bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Leviticus 9
Leviticus 9
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 10 →
1
Siku ya nane Mose akamwita Haroni nao wanawe na wazee wa Isiraeli,
2
akamwambia Haroni: Jichukulie ndama dume, awe ng'ombe ya tambiko ya weuo, tena dume la kondoo, awe ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima, wote wawili wawe pasipo kilema, uwatoe mbele ya Bwana.
3
Nao wana wa Isiraeli waambie kwamba: Chukueni dume la mbuzi, awe ng'ombe za tambiko ya weuo, tena ndama na mwana kondoo wa mwaka mmoja wasio na kilema, wawe ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima.
4
Tena chukueni dume la ng'ombe na la kondoo, wawe ng'ombe z tambiko za shukrani wa kuwachinja mbele ya Bwana na vilaji vya tambiko vilivyochanganywa na mafuta. Kwani leo Bwana atawatokea ninyi.
5
Wakayachukua yote, Mose aliyowaagiza, wakayapeleka hapo mbele ya Hema la Mkutano; nao mkutano wote ulipokuja, wakasimama mbele ya Bwana.
6
Mose akasema: Hili ndilo neno, Bwana aliloliagiza, mlifanye, utukufu wa Bwana uwatokee.
7
Kisha Mose akamwambia Haroni: Ikaribie meza ya kutambikia, utengeneze ng'ombe yako ya tambiko ya weuo nayo ya kuteketezwa nzima, ujipatie upozi mwenyewe! Tena kwa ajili ya watu nao litengeneze nalo toleo lao hawa watu, uwapatie upozi nao, kama Bwana alivyoyaagiza!
8
Ndipo, Haroni alipoikaribia meza ya kutambikia, akamchinja ndama wake wa kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo.
9
Nao wanawe Haroni wakampelekea hiyo damu, naye akakichovya kidole chake katika damu, akazipaka pembe za meza ya kutambikia, nayo damu nyingine akaimwagia misingi ya meza ya kutambikia.
10
Nayo mafuta na mafigo na kile kipande cha ini cha hiyo ng'ombe ya tambiko ya weuo akayachoma moto mezani pa kutambikia, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
11
Nazo nyama na ngozi akaziteketeza kwa moto nje ya makambi.
12
Tena alipomchinja ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima, wanawe Haroni wakampelekea hiyo damu, naye akainyunyiza pande zote juu ya meza ya kutambikia.
13
Hiyo ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ilipokwisha kuchanguliwa, wakampelekea vipande vyake pamoja na kichwa, naye akavichoma moto mezani pa kutambikia.
14
Alipokwisha kuuosha utumbo na miguu akaichoma moto juu ya hiyo ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima mezani pa kutambikia.
15
Kisha akayatoa matoleo ya watu. Akamchukua dume la mbuzi aliye ng'ombe ya tambiko ya weuo ya watu, akamchinja na kumtoa kama yule wa kwanza, awe ng'ombe ya tambiko ya weuo.
16
Akaitoa nayo ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima, akaifanya kama desturi.
17
Alipovitoa vilaji vya tambiko akalijaza gao lake humo, akavichoma moto mezani pa kutambikia penye ng'ombe ya tambiko ya asubuhi ya kuteketezwa nzima.
18
Kisha akamchinja dume la ng'ombe na dume la kondoo walio ng'ombe za tambiko za shukrani za watu, nao wanawe Haroni wakampelekea hizo damu, akazinyunyiza pande zote juu ya meza ya kutambikia.
19
Nayo mafuta ya dume la ng'ombe, nayo ya dume la kondoo: mkia nayo yaufunikayo utumbo na mafigo na kile kipande cha ini,
20
haya mafuta wakayaweka juu ya vidari, naye Haroni akayachoma moto haya mafuta mezani pa kutambikia.
21
Lakini kidari na paja la kuume Haroni akavipitisha motoni huku na huko kuwa vipaji vya tambiko vya kupitishwa motoni mbele ya Bwana, kama Mose alivyoagiza.
22
Kisha Haroni akawainulia watu mikono yake, akawabariki. Alipokwisha akashuka na kutoka hapo, alipozitoa ng'ombe za tambiko za weuo na za kuteketezwa nzima na za shukrani.
23
Kisha Mose na Haroni wakaingia Hemani mwa Mkutano; napo walipotoka wakawabariki hao watu, ndipo, utukufu wa Bwana ulipowatokea watu wote.
24
Moto ukatoka mbele ya Bwana, ukaila juu ya meza ya kutambikia ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima pamoja na yale mafuta. Watu wote walipoviona wakapiga shangwe na kuanguka kifudifudi.
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 10 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27