bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Leviticus 24
Leviticus 24
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 25 →
1
Bwana akamwambia Mose kwamba:
2
Waagize wana wa Isiraeli, wakupatie mafuta ya chekele yaliyotwangwa vema kuwa safi ya kinara ya kutia siku zote katika taa zake.
3
Hapo nje ya pazia penye Sanduku la Ushahidi katika Hema la Mkutano Haroni azitengeneze hizo taa, ziwake tangu jioni hata asubuhi mbele ya Bwana pasipo kukoma. Maongozi haya na yawe ya kale na kale kwa vizazi vyenu.
4
Penye kile kinara cha dhahabu tupu na azitengeneze taa zake, ziwake mbele ya Bwana siku zote.
5
Tena uchukue unga mwembamba, uuoke kuwa mikate kumi na miwili, kila mikate mmoja uwe wa pishi moja ya unga.
6
Kisha uiweke mistari miwili, kila mstari wenye mikate sita, juu ya meza ya dhahabu tupu mbele ya Bwana.
7
Kisha uweke juu ya kila mstari uvumba ulio safi, uwe moto wa kumpendeza Bwana na kumkumbusha hiyo mikate.
8
Kila siku ya mapumziko sharti aitengeneze tena mbele ya Bwana pasipo kukoma. Hili na liwe agano la kale na kale nao wana wa Isiraeli, wasiache kuitoa.
9
Kisha hiyo mikate itakuwa yao Haroni na wanawe, nao sharti waile mahali patakatifu. Kwa kuwa mitakatifu yenyewe sharti iwe fungu lao litokalo kwenye mioto ya Bwana. Hii na iwe haki yao ya kale na kale.
10
Ikawa, mwana wa mwanamke wa Kiisiraeli mwenye baba wa Kimisri alipotokea katikati ya wana wa Isiraeli, huyu mwana wa mwanamke wa Kiisiraeli akagombana na mtu wa Kiisiraeli makambini.
11
Naye yule mwana wa mwanamke wa Kiisiraeli akalitukana Jina la Bwana pamoja na kuliapiza. Ndipo, walipompeleka kwa Mose, nalo jina la mama yake lilikuwa Selomiti, binti Diburi, wa shina la Dani.
12
Wakamweka kifungoni, wapate kuelezwa, kinywa cha Bwana kitakavyowaambia.
13
Bwana akamwambia Mose kwamba:
14
Huyo mwenye kutukana mtokeze nje ya malago, kisha wote walioyasikia na wambandikie mikono yao kichwani pake, kisha watu wote wa mkutano huu na wamwue kwa kumpiga mawe.
15
Lakini wana wa Isiraeli waambie kwamba: Mtu ye yote atakayemwapiza Mungu wake sharti alipishwe hilo kosa lake.
16
Atakayelitukana Jina la Bwana sharti auawe kabisa, watu wote wa mkutano huu wakimpiga mawe. Kama ni mgeni au kama ni mwenyeji, kwa kulitukana hilo Jina hana budi kuuawa.
17
Mtu akimpiga mwenzake, afe, sharti auawe naye.
18
Lakini akipiga nyama, naye akifa, sharti amlipe, nyama aliye mzima kwa yule aliyekufa.
19
Mtu akimwumiza mwenziwe, apate kilema, naye sharti afanyiziwe yaleyale, aliyoyafanya:
20
kidonda kwa kidonda, jicho kwa jicho, jino kwa jino. Kilema, alichompatia mwenzake, apatiwe naye.
21
Ni hivi: mtu atakayempiga nyama, naye akifa, sharti amlipe; lakini mtu atakayempiga mwenziwe, naye akifa, sharti auawe.
22
Hukumu za kwenu sharti ziwe moja, mwenye kuhukumiwa kama ni mgeni au kama ni mwenyeji. Kwani mimi Bwana ni Mungu wenu.
23
Mose alipokwisha kuwaambia wana wa Isiraeli maneno haya, wakamtokeza yule mwenye kutukana nje ya makambi, wakamwua kwa kumpiga mawe; wana wa Isiraeli wakafanya, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 25 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27