bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Leviticus 20
Leviticus 20
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 21 →
1
Bwana akamwambia Mose kwamba:
2
Waambie wana wa Isiraeli: Mtu ye yote, kama ni mwana wa Isiraeli au kama ni mgeni akaaye ugenini kwao Waisiraeli atakayetoa hata mmoja tu miongoni mwao walio wa uzao wake na kumpa Moloki sharti auawe, watu wa nchi hiyo sharti wamtupie mawe.
3
Nami nitamkazia macho mtu aliye hivyo, nimng'oe katikati yao walio ukoo wake, kwani miongoni mwao walio wa uzao wake ametoa mtu wa kumpa Moloki, kusudi apapatie Patakatifu pangu uchafu, alibezeshe nalo Jina langu takatifu.
4
Ijapo watu wa nchi hiyo wayapofushe macho yao, wakiyaona, mtu yule aliyoyafanya alipotoa mtu miongoni mwao walio wa uzao wake na kumpa Moloki, wasipate kumwua,
5
mimi na nimkazie macho yangu mtu aliye hivyo nao walio wa kizazi chake, nimng'oe yeye pamoja nao wote waliomfuata na kuufanya ugoni wake wa kumfuata Moloki kufanya ugoni naye, basi, na niwang'oe, watoweke katikati yao walio ukoo wao.
6
Hata mtu akiwageukia waganga wa kutiisha mizimu na waaguaji, kufanya ugoni nao, na nimkazie macho yangu aliye hivyo, na nimg'oe katikati yao walio ukoo wake.
7
Kwa hiyo jitakaseni, mpate kuwa watakatifu! Kwani mimi Bwana ni Mungu wenu.
8
Yaangalieni maongozi yangu, myafanye! Mimi ni Bwana anayewatakasa ninyi.
9
Mtu ye yote atakayemwapiza baba yake au mama yake sharti auawe kabisa; akimwapiza baba yake au mama yake atakuwa amekora manza za kumwagwa damu yake.
10
Mtu akizini na mke wa mwingine, basi, yeye aliyezini na mke wa mwenzake sharti auawe, mwenyewe pamoja na mwanamke, aliyezini naye.
11
Mtu atakayelala na mkewe baba yake atakuwa ameufunua uchi wake baba yake; kwa hiyo wote wawili sharti wauawe, maana wamekora manza za kumwagwa damu zao.
12
Mtu akilala na mke wa mwanawe, sharti wauawe wote wawili, maana wamefanya uchafu ulio mbaya zaidi, nao wamekora manza za kumwagwa damu zao.
13
Mtu akilala na mwanamume mwingine, kama wanavyolala na mwnamke, wamefanya tapisho, wote wawili sharti wauawe, maaana wamekora manza za kumwagwa damu zao.
14
Mtu akimchukua mwanamke pamoja na mama yake, ni ugoni, sharti wamteketeze kwa moto pamoja nao wale wanawake, ugoni ulio hivyo usiwe kwenu.
15
Mtu akilala na nyama sharti auawe, hata huyo nyama sharti mmwue.
16
Mwanamke akimkaribia nyama ye yote kulala naye, sharti mmwue huyo mwanamke pamoja na huyo nyama, wafe kabisa, maana wamekora manza za kumwagwa damu zao.
17
Mtu akimchukua umbu lake aliye binti baba yake au binti mama yake, auone uchi wake, naye auone uchi wake yeye mwenyewe, ni tendo litwezalo, nao sharti wang'olewe machoni pao walio wana wa ukoo wao, maana ameufunua uchi wa umbu lake; hizi manza, alizozikora, zitamkalia.
18
Mtu akilala na mwanamke aliye miezini, akiufunua uchi wake na kukitokeza waziwazi kijito chake, naye mwanamke akikifunua kijito cha damu yake, wote wawili sharti wang'olewe katikati yao walio ukoo wao.
19
Uchi wa mama yako mkubwa na mdogo nao uchi wa shangazi yako usiufunue, kwani ni kuutokeza waziwazi uchi wao walio ndugu wa kuzaliwa nao; hizo manza, walizozikora, zitawakalia.
20
Mtu akilala na mkewe baba yake mkubwa au mdogo, ameufunua uchi wa baba yake mkubwa au mdogo, nao huu ukosaji wao utawakalia, wafe pasipo kuzaa watoto.
21
Mtu akimchukua mkewe mkubwa au mdogo wake, ni uchafu, maana ameufunua uchi wa ndugu yake wa kuzaliwa naye, nao watakufa pasipo kuzaa watoto.
22
Yaangalieni maongozi yangu yote na maamuzi yangu yote, myafanye, ile nchi isiwatapike, nitakapowapeleka, mkae huko.
23
Msiyafuate maongozi ya wamizimu, nitakaowafukuza mbele yenu. Kwa kuwa waliyafanya hayo makosa yote, nalichukizwa nao.
24
Kwa hiyo niliwaambia ninyi: Ninyi mtaichukua nchi yao, iwe yenu, mimi nitawapa kuichukua hiyo nchi ichuruzikayo maziwa na asali. Mimi ni Bwana Mungu wenu niliyewatenga na kuwatoa katika makabila mengine.
25
Nanyi mwapambanue nyama wenye kutkata nao wenye uchafu, nao ndege wenye uchafu nao wenye kutakata, msijifanye wenyewe kuwa tapisho kwa ajili ya nyama na ndege, wala kwa ajili ya wadudu wote watambaao katika nchi, niliowatenga kuwa kwenu wenye uchafu.
26
Ndipo, mtakapokuwa watakatifu wangu, kwani mimi Bwana ni mtakatifu, nikawatenga ninyi na kuwatoa katika makabila yote, mwe wangu.
27
Mtu mume au mke akiwa mwenye roho ya kutiisha mizimu au mwenye roho ya kuagua sharti wauawe kwa kupigwa mawe, maana wamekora manza za kuuawa.
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 21 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27