bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Leviticus 21
Leviticus 21
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 22 →
1
Bwana akamwambia Mose: Waambie watambikaji, wana wa Haroni, kwamba: Mtambikaji asijipatie uchafu kwa kugusa mfu kwao walio ukoo wake,
2
ila kwao tu walio ndugu zake wa kuzaliwa nao, maana ndio walio kwake karibu: mama yake na baba yake na mwanawe wa kiume na wa kike na mkubwa au mdogo wake,
3
hata umbu lake aliyezaliwa naye akiwa ni mwanamwali bado, asipokuwa bado na mwanamume, basi, hata kwake ataweza kujipatia uchafu.
4
Lakini kwa mwingine aliye wa ukoo wake, ijapo awe mkuu, asijipatie uchafu wa kuupoteza utakatifu wake.
5
Wasijinyoe vichwani kuwa wenye kipara, wala ndevu zao wasizikate pembenipembeni, wala wasijichore nembo miilini mwao.
6
Sharti wawe watakatifu wa Mungu wao, wasilibezeshe Jina la Mungu wao. Kwani ndio wanaozitoa ng'ombe za tambiko za kumteketezea Bwana, zilizo chakula chake Mungu wao, kwa hiyo sharti wawe watakatifu.
7
Mwanamke mgoni wasimchukue wala asiye mwenye macheo, wala mwanamke aliyefukuzwa na mumewe wasimchukue, kwani yeye ni mtakatifu wa Mungu wake.
8
Nawe sharti umwazie kuwa mtakatifu kwa kuwa yeye ndiye anayemtolea Mungu wako chakula chake, kwa hiyo awe mtakatifu kwako, kwani mimi Bwana ninayewatakasa ninyi ni mtakatifu.
9
Binti mtambikaji akianza kuzini humbezesha baba yake, kwa hiyo sharti ateketezwe kwa moto.
10
Naye aliye mtambikaji mkuu miongoni mwa ndugu zake aliyemiminiwa kichwani pake mafuta ya kumpaka, aliyejazwa gao lake, apate kuyavaa yale mavazi yampasayo, asiziache wazi nywele za kichwani pake, wala asizirarue nguo zake,
11
wala asiingie mo mote mwenye mfu ye yote, asijipatie uchafu, wala kwa baba yake wala kwa mama yake.
12
Asitoke Patakatifu, asipapatie Patakatifu pa Mungu wake uchafu, kwani amekwisha kuvikwa kilemba, ndio mafuta ya Mungu wake yaliyompaka. Mimi ni Bwana.
13
Naye mwanamke, atakayemchukua, sharti awe mwanamwali.
14
Asichukue mjane wala aliyefukuzwa na mumewe wala mgoni asiye mwenye macheo, ila achukue mwanamwali tu aliye wa ukoo wao, apate kuwa mkewe.
15
Ni kwamba: asiwatie uchafu walio wa uzao wake kwao walio ukoo wake, kwani mimi Bwana ndiye aliyemtakasa.
16
Bwana akamwambia Mose kwamba:
17
Mwambie Haroni kwamba: Mtu aliye wa vizazi vitakavyozaliwa nao walio wa uzao wako, kama ni mwenye kilema, asije kumtolea Mungu wake chakula chake.
18
Kila mtu mwenye kilema asinikaribie, kama ni kipofu au kiwete au mwenye pua mbaya au mwenye kiungo kilicho kirefu zaidi,
19
au kama ni mtu aliyevunjika mguu au mkono,
20
au kama ni mwenye nundu au mwenye kifua kikuu au mwenye chongo au mwenye upele mbaya au mwenye buba au mwenye mapumbu yaliyovunjika.
21
Kila mwenye kilema aliye wa uzao wake mtambikaji Haroni asije kumtolea Bwana ng'ombe za tambiko za kuteketezwa; kwa kuwa mwenye kilema asije kumtolea Mungu wake chakula chake.
22
Lakini kula ataweza kula chakula cha Mungu wake kilicho kitakatifu chenyewe nacho kilicho kitakatifu.
23
Asiingie tu hapo mbele ya lile pazia, wala asiijie meza ya kutambikia kwa kuwa mwenye kilema, asipapatie Patakatifu pangu uchafu. Kwani mimi ni Bwana anayepatakasa.
24
Nayo maneno haya Mose akamwambia Haroni na wanawe na watu wote wa Isiraeli.
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 22 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27