bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Leviticus 7
Leviticus 7
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 8 →
1
Nayo haya ndiyo maongozi ya ng'ombe za tambiko za upozi: ni takatifu zenyewe.
2
Mahali hapo, wanapozichinja ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, papo hapo na wazichinje nazo ng'ombe za tambiko za upozi, nazo damu zao na azinunyize pande zote juu ya meza ya kutambikia.
3
Nayo mafuta yote ayatoe humo, ayapeleke: mkia na mafuta yanayoufunika utumbo,
4
nayo mafigo yote mawili pamoja na mafuta yanayoshikamana nayo penye nyama za viuno na kipande cha ini kilicho pamoja na mafigo; basi, haya yote na ayaondoe.
5
Kisha mtambikaji na ayachome moto mezani pa kutambikia kuwa moto wa Bwana. Hii ndiyo ng'ombe ya tambiko ya upozi.
6
Watambikaji wote walio wa kiume na wazile nyama zake; nazo ziliwe mahali patakatifu, maana nazo ni takatifu zenyewe.
7
Mambo ya ng'ombe za tambiko za weuo yalivyo, ndivyo, nayo ya ng'ombe za tambiko za upozi yalivyo, maongozi yao ni yayo hayo: nyama zitakuwa zake mtambikaji yule aliyempatia upozi mwenye ng'ombe.
8
Naye mtambikaji akipeleka ng'ombe ya tambiko ya mtu ya kuteketezwa nzima, ngozi ya hiyo ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima itakuwa yake mtambikaji yule aliyeipeleka.
9
Navyo vilaji vyote vya tambiko vinavyookwa jikoni, navyo vyote vilivyotengenezwa chunguni au kangoni vitakuwa vyake mtambikaji yule aliyevipeleka.
10
Navyo vilaji vyote vya tambiko vilivyochanganywa na mafuta navyo vilivyo vikavu vitakuwa vyao wana wote wa Haroni, wavitumie kila mtu na ndugu yake.
11
Haya ndiyo maongozi ya ng'ombe za tambiko za shukrani, mtu atakazomtolea Bwana:
12
Mtu akiitoa kuwa ya sifa, na aitoe hiyo ng'ombe ya tambiko ya sifa pamoja na vikate visivyochachwa, vilivyochanganywa na mafuta, na unga mwembamba wa vitumbua wa kutengeneza vikate vilivyochanganywa na mafuta.
13
Hili toleo lake alipeleke pamoja na mikate ilivyochachwa na pamoja na ng'ombe yake ya tambiko ya shukrani, atakayoitoa kuwa ya sifa.
14
Katika hayo matoleo yote na atoe moja la kumnyanyulia Bwana; nalo ni lake mtambikaji yule atakayeinyunyiza damu ya ng'ombe ya tambiko ya shukrani.
15
Nazo nyama za hiyo ng'ombe ya tambiko ya shukrani iliyo ya sifa na ziliwe siku hiyo ya kutolewa kwake, wasiziweke mpaka kesho.
16
Akiitoa hiyo ng'ombe yake ya tambiko kwa ajili ya kiapo au kwa mapenzi yake mwenyewe, nyama zake hiyo ng'ombe ya tambiko na ziliwe siku hiyo ya kutolewa kwake, hata kesho yake masao yake yatalika.
17
Lakini nyama za hiyo ng'ombe ya tambiko zitakazosazwa mpaka siku ya tatu sharti ziteketezwe kwa moto.
18
Kama nyama za ng'ombe yake ya tambiko ya shukrani zingeliwa siku ya tatu, mwenye kuitoa asingependeza, wala asingewaziwa kuwa mwenye kuitoa, ila zitakuwa machukizo tu, naye kila mtu atakayezila atakuwa amekora manza.
19
Nazo nyama zilizogusana nacho cho chote kilicho kichafu zisiliwe, ila ziteketezwe kwa moto. Nyama nyingine za tambiko kila atakataye atazila hizo nyama.
