bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Leviticus 3
Leviticus 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 4 →
1
Kama toleo lake ni ng'ombe ya tambiko ya shukrani, aliyoitoa katika ng'ombe wake, kama ni wa kiume au wa kike, sharti apeleke asiye na kilema, apate kumtoa mbele ya Bwana.
2
Kisha aubandike mkono wake kichwani pake toleo lake, amchinje hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano, nayo damu wana wa Haroni walio watambikaji na wainyunyize pande zote juu ya meza ya kutambikia.
3
Kisha na atoe katika huyo ng'ombe aliyechinjwa kuwa ng'ombe ya tambiko ya shukrani vile vipande vya kumchomea Bwana kwa moto, ni mafuta yanayoufunika utumbo pamoja na mafuta yote yanayoshikamana na utumbo,
4
tena mafigo yake mawili pamoja na mafuta yanayoshikamana nayo penye nyama za viuno na kipande cha ini kilicho pamoja na mafigo; basi, haya yote na ayaondoe.
5
Kisha wana wa Haroni na wayachome moto mezani pa kutambikia juu ya ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima iliyowekwa juu ya kuni zilizopangwa motoni; huu ndio moto wenye mnuko wa kumpendeza Bwana.
6
Lakini kama ng'ombe yake ya tambiko, anayotaka kumtolea Bwana, ameitoa katika mbuzi au kondoo, kama ni wa kiume au wa kike, sharti apeleke asiye na kilema.
7
Kama anapeleka kondoo kuwa toleo lake, sharti ampeleke kumtoa mbele ya Bwana.
8
Kisha aubandike mkono wake kichwani pake toleo lake, amchinje mbele ya Hema la Mkutano, nayo damu yake wana wa Haroni na wainyunyize pande zote juu ya meza ya kutambikia.
9
Kisha na atoe katika kondoo aliyechinjwa kuwa ng'ombe ya tambiko ya shukrani vile vipande vya kumchomea Bwana kwa moto, ni mafuta yake: mkia wenye mafuta, wote mzima auondoe kwa kuukata hapo, ulipoungwa na mifupa ya mgongoni, tena yale mafuta yanayoufunika utumbo pamoja na mafuta yote yanayoshikamana na utumbo,
10
tena mafigo yake mawili pamoja na mafuta yanayoshikamana nayo penye nyama za viuno na kipande cha ini kilicho pamoja na mafigo; basi, haya yote na ayaondoe.
11
Kisha mtambikaji na ayachome moto mezani pa kutambikia; hivyo yatakuwa vilaji vya moto wa Bwana.
12
Lakini kama toleo lake ni mbuzi, sharti ampeleke kumtoa mbele ya Bwana.
13
Kisha aubandike mkono wake kichwani pake, amchinje mbele ya Hema la Mkutano, nayo damu yake wana wa Haroni na wainyunyize pande zote juu ya meza ya kutambikia.
14
Kisha na atoe katika hilo toleo lake vile vipande vya kumchomea Bwana kwa moto: mafuta yanayoufunika utumbo pamoja na mafuta yote yanayoshikamana na utumbo,
15
tena mafigo yake mawili pamoja na mafuta yanayoshikamana nayo penye nyama za viuno na kipande cha ini kilicho pamoja na mafigo; basi, haya yote na ayaondoe.
16
Kisha mtambikaji na ayachome moto mezani pa kutambikia; hivyo yatakuwa vilaji vya moto vyenye mnuko unaopendeza. Mafuta yote ni yake Bwana.
17
Huu ndio mwiko wa vizazi vyenu wa kale na kale mahali po pote, mtakapokaa: msile mafuta yo yote wala damu yo yote!
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27