bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Leviticus 5
Leviticus 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 6 →
1
Tena mtu anaweza kukosa hivi: akisikia shaurini sauti ya mwenye kuapiza, naye ni shahidi kwa kuliona lile jambo au kwa kulijua, basi, asipolieleza, atakuwa amekora manza zitakazomkalia.
2
Au hivi: mtu akigusa cho chote kisichotakata, kama ni mzoga wa nyama chafu wa porini au mzoga wa nyama chafu wa kufugwa au mzoga wa dudu chafu, asijue, ya kuwa amejipatia uchafu, basi, naye ni mwenye manza.
3
Au hivi: mtu akigusa uchafu wo wote wa mtu au kichafu cho chote, basi, hapo atakapokijua atakuwa ni mwenye manza.
4
Au hivi: mtu akiapa kwa upuzi wa midomo tu, kama ni kwamba kufanya mabaya au mema, kwa hayo yote, mtu anayoyaapa kwa kujipuza, asijue, ya kwamba amekosa, basi, hapo atakapoyajua atakuwa ni mwenye manza kwa kosa moja kama hilo kuliko mengine.
5
Na viwe hivyo: mtu, aliyekora manza kwa kosa moja kama hilo kuliko mengine, na aungame aliyoyakosea,
6
kisha ampelekee Bwana malipo ya manza zake, alizozikora kwa ajili ya kosa lake, alilolikosa, akitoa katika kundi lake jike la kondoo au la mbuzi kwa ajili ya kosa lake. Ndipo, mtambikaji atakapompatia upozi, aondolewe kosa lake.
7
Lakini mkono wake usipomfikilia kondoo, na ampelekee Bwana hua wawili au makinda mawili ya njiwa manga kuwa ng'ombe yake ya tambiko ya weuo kwa ajili ya hilo kosa, alilolikosa, mmoja wa weuo, mmoja wa kuteketezwa nzima.
8
Akiwapeleka kwa mtambikaji, huyo atatoa kwanza yule wa weuo akivunja kichwa chake hapo, kinaposhikamana na shingo, lakini hatakiondoa kabisa.
9
Nayo damu yake nyingine ya yule wa weuo atainyunyizia ukutani pake meza ya kutambikia, nyingine itakayosalia na imwagike misingini pake meza ya kutambikia. Hivyo ndivyo, anavyokuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo.
10
Yule wa pili atamfanya kuwa ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima kama desturi. Hivyo ndivyo, mtambikaji atakavyompatia upozi, aondolewe kabisa kosa lake, alilolikosa.
11
Lakini mkono wake usipowafikilia hua wawili au makinda mawili ya njiwa manga, basi, toleo lake, atakalopeleka, kwa kuwa alikosa, na liwe vibaba viwili na nusu vya unga mwembamba kuwa kipaji chake cha tambiko cha weuo; asiumiminie mafuta, wala asitie uvumba juu yake, kwani ndio kipaji cha tambiko cha weuo.
12
Akiupeleka kwa mtambikaji, huyo mtambikaji na achukue humo wa kulijaza gao lake, uwe wa kumkumbushia Bwana, akiuchoma moto hapo pa kutambikia juu ya mioto ya Bwana. Hivyo nao utakuwa kipaji cha tambiko cha weuo.
13
Hivyo ndivyo, mtambikaji atakavyompatia upozi kwa ajili ya kosa lake, alilolikosa kuliko mengine, aondolewe kabisa kosa lake; nao unga uliosalia utakuwa wake mtambikaji kama ule wa vilaji vya tambiko.
14
Bwana akamwambia Mose kwamba:
15
Mtu akilivunja Agano, akikosa kwa kuchukua kitu kilicho mali ya Bwana, asipovijua, na ampelekee Bwana ng'ombe yake ya tambiko ya upozi, akitoa katika kundi lake dume la kondoo asiye na kilema, unayemwona kuwa wa fedha mbili tatu zilizopimwa kwa kipimo cha Patakatifu; huyo atakuwa ng'ombe yake ya tambiko ya upozi.
16
Kisha nazo mali za Patakatifu, alizozikosea kwa kuzichukua, atazilipa na kuongeza fungu la tano; zote ampe mtambikaji. Ndipo, mtambikaji atakapompatia upozi na kumtoa yule dume la kondoo kuwa ng'ombe ya tambiko ya upozi, kisha ataondolewa kosa lake.
17
Hata mtu akikosea agizo lo lote la Bwana, ijapo ni moja tu, kwa kufanya yasiyofanywa, asipovijua, naye atakuwa amekora manza, nao uovu wake utamkalia.
18
Kwa hiyo na atoe katika kundi lake dume la kondoo asiye na kilema, unayemwona, ya kama anatosha kuwa ng'ombe ya tambiko ya upozi. Kisha ampeleke kwa mtambikaji, naye mtambikaji atampatia upozi kwa ajili ya kosa lake, alilolikosa pasipo kulijua kuwa ni kosa; naye akiwa hakuvijua kweli ataondolewa kosa lake.
19
Basi, hii ni ng'ombe ya tambiko ya upozi, kwa maana manza, alizozikora, alizikora kwake Bwana.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27