20
Lakini kila mtu atakayekula nyama za ng'ombe ya tambiko ya shukrani zilizo zake Bwana, akiwa mwenye uchafu, basi, roho yake huyo mtu na ing'olewe, atoweke kwenye watu wa kabila lake.
21
Tena mtu akigusa cho chote chenye uchafu, kama ni mtu aliye na uchafu wake au nyama chafu au tapisho lo lote linalochafua, naye akila nyama za ng'ombe ya tambiko ya shukrani zilizo zake Bwana, basi, roho yake huyo mtu na ing'olewe, atoweke kwenye watu wa kabila lake.
22
Bwana akamwambia Mose kwamba:
23
Waambie wana wa Isiraeli kwamba: Mafuta yote ya ng'ombe na ya kondoo na ya mbuzi msiyale!
24
Tena mafuta ya nyama aliyekufa kibudu nayo mafuta ya nyama aliyeraruliwa na nyama mwingine mtayatumia ya kazi yo yote, lakini kula msiyale!
25
Kwani kila atakayekula mafuta ya nyama, watu wanayomtolea Bwana kuchomwa motoni, basi, roho yake huyo mtu aliyeyala na ing'olewe, atoweke kwenye watu wa kabila lake.
26
Nazo damu zote pia msizile mahali po pote, mtakapokaa, wala za ndege wala za nyuma.
27
Kila mtu atakayekula damu zo zote roho yake na ing'olewe, atoweke kwenye watu wa kabila lake.
28
Bwana akamwambia Mose:
29
Waambie wana wa Isiraeli kwamba: Atakayemtolea Bwana ng'ombe yake ya tambiko ya shukrani sharti ampelekee Bwana toleo lake, alilolitoa katika hiyo ng'ombe yake ya tambiko ya shukrani.
30
Mikono yake mwenyewe na iyapeleke yatakayochomwa kwa moto wa Bwana, ni mafuta pamoja na kidari; akiyapeleka haya, kidari na wakipitishe motoni mbele ya Bwana, kiwe kipaji cha tambiko cha kupitishwa motoni.
31
Kisha mtambikaji na ayachome moto yale mafuta mezani pa kutambikia, lakini kidari kitakuwa chao Haroni na wanawe.
32
Nayo mapaja ya kuume ya ng'ombe zenu za tambiko za shukrani sharti mwape watambikaji kuwa vipaji vya tambiko vya kunyanyuliwa.
33
Atakayetoa damu za ng'ombe za tambiko za shukrani pamoja na mafuta yao miongoni mwa wana wa Haroni, basi, lile paja la kuume ni fungu lake yeye, atakalolipata.
34
Kwani vidari vya kupitishwa motoni na mapaja ya kunyanyuliwa ninayachukua kwa wana wa Isiraeli katika ng'ombe zao za tambiko za shukrani, nimpe mtambikaji Haroni na wanawe kuwa haki yao ya kale na kale kwao wana wa Isiraeli.
35
Haya ndiyo, Haroni na wanawe watakayoyapata kwenye mioto ya Bwana kwa hivyo, walivyopakwa mafuta; Bwana aliwagawia haya siku ile, alipowatoa kuwa watambikaji wake.
36
Siku ile, Bwana alipowapaka mafuta, aliwaagiza wana wa Isiraeli, wawape haya, nayo ni haki ya kale na kale ya vizazi vyao.
37
Haya ndiyo malinganyo ya kutumia ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na vilaji vya tambiko na ng'ombe za tambiko za weuo na za upozi na za kujazwa gao nazo ng'ombe za tambiko za shukrani.
38
Ndiyo, Bwana aliyomwagiza Mose mlimani kwa Sinai siku ile, alipowaagiza wana wa Isiraeli kumtolea Bwana matoleo yao katika nyika ya Sinai.
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27