bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Leviticus 18
Leviticus 18
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 19 →
1
Bwana akamwambia Mose kwamba:
2
Sema na wana wa Isiraeli na kuwaambia: Mimi Bwana ni Mungu wenu.
3
Msifanye matendo kama yale ya nchi ya Misri, mlikokaa, wala msifanye matendo kama yale ya nchi ya Kanaani, nitakakowapeleka kukaa huko, wala msiyafuate maongozi yao.
4
Mtakapoyafanya maamuzi yangu na kuyaangalia maongozi yangu, myafuate, mimi Bwana nitakuwa Mungu wenu.
5
Kwa hiyo yaangalieni maongozi yangu! Naye mtu ye yote atakayeyafanya maamuzi yangu atapata uzima kwa njia hiyo, maana mimi ni Bwana.
6
Mtu ye yote asiingie kwa mwenziwe aliye ndugu yake wa kuzaliwa naye, amfunue uchi wake. Maana mimi ni Bwana.
7
Uchi wa baba yako wala uchi wa mama yako usiufunue; aliye mama yako usimfunue uchi wake.
8
Uchi wa mkewe baba yako usiufunue. Kwani ndio uchi wa baba yako.
9
Uchi wa umbu lako aliye binti baba yako au binti mama yako, kama amezaliwa nyumbani mwenu au nje, usiufunue uchi wao hao.
10
Uchi wa binti mwanao, wa kiume au wa kike, usifunue uchi wao hao, kwani ni uchi wako mwenyewe.
11
Uchi wake binti mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, usiufunue huo uchi wake, maana ni umbu lako.
12
Uchi wake umbu lake baba yako usiufunue, maana ni ndugu ya baba yako wa kuzaliwa naye.
13
Uchi wa ndugu ya mama yako usiufunue. Kwani ni ndugu ya mama yako wa kuzaliwa naye.
14
Uchi wa baba yako mkubwa au mdogo usiufunue, wala mkewe usimkaribie, maana ni mama yako.
15
Uchi wa mkweo aliye mke wa mwanao wa kiume usiufunue huo uchi wake.
16
Uchi wa mkewe mkubwa au mdogo wako usiufunue, maana ni uchi wa ndugu yako wa kuzaliwa naye.
17
Uchi wa mwanamke usiufunue pamoja nao wa mwanawe wa kike. Wala usimchukue binti mwanawe wa kiume wala binti mwanawe wa kike kuufunua uchi wake. Maana hao wanawake ni ndugu wa kuzaliwa pamoja; huo ndio uzinzi.
18
Wala usichukue mwanamke ukiwa na ndugu yake wa kike, umtie yule wivu kwa kuufunua uchi wake huyu siku zile, yule akiwa angaliko yu hai.
19
Usimkaribie mwanamke aliye mwenye uchafu kwa kuwa miezini, uufunue uchi wake.
20
Usiingie kwa mkewe mwenzako, ulale naye na kumpa mimba, usijipatie uchafu kwake.
21
Namo miongoni mwao walio wa uzao wako usitoe hata mmoja wa kumpa Moloki, wamwingize motoni, usipate kulichafua Jina la Mungu wako. Mimi ni Bwana.
22
Aliye wa kiume usilale naye, kama unavyolala na mwanamke, maana hayo ni matapisho.
23
Wala usije kulala na nyama ye yote ukijipatia uchafu kwake, wala mwanamke asisimame mbele ya nyama kupata mimba kwake; huo ndio uchafu mbaya zaidi.
24
Usijichafue kwa mambo hayo yote! Kwani kwa kuyafanya hayo yote walijichafua wamizimu wote, nitakaowafukuza mbele yenu.
25
Kwa kuwa nchi ilipata kuwa yenye uchafu, nitailipisha huu uovu wake, iwatapike waliokuwa wenyeji huko.
26
Lakini ninyi yaangalieni maongozi yangu na maamuzi yangu, msiyafanye hayo matapisho yote, wala ninyi mlio wenyeji wala wageni watakaokuwa kwenu.
27
Kwani matapisho hayo yote waliyafanya wao waliokuwako mbele yenu katika nchi hiyo, hata nchi ikapata kuwa yenye uchafu.
28
Nanyi mtakapoyafanya, nchi itawatapika kwa kuichafua, kama ilivyowatapika wamizimu waliokuwako mbele yenu.
29
Kwani wote watakaoyafanya matapisho hayo, basi, wao watakaoyafanya watang'olewa kwao walio ukoo wao.
30
Kwa hiyo yaangalieni, niliyowaambia, yanayowapasa kuyaangalia, msiyafuate na kuyafanya yale maongozi yatapishayo, yaliyofanywa mbele yenu, msijipatie uchafu kwa kuyafanya. Mimi Bwana ni Mungu wenu.
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 19 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27