bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Leviticus 19
Leviticus 19
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 20 →
1
Bwana akamwambia Mose kwamba:
2
Sema na mkutano wote wa wana wa Isiraeli, uwaambie: Sharti mwe watakatifu, kwani mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu.
3
Mtu sharti amche mama yake na baba yake. Nazo siku zangu za mapumziko sharti mziangalie. Mimi Bwana ni Mungu wenu.
4
Msivigeukie vinyago vilivyo vya bure, wala msijitengenezee miungu ya shaba au ya vinginevyo vilivyoyeyushwa. Mimi Bwana ni Mungu wenu.
5
Mtakapomtolea Bwana ng'ombe ya tambiko ya shukrani, sharti mwitoe hivyo, atakavyopendezwa nanyi.
6
Siku ya kuitoa na iliwe, hata kesho yake; lakini nyama zitakazosalia mpaka siku ya tatu na ziteketezwe kwa moto.
7
Lakini ikiliwa siku ya tatu, itachukiza, haitapendeza.
8
Naye atakayeila atakuwa amekora manza, kwa kuwa ameichafua iliyo takatifu ya Bwana, kwa hiyo yeye mwenyewe atang'olewa kwao walio ukoo wake.
9
Mtakapovuna mavuno ya nchi yenu, msikate napo pembeni penye mashamba yenu kupavunia napo, wala msiokoteze viokotezo vya mavuno yenu.
10
Wala usiipukuse mizabibu yako, wala zabibu zako zilizoanguka usiziokoteze, ila uziache, ziokotezwe na wakiwa na wageni. Mimi Bwana ni Mungu wenu.
11
Msiibe, wala msidanganywe, wala msiongopeane wenyewe na wenyewe.
12
Msiape kiapo cha uwongo na kulitaja Jina langu. Maana hivyo utalichafua Jina la Mungu wako. Mimi ni Bwana.
13
Usimkorofishe mwenzio na kumnyang'anya. Mshahara wa kazi, uliyofanyiziwa, usilale nao, mpaka kuche.
14
Usiapize kiziwi, wala usiweke makwazo, kipofu anapopitia, ila umwogope Mungu wako! Mimi ni Bwana.
15
Msifanye mapotovu mashaurini mkiupendelea uso wa mkiwa au mkimtukuza mkuu, ila umwamulie mwenzako kwa wongofu.
16
usitembee kwa wenzako wa ukoo, upate mtu wa kumchongea. Usitoe ushahidi wa uwongo wa kumwua mwenzako. Mimi ni Bwana.
17
Usimchukie ndugu yako moyoni mwako. Kuonya umwonye mwenzako, kusudi usijikoseshe kwa ajili yake.
18
Usijilipize mwenyewe, wala usiwakasirikie wana wa ukoo wako, ila umpende mwenzio, kama unavyojipenda mwwenyewe. Mimi ni Bwana.
19
Yaangalieni maongozi yangu! Usiwaache nyama wako wa kufuga, walale pamoja na nyama wengine, wala shamba lako usilipande mbegu za namna mbili, wala mwilini mwako usivae nguo iliyofumwa kwa nyuzi za namna mbili.
20
Mtu akilala kwa mwanamke kijakazi na kumpa mimba, naye alikuwa ameposwa na mtu mwingine, basi, akiwa hakukombolewa wala hakufunguliwa kujiendea, na wapatilizwe, lakini wasiuawe, kwa kuwa yule mwanamke hakufunguliwa kujiendea.
21
Naye mume sharti apeleke dume la kondoo hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano kuwa ng'ombe ya tambiko ya upozi ya kumtolea Bwana kwa ajili ya manza, alizozikora.
22
Naye mtambikaji na ampatie upozi na kumtoa yule dume la kondoo kuwa ng'ombe ya tambiko ya upozi mbele ya Bwana kwa ajili ya kosa lake, alilolikosa; ndipo, atakapoondolewa hilo kosa lake, alilolikosa.
23
Mtakapoingia katika nchi ile mtapanda miti yo yote yenye matunda ya kula, lakini kwanza iacheni yenye magovi yao, ndio matunda yao, miaka mitatu mwiwazie kuwa haijatahiriwa, isiliwe.
24
Katika mwaka wa nne matunda yao yote pia yawe matakatifu ya kumtolea Bwana shukrani.
25
Katika mwaka wa tano mtaweza kuyala matunda yao; ndivyo, mtakavyojiongezea mapato yao. Mimi Bwana ni Mungu wenu.
26
Msile cho chote kilicho chenye damu bado. Msipige bao, wala msiagulie mawingu.
27
Msichege nywele pembeni vichwani penu, wala ndevu zenu msizikate pembenipembeni.
28
Msijichanje chale miilini mwenu kwa ajili ya wafu, wala msijiandike nembo miilini mwenu. Mimi ni Bwana.
29
Mwanao wa kike usimtie uchafu na kumzinisha, hiyo nchi isipate kuwa yenye uzinzi, hiyo nchi ikijaa ugoni.
30
siku zangu za mapumziko sharti mziangalie, napo Patakatifu pangu sharti mpache. Mimi ni Bwana.
31
Msiwageukie waganga wa kutiisha mizimu wa waaguaji. Msiwatafute, mkajipatia uchafu kwao. Mimi Bwana ni Mungu wenu.
32
Mbele yake mwenye mvi sharti uinuke, naye aliye mzee sharti umheshimu usoni pake kwa kumwogopa Mungu wako. Mimi ni Bwana.
33
Mgeni akikaa ugenini kwenu katika nchi yenu, msimwonee,
34
ila awe kwenu kama mwenyeji, ijapo ni mgeni akaaye ugenini kwenu. Mmpende, kama mnavyojipenda; kwani nanyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri. Mimi Bwana ni Mungu wenu.
35
Msifanye mapotovu wala mashaurini wala kwa kutumia vipimo vya kudanganya kama mizani au vibaba.
36
Sharti mtumie mizani ya sawasawa na vyuma vya kupimia vya sawasawa na pishi za sawasawa na visaga vya sawasawa. Mimi Bwana ni Mungu wenu aliyewatoa katika nchi ya Misri.
37
Yaangalieni maongozi yangu yote na maamuzi yangu, myafanye! Mimi ni Bwana.
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 20 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27