bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Leviticus 17
Leviticus 17
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 18 →
1
Bwana akamwambia Mose kwamba:
2
Sema na Haroni na wana wote wa Isiraeli, uwaambie: Hili ni neno, aliloliagiza Bwana kwamba:
3
Mtu ye yote wa mlango wa Isiraeli atkayechinja ng'ombe au kondoo au mbuzi makambini au atakayemchinja nje ya makambi,
4
asimpeleke pa kuliingilia Hema la Mkutano, amtolee Bwana toleo la tambiko mbele ya Kao lake Bwana, mtu huyu na awaziwe kuwa mwenye manza za damu: kwa kuwa alimwaga damu, sharti ang'olewe mtu huyu katikati yao walio ukoo wake.
5
Ni kwamba: ng'ombe zao za tambiko, wanazozichinja maporini, wana wa Isiraeli sharti wampelekee Bwana hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano na kumpa mtambikaji, ndipo wazichinje kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani za Bwana.
6
Nazo damu mtambikaji na azinyunyize juu ya meza ya kumtambikia Bwana hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano, nayo mafuta na ayateketeze kuwa moshi wenye mnuko wa kumpendeza Bwana.
7
Ng'ombe zenu za tambiko msizitolee tena mashetani, mnaowwafuata kufanya ugoni nao. Haya sharti yawe kwao maongozi ya kale na kale ya kuongoza vizazi na vizazi vya kwao.
8
Tena uwaambie: Mtu ye yote wa mlango wa Isiralei, hata mgeni atakayekaa kwao, atakayetoa ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima au ng'ombe nyingine ya tambiko,
9
asipoipeleka pa kuliingilia Hema la Mkutano kuiteketeza hapo, iwe ng'ombe ya tambiko ya Bwana, mtu huyu sharti ang'olewe kwao walio wa ukoo wake.
10
Mtu ye yote wa mlango wa Isiraeli, hata mgeni atakayekaa kwao, atakayekula damu yo yote, mtu huyu atakayekula damu nitamkazia macho yangu, nimng'oe katikati yao walio ukoo wake.
11
Kwani roho ya mwili imo katika damu, nami niliwapa damu, mzipeleke mezani pa kutambikia, ziwapatie upozi ninyi wenyewe, kwani damu humpatia mtu upozi, kwa kuwa roho imo.
12
Kwa hiyo nimewaambia wana wa Isiraeli: Atakayekaa kwenu asile damu, wala mgeni atakayekaa kwenu asile damu!
13
Mtu ye yote aliye wa wana wa Isiraeli naye mgeni atakayekaa kwao, akiwinda nyama au ndege anayelika, sharti aimwage damu yake na kuifunika kwa mchanga.
14
Kwani roho ya kila mwenye mwili ni damu yake, maana humu ndimo, roho yake ilimo; kwa hiyo nimewaambia wana wa Isiraeli: Msile damu zao wo wote walio wenye miili! Kwani roho ya kila mwenye mwili ni damu yake, naye kila atakayeila sharti ang'olewe.
15
Tena kila atakayekula kibudu au nyama aliyeraruliwa na nyama mwingine, kama ni mwenyeji au kama ni mgeni, sharti azifue nguo zake na koga majini, naye atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni, kisha atakuwa ametakata.
16
Lakini asipozifua nguo zake, wala asipouogesha mwili wake majini, atakuwa amekora manza zitakazomkalia.
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 18 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27