tambiko uvitoe, vikiwa vyenye chumvi.
14
Lakini ukimtolea Bwana vilaji vya tambiko vya malimbuko, yawe masuke yaliyochomwa moto au chenga za ngano mpya, basi, hayo utayatoa kuwa vilaji vya tambiko vya malimbuko.
15
Utayatia hata mafuta, kisha utaweka uvumba juu yao; ndivyo, yatakavyokuwa vilaji vya tambiko.
16
Humo katika hizo chenga na yale mafuta mtambikaji atachukua mengine pamoja na uvumba wote, ayavukize yote, yawe ya kumkumbushia Bwana, maana ndio moto wa Bwana.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27