bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Leviticus 11
Leviticus 11
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 12 →
1
Bwana akasema na Mose na Haroni, akawaambia:
2
Waambieni wana wa Israeli kwamba: Katika nyama wote walioko nchini mtakula hawa wenye miguu minne:
3
wote wenye kwato zilizopasuka na kutengeka kabisa, kama ni wenye kucheua, mtawala.
4
Lakini miongoni mwao wenye kucheua wapasukao kwato msiwale hawa: Ngamia; kweli anacheua, lakini hazipasui kwato zake vema, kwa hiyo ni mwiko kwenu.
5
Pelele; naye anacheua, lakini hazipasui kwato, kwa hiyo ni mwiko kwenu.
6
Sungura; naye anacheua, lakini hazipasui kwato, kwa hiyo ni mwiko kwenu.
7
Nguruwe; kweli anazipasua kwato na kuzitenga kabisa, lakini hacheui, kwa hiyo ni mwiko kwenu.
8
Nyama zao hao msizile, nayo mizoga yao msiiguse! kwani wao ni mwiko kwenu.
9
Katika nyama wote waliomo majini mtakula hawa: wote wenye mapezi na magamba waliomo majini baharini na mitoni mtawala.
10
Lakini wote wasio wenye mapezi na magamba waliomo baharini na mitoni miongoni mwao viumbe vyote vinavyotembea majini namo miongoni mwao nyama wote waliomo majini na wawe tapisho kwenu.
11
Kweli na wawe tapisho kwenu! Nyama zao msizile, nayo mizoga yao na mwione kuwa tapisho;
12
wote waliomo majini wasio wenye mapezi na magamba wawe tapisho kwenu.
13
Namo katika ndege wamo, mtakaowaona kuwa tapisho, hawaliki kwa kuwa tapisho: kozi na pungu na furukombe,
14
na tumbuzi na mwewe na ndugu zake,
15
na makunguru yote na ndugu zao,
16
na mbuni na kinega na dudumizi na kipanga na ndugu zake,
17
na mumbi na shakwe na bundi,
18
na yangeyange na korwa na tai,
19
na korongo na kitwitwi na ndugu zake na hudihuda na popo.
20
Wadudu wote wenye mabawa wanaokwenda kwa miguu minne wawe tapisho kwenu.
21
Katika wadudu wote wenye mabawa wanaokwenda kwa miguu minne mtawala wao tu walio wenye miguu miwili mirefu ya kurukia nchini inayokaa penye miguu yao mingine juu kidogo.
22
Mtakaowala miongoni mwao, ndio panzi na ndugu zao na nzige na ndugu zao na senene na ndugu zao na funutu na ndugu zao.
23
Lakini wadudu wote wengine wenye mabawa wanaokwenda kwa miguu minne wawe tapisho kwenu.
24
Kwao hao mtajipatia uchafu; kila atakayegusa mizoga yao atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
25
Naye kila atakayechukua mzoga wao mmoja miongoni mwao sharti azifue nguo zake, naye atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
26
Kila nyama mwenye kwato zilizopasuka pasipo kutengeka kabisa nao wasiocheua ndio walio wachafu kwenu; kila atakayewagusa atakuwa mwenye uchafu.
27
Nao nyama wote wenye miguu minne wanaokanyaga kwa nyayo ndio walio wachafu kwenu; kila atakayegusa mizoga yao atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
28
Naye atakayechukua mizoga yao sharti azifue nguo zake, naye atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni. Hao ndio walio wachafu kwenu.
29
Tena katika nyama wadogo wanaotambaa juu ya nchi ndio hawa watakaokuwa wachafu kwenu: Fuko na panya ma mjusi na ndugu zao:
30
guruguru na kenge na mbulu na goromoha na kinyonga.
31
Hawa ndio walio wachafu kwenu katika nyama watambaao. Kila atakayewagusa wakiisha kufa atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
32
Hata kila kitu, hawa watakachokiangukia wakifa, kitakuwa chenye uchafu kama ni chombo chochote cha mti au nguo au ngozi au gunia. Nacho kila chombo kinachotumiwa cha kufanyizia kazi kitiwe majini, nacho kitakuwa chenye uchafu mpaka jioni; ndipo, kitakapokuwa kimetakata tena.
33
Lakini kila chombo cha udongo, ambacho mmoja wao ataanguka ndani yake, sharti wakivunje, nayo yote yaliyomo yatakuwa yenye uchafu.
34
Vilaji vyote vinavyoliwa vikiingiwa na maji kama hayo ni vyenye uchafu; navyo vinywaji vyote vinavyonywewa vikiwa katika chombo kama hicho ni vyenye uchafu.
35
Nacho cho chote, mzoga mmoja tu miongoni mwao utakachokiangukia, ni chenye uchafu; kama ni jiko la kuchomea mikate au la kupikia, sharti libomolewe, maana ni lenye uchafu, hata kwenu sharti liwe lenye uchafu.
36
Lakini chemchemi na mashimo, maji yalimokusanyika, yatakuwa yametakata; lakini atakayeigusa mizoga yao akiyatoa humo atakuwa mwenye uchafu.
37
Tena kama mzoga mmoja miongoni mwao utaangukia mbegu zo zote za kupanda, watu wanazotaka kuzipanda, zitakuwa zimetakata.
38
Lakini kama mzoga mmoja miongoni mwao utaziangukia hizo mbegu, zikiisha lowekwa, sharti ziwe chafu kwenu.
39
Tena mmoja wao hao nyama, mnaowala, akifa, atakayeugusa mzoga wake atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
40
Atakayekula nyama ya mzoga wake sharti azifue nguo zake, tena atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni. Naye atakayeuchukua mzoga wake sharti azifue nguo zake, tena atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
41
Nyama wadogo wanaotambaa juu ya nchi wote pia wawe tapisho kwenu, wasiliwe.
42
Wote wanaojikokota tumboni nao wote wanaokwenda kwa miguu minne nao wote wenye miguu mingi zaidi, wale wadudu wote wanaotambaa juu ya nchi msiwale, kwani ndio tapisho.
43
Msijifanye wenyewe kuwa tapisho kwa ajili ya hao wadudu watambaao, wala msijipatie uchafu kwa ajili yao mkichafuliwa nao.
44
Kwani mimi ni Bwana, Mungu wenu, kwa hiyo sharti mjitakase, mwe watakatifu, kwani mimi ni mtakatifu. Msijipatie uchafu wenyewe kwao hao wadudu wote wanaotambaa juu ya nchi.
45
Kwani mimi ndiye Bwana aliyewatoa ninyi katika nchi ya Misri na kuwapandisha kuja huku, niwe Mungu wenu; kwa hiyo sharti mwe watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu!
46
Haya ndiyo maonyo ya kufundisha mambo ya nyama na ya ndege na ya viumbe vyote vyenye uzima vinavyotembea majini na ya wadudu wote watambaao juu ya nchi,
47
mpate kuwapambanua walio wachafu nao wanaotakata, ndio nyama wanaoliwa nao wasioliwa.
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 12 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